Hesperian Health Guides
Uzazi wa mpango baada ya utoaji mimba
HealthWiki > Pale ambapo Wanawake hawana Daktari > Sura ya 15: Utoaji mimba na matatizo yanayotokana na utoaji mimba > Uzazi wa mpango baada ya utoaji mimba
|
|
|
|
|
|
Kuna uwezekano mkubwa kwamba mwanamke au msichana ambaye ametolewa mimba hakutaka kuupata ujauzito huo. Huu ni muda mzuri kumpatia taarifa juu ya njia za uzazi wa mpango na upatikanaji wake.
- Mwanamke kufunga kizazi: Kama ujauzito wako ulikuwa chini ya miezi 3, unaweza kufanyiwa huduma ya kufunga kizazi wakati wa utoaji mimba au mara baada ya hapo. Ni muhimu sana kufikiri kwa makini kabla ya kufikia uamuzi huu. Kufunga kizazi ni hali ya kudumu ambayo inamaanisha kwamba hutaweza kuzaa tena.
- Mwanaume kufunga uzazi: Ufungaji uzazi kwa mwanaume unaweza kufanyika wakati wote na ni hali ya kudumu. Uamuzi huu unahitaji kuufikiria kwa makini.
- Kondom: Wewe na mwenzi wako mnaweza kutumia kondom mara mtakapoamua kufanya ngono tena. Kondom pia hukinga dhidi ya maambukizi kupitia ngono, vikiwemo VVU.
- Dawa za kuua mbegu za kiume: Unaweza kutumia dawa za kuua mbegu za kiume mara utakapofanya ngono tena. Usitumie dawa za kuua mbegu za kiume kama una VVU, au una wenzi wengi.
- Diaframu: Kama hakukuwa na maambukizi au majeraha, unaweza kufungwa diaframu baada ya utoaji mimba.
Kwa taarifa zaidi juu ya njia zote hizi, angalia sura juu ya “Uzazi wa mpango.”
|
Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Mei 2017