Hesperian Health Guides

Kufanya uamuzi juu ya kutoa mimba

Katika sura hii:

WWHD10 Ch15 Page 243-1.png

Uamuzi wako wa kutoa mimba mara nyingi utategemea iwapo huduma salama inapatikana eneo unapoishi. Hutegemea pia jinsi gani tendo la kuitoa mimba hiyo au mtoto akiachwa litatakapoathiri maisha yako.

Kama huduma ya utoaji mimba salama haipatikani, unaweza kufikiria nani atakayekusaidia kumlea mtoto huyu: ndugu, mtu mwingine au kituo ambacho kiko tayari kumlea, kama jambo hili linakubalika kwako na jamii yako.

Inaweza kusaidia kuyafikiria maswali yafuatayo:

  • Je utaweza kumlea mtoto? Unao uwezo wa kiuchumi wa kutosha wa kumhudumia mtoto?
  • Je ujauzito huo ni hatari kwa afya yako?
  • Una mwenzi au mume, au ndugu ambaye atakusaidia kumhudumia mtoto? Unaweza kuongea naye juu ya uamuzi huu?
  • Je dini yako au familia yako inakataza utoaji mimba? Kama ndiyo, utajisikiaje kama utafanya tendo hilo?
  • Je utoaji mimba utafanyikaje?
  • Ujauzito una muda gani?
  • Je yawezekana una maambukizi ya ngono? Unaweza kuwa katika hatari kubwa ya maambukizi kupitia ngono kama wewe ni kijana, hujaoa au kuolewa, au una mwenzi mpya, au kama tayari una dalili za maambukizi kupitia ngono. Unaweza kwanza kutafuta matibabu kabla ya tendo hilo la kutoa mimba.
  • Je ni matatizo gani ya kiafya ambayo yanaweza kusababishwa na utoaji mimba hiyo? Kama una VVU au UKIMWI, hatari za utoaji mimba usiyo salama huongezeka.
  • Unaweza kwenda wapi kupata huduma ya dharura kama yatatokea matatizo makubwa ya kiafya? Utakwendaje?


Taarifa katika sehemu ya sura hii iliyobaki zinaweza kukusaidia kuamua iwapo huduma salama ya utoaji mimba zinapatikana katika eneo lako au la.


Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Mei 2017