Hesperian Health Guides
Nini cha kutarajia baada ya kutoa mimba?
HealthWiki > Pale ambapo Wanawake hawana Daktari > Sura ya 15: Utoaji mimba na matatizo yanayotokana na utoaji mimba > Nini cha kutarajia baada ya kutoa mimba?
Hedhi ya kawaida ya kila mwezi inapaswa kuanza tena kati ya wiki 4 hadi 6 baada ya kutoa mimba. Lakini unaweza kupata ujauzito tena baada ya siku 11.
Baada ya kutoa mimba, dalili za ujauzito kama vile kichefuchefu na maziwa kuuma, zinapaswa kutoweka ndani ya siku 1. Kama hazitatoweka, inamaanisha unaweza kuwa bado na ujauzito, aidha kwenye mji wa mimba au kwenye mojawapo wa mirija inayopitisha mayai ya uzazi (ectopic pregnancy). Hii ni dharura. Muone daktari au mfanyakazi wa afya mara moja.
Unaweza kusikia uchovu kidogo na kupata maumivu tumboni au maumivu ya siku moja baada ya utoaji mimba. Utakuwa unatokwa damu kiasi ukeni kwa muda hadi wiki 2. Lakini baada ya siku 1, itakuwa kama hedhi nyepesi ya kila mwezi. Hedhi yako ya mwezi inapaswa kurudia hali ya kawaida ndani ya wiki 4 hadi 6 baada ya utoaji mimba. Inaweza kuchukua muda zaidi kama ujauzito wako ulikuwa zaidi ya miezi 5 hadi 6.
Kama hukupata mtu wa kuongea naye baada ya kutoa mimba, inaweza kusaidia sasa kuongea na mtu unayemwamini juu ya mawazo yako. Maongezi haya yanaweza kukusaidia kujisikia vizuri.
Jinsi ya kujitunza baada ya kutoa mimba:
- Ili kuzuia maambukizi, tumia miligramu 100 za doxycycline mara 2 kwa siku, siku hiyo ya kutoa mimba. (Lakini kama unanyonyesha, ni bora kutumia miligramu 500 ya erythromycin mara 4 kila siku, kwa siku 7 badala ya doxycycline.)
Baada ya kutoa mimba, anza uzazi wa mpango mara moja. Usipofanya hivyo, unaweza kupata mimba tena kabla ya hedhi yako ya mwezi unaofuata. |
- Usifanye ngono au kuingiza kitu chochote kwenye uke wako angalau kwa siku 2 baada ya damu kusimama.
- Kama una mkakamao wa misuli tumboni au maumivu, pangusa au kanda polepole, au tumia chupa ya maji ya moto kukanda juu ya tumbo lako. Au tumia panado paracetamol au ibrofeni ibuprofen.
- Ili kupunguza maumivu na utokaji damu, pangusa au kanda sehemu ya chini ya tumbo lako mara kwa mara. Hii husaidia ukubwa wa tumbo kupungua kurudia hali ya kawaida na hivyo kupunguza uvujaji damu.
- Kunywa vinywaji kwa wingi husaidia kupona haraka.
- Unaweza kurudia shughuli zako za kawaida mara utakapojisikia vizuri, kawaida ndani ya siku 1.