Hesperian Health Guides

Matatizo ya kiafya yanayohusiana na utoaji mimba

Katika sura hii:

Mwanamke mwenye dalili za hatari baada ya utoaji mimba anahitaji msaada wa kitabibu haraka! Anapaswa kwenda haraka kwenye kituo cha afya au hospitali ili aweze kupata huduma stahili. Mara nyingi tumbo la uzazi lazima lisafishwe kabisa kwa kutumia vifaa vya unyonyaji au ufyonzaji (MVA). Wakati huo huo, taarifa kwenye kurasa 8 zifuatazo zinaweza kusaidia kama hakuna usafiri wa haraka au kama huduma ya matibabu ipo mbali sana.

Tiba ya haraka ya matatizo ya afya yanaohusiana na utoaji mimba huzuia magonjwa, ugumba, na kifo. Tafuta msaada haraka kama una matatizo baada ya utoaji mimba. USISUBIRI!

mwanamke amelala kwa kuegemea mito kadhaa kukiwa na dimbwi la damu katikati ya miguu yake

Damu nyingi kutoka ukeni

Kawaida tatizo kubwa baada ya utoaji mimba ni kutokwa na damu nyingi. Mara nyingi husababishwa na vipande vidogo vya ujauzito kubaki tumboni. Hii humaanisha kuwa utoaji mimba haukukamilika. Kama vipande hivyo vitatolewa, mara nyingi utokaji damu husimama. Wakati mwingine utokaji damu husababishwa na mchaniko kwenye mlango wa kizazi au seviksi ambao lazima ushonwe ili damu isimame.

Mwanamke anakuwa anatokwa na damu nyingi sana iwapo atakuwa analoanisha zaidi ya padi nzito au vitambaa 2 ndani ya saa moja kwa saa 2 mfululizo. Uvujaji polepole wa damu yenye rangi kali nyekundu pia ni hatari. Hili likitokea, mwanamke anaweza kupoteza kiasi kikubwa cha damu haraka na ni hatari. Kama haiwezekani kupata msaada wa kitabibu haraka, jaribu njia zifuatazo kusimamisha utokaji damu huo.

Kusimamisha utokaji damu

mwanamke ameegemea mito akipangusha au kukanda tumbo lake, damu ikiwa imetwama katikati ya miguu yake.

Mwanamke ambaye anatokwa damu sana anaweza kusaidia tumbo lake kubana na kufunga kwa kupangusha au kukanda tumbo hilo mara kadhaa. Aidha anaweza kufanya mwenyewe au kupata msaada wa mtu mwingine. Pangusa au singa, au kanda tumbo lako la chini kwa nguvu ukiwa umelala au umechutama.

Kama kuna vipande vya tishu ambavyo vimekwama tumboni au kwenye mlango wa kizazi, mwanamke anaweza kuvitoa nje kwa kuchutama na kusukuma kama vile anajisaidia haja kubwa.

Hata kama hatua hizi zitaonekana kusaidia, tafuta msaada wa kitabibu haraka. Mwanamke atahitaji dawa za antibiotiki na zaidi ya hapo anaweza kuhitaji kusafishwa tumbo kabisa.

Msaada wa dharura kwa tatizo la kutokwa na damu nyingi

Wafanyakazi wa afya na wengine ambao wamepitia mafunzo ya uchunguzi wa nyonga (pelvisi) za wanawake wanaweza kufuata hatua zifuatazo na kusimamisha damu kutoka hadi tumbo litakaposafishwa.

MUHIMU! Kwa sababu njia ya kuingia tumbo la mwanamke ni wazi, ni hatari sana kuingiza kitu chochote kwenye uke. Mwanamke anaweza kupata maambukizi makali kwa urahisi. Hili linaweza kufanyika tu pale anapokuwa anatokwa na damu nyingi sana na maisha yake kuwa katika hatari.


WWHD10 Ch15 Page 252-1.png
  1. Nawa mikono yako na pia safisha sehemu za uke wa mwanamke kwa maji safi na sabuni.

  2. WWHD10 Ch15 Page 252-2.png
  3. Vaa glovu safi au mfuko wa nailoni safi kwenye mkono mmoja. Mkono uliovalishwa glovu usiguse kitu chochote kabla ya kuingizwa kwenye uke.

  4. Mwelekeze mwanamke kulalia mgongo wakati miguu na magoti yake yakiwa yamepanuliwa. Msaidie ajisikie vizuri.
  5. WWHND12 Ch15 Page 252-3.png
    WWHD10 Ch15 Page 252-4.png
    Tumia fosepsi (kishikio) kilichotakaswa kuondoa vipande vyovyote vya tishu ambavyo utaona kwenye mlango wa tumbo la uzazi.
  6. Kama unacho kifaa cha spekilamu (kifaa maalum cha kupanua sehemu ya mwili ambayo haionekani vizuri ili iweze kuchunguzwa) ambacho kimetakaswa, jaribu kuingiza ukeni kuangalia mlango wa tumbo la kizazi. Kama utaona ndani vipande vya tishu au damu iliyoganda, jaribu kuvikamata kwa kutumia fosepsi na kuviondoa taratibu.

  7. mlango wa tumbo la uzazi la mwanamke (seviksi) ukionekana kupitia spekilamu kwenye uke wake
    WWHND10 Ch15 Page 252-5a.png
    seviksi-mlango wa tumbo la uzazi
  8. Kama huna spekilamu, ingiza ndani ya uke wa mwanamke mkono wako uliovalishwa glovu, ukianza na kidole kimoja, na baada ya hapo vidole 2.

  9. Gusa mlango wa kizazi. Utaonekana kuwa gumu na kuteleza kuliko ngozi inayozunguka. Utaonekana hivi:
  10. WWHD10 Ch15 Page 253-1.png


  11. Tembeza kidole chako kutoka upande mmoja wa mlango hadi mwingine na kujaribu kuhisi kama kuna vipande vya ujauzito vilivyobaki ndani. Vikiguswa vitakuwa kama nyama laini. Taratibu jaribu kuviondoa. Kama vipande hivyo vinateleza sana, toa nje mkono wako na kuviringisha juu ya vidole 2 kitambaa maalum chembamba kinachoona kilichotakaswa (stirile gauze), au kitambaa kisafi ambacho kimechemshwa kwenye maji na kukaushwa, na kujaribu tena kuviondoa.
  12. WWHD10 Ch15 Page 253-2.png


  13. Baada ya kuviondoa vipande hivyo vya tishu, ingiza mkono wako uliovalishwa glovu, vidole 2 vikiwa chini ya tumbo. Kwa kutumia mkono mwingine pangusa, kanda au singa tumbo lake kusaidia kusimamisha utokaji damu. Tumbo lake linapaswa kuwa kati ya mikono yako 2.

  14. Taarifa zaidi
    jinsi ya kuchoma sindano
  15. Mchome mwanamke sindano ya ergometrine (miligramu 0.2) kwenye msuli mkubwa, kama vile kwenye kalio au paja. Halafu mpatie kidonge 1 cha miligramu 0.2 au sindano ya ergometrine kila saa 6 kwa saa 24. Au unaweza kutumia misoprostol: mpatie 600 mcg kwa njia ya mdomo, au baada ya kuvaa glovu ingiza 600 mcg kwenye unyeo (njia ya haja kubwa).

  16. Mpe antibiotiki kuzuia maambukizi mara moja. Atakuwa katika hatari kubwa ya maambukizi kwa sababu tumbo liko wazi kuingiliwa na vijidudu.

  17. Kama atakuwa ameamuka, mpe vinywaji. Kama atakuwa bado hajapata fahamu, angalia ukurasa ufuatao.
  18. USAFIRI!


  19. Mpeleke hospitali mara moja, hata kama utakuwa unafikiri kuwa umetoa mabaki yote ya vipande vya tishu na damu imesimama. Bado atahitaji kusafishwa kizazi kabisa. Kama damu haitasimama, endelea kupangusa au kukanda tumbo la chini wakati unampeleka hospitali.

Mzunguko hafifu wa damu mwilini

Mzunguko hafifu wa damu mwilini ni hali inayotishia maisha ambayo inaweza kutokana na kutokwa na damu nyingi sana. Uvujaji damu ndani ya mwili pia unaweza kusababisha mzunguko hafifu wa damu.

HATARI! Kutokwa na damu nyingi sana kunaweza kusababisha MZUNGUKO HAFIFU WA DAMU, ambao unaweza kuua. Msafirishe haraka.

Dalili:
  • Mapigo ya moyo kwenda mbio sana, zaidi ya mapigo 100 kwa dakika kwa mtu mzima
  • Ngozi iliopauka, baridi, na yenye unyevu
  • Rangi ya kigubiko cha jicho cha ndani, mdomo na viganja kufifia/kupauka
  • Kupumua haraka haraka, zaidi ya pumzi 30 kwa dakika
  • Kuchanganyikiwa au kupoteza fahamu (kuzirai)
Matibabu kama atakuwa bado ana fahamu:
  • Mlaze mwanamke chini miguu yake ikiwa imeinuliwa juu kuliko kichwa.
  • Mfunike na blanketi au nguo.
  • Kama anaweza kunywa, mpe maji kidogo kidogo au kinywaji maalum cha kuongeza maji mwilini (rehydration drink).
  • Msaidie abaki mtulivu.
  • Kama unaweza, mwanzishie dripu ya haraka kwa njia ya sindano, au mwongezee maji kwa kutumia njia ya haja kubwa (rectal fluids).
Matibabu kama amepoteza fahamu:
  • Mlaze upande, kichwa nacho kilazwe upande na miguu yake ikiwa imeinuliwa kidogo.
mwanamke akiwa amelala kwenye kitanda cha kupumzikia kilichoinuliwa upande mmoja na matofali yaliyopangwa
Hakikisha miguu yake imeinuliwa juu kuliko kichwa chake.
  • Kama anaonekana kukabwa na kitu, vuta mbele ulimi wake kwa kutumia kidole chako.
  • Kama ametapika, safisha ndani ya mdomo wake haraka. Hakikisha kichwa chake kiko usawa wa chini, kimebinuliwa kwa kuangalia nyuma na kulalia upande mmoja ili asivute matapishi kwenye mapafu yake wakati akipumua.
  • Usimpe kitu chochote kwa njia ya mdomo hadi atakapokuwa amekaa angalau saa 1 baada ya kuamuka.

USAFIRI!

  • Kama unajua jinsi ya kutoa huduma ya dripu, mpatie dripu ya haraka kwa njia ya sindano. Kama huwezi, mpatie huduma hiyo kwa njia ya haja kubwa (rectal fluids).

Usimsubiri mfanyakazi wa afya. Mpeleke hospitali mara moja kupata msaada wa haraka. Anahitaji msaada wa kitabibu haraka!

Maambukizi

Kama kuna maambukizi, uwezekano mkubwa ni maambukizi kidogo kama utoaji mimba ulifanyika mapema kabla ya kufikisha miezi 3 (wiki 12).

Maambukizi makubwa ni maambukizi ambayo yameenea kwenye damu (sepsisi). Mwanamke ana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi makubwa kama utoaji mimba ulifanyika baada ya miezi 3 au 4 ya hedhi ya mwisho (mimba ya zaidi ya miezi 3), au kama kulitokea majeraha kwenye tumbo la uzazi wakati wa utoaji mimba. Sepsisi ni hali ya hatari sana na inaweza kusababisha mzunguko hafifu wa damu mwilini. Maambukizi yanaweza kutokea kwa sababu:

  • Mkono usiyo msafi au kifaa kiliingizwa ndani ya tumbo la uzazi.
  • Vipande vya ujauzito vilibaki ndani na huenda vimepata maambukizi.
  • Mwanamke tayari alikuwa na maambukizi alipotoa mimba hiyo.
  • Shimo au jeraha kutokana na ukuta wa ndani ya tumbo la uzazi kutobolewa.
mwanamke ameshika kichwa chake, akitokwa na jasho na kutetemeka
Dalili za maambukizi madogo:
  • Homa kidogo
  • Maumivu kidogo tumboni
Matibabu kwa ajili ya maambukizi madogo:

Katika kudhibiti maambukizi madogo yasiongezeke na kuwa makubwa zaidi, yatibu haraka na dawa zilizoorodheshwa hapo chini. Mwanamke anahitaji zaidi ya dawa moja kwa sababu maambukizi baada ya utoaji mimba husababishwa na aina tofauti za vijidudu.

Kama dawa zilizoorodheshwa chini hazipatikani, angalia “Kurasa za kijani” kwa dawa zingine ambazo zinaweza kufanya kazi. Mwanamke ambaye ananyonyesha anapaswa kupatiwa matibabu ya maambukizi tumboni baada ya kujifungua.

Dalili za maambukizi makubwa au makali:
  • baridi kali na homa kali
  • maumivu ya misuli, udhaifu, na uchovu
  • tumbo kuvimba, gumu, na linauma
  • majimaji yenye harufu mbaya kutoka ukeni
mwanamke amelala chini, akitokwa jasho na anaonekana mgonjwa

USAFIRI!

Matibabu ya maambukizi makubwa:
  • Mpeleke mwanamke kwenye kituo cha afya au hospitali haraka.
  • Mwanzishie dawa zifuatazo mara moja, hata kama tayari mtakua njiani kuelekea hospitalini.


Dawa kwa ajili ya maambukizi baada ya utoaji mimba

Matibabu:
Mpe kundi mojawapo la dawa (mpe dawa zote 3 katika kundi husika):
Mpe dawa zote 3
ceftriaxone Miligramu 250 kwa njia ya sindano kwenye misuli Mara 1 tu
na
doxycycline Miligramu 100 kwa njia ya mdomo Mara 2 tu
(epuka doxycycline kama unanyonyesha)
na
metronidazole Miligramu 500 kwa njia ya mdomo au kwa njia ya dripu Mara 3 tu
AU
ampicillin Gramu 2 (miligramu 2000) kwa njia ya dripu au sindano kwenye misuli mara ya kwanza tu, baada ya hapo gramu 1 (miligramu 1000) kwa njia ya dripu au sindano kwenye misuli kila unapotoa Mara 4 tu
na
gentamicin Miligramu 80 dripu au sindano kwenye misuli Mara 3 tu
na
metronidazole 5 Miligramu 500 kwa njia ya mdomo au dripu Mara 3 tu
AU
Mpe dawa 2
clindamycin miligramu 900 kwa njia ya dripu Mara 3 tu
na
gentamicin Miligramu 80 kwa njia ya dripu au sindano kwenye misuli Mara 3 tu
MUHIMU! Kama mwanamke hapati nafuu ndani ya saa 24 tangu aanze dawa ya kwanza, atahitaji kwenda hospitali mara moja.
Simamisha utoaji dawa kwa njia ya sindano au dripu pale dalili za maambukizi zitakapokuwa zimetoweka angalau kwa saa 48. Baada ya hapo anza kumpa dawa kwa njia ya mdomo na maji mengi.
Baada ya dalili kutoweka kwa saa 48
Mpe dawa 2:
doxycycline Miligramu 100 kwa njia ya mdomo Mara 2 kila siku kwa siku 10
(epuka kutumia doxycycline kama unanyonyesha)
na
metronidazole Miligramu 500 kwa njia ya mdomo Mara 3 kila siku kwa siku 10

Jeraha ndani ya mwili

Jeraha ndani ya mwili kutokana na utoaji mimba mara nyingi husababishwa na kifaa kikali ambacho kinaweza kuacha shimo tumboni. Kifaa kinaweza kusababisha madhara kwa viungo vya ndani, kama vile mirija ya mayai, ovari (mifuko ya mayai), utumbo, na kibofu.

Mwanamke anapokuwa na majeraha ya ndani anaweza kutokwa na damu nyingi sana.

Dalili (atakuwa na baadhi au dalili zote zifuatazo):
mwanamke akiinamisha kichwa na kuweka sikio juu ya tumbo la mwanamke kusikilizia
Sikiliza kwa dakika 2 kama kuna mgugumo.
  • Tumbo lake ukiligusa linaonekana kukakamaa na ni gumu na halitoi sauti au mgugumo ndani
  • Maumivu makali au mkakamao wa misuli tumboni wenye maumivu
  • Homa
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Maumivu kwenye bega moja au yote mawili
Matibabu:

USAFIRI!

  • Haraka sana mpeleke hospitali au kwenye kliniki ili aweze kufanyiwa upasuaji. Jeraha ndani ya mwili lazima litibiwe mara moja au linaweza kusababisha maambukizi, mzungunguko hafifu wa damu, na kifo.
  • Usimpe kitu chochote kwa njia ya mdomo — siyo chakula, siyo kinywaji, siyo hata maji — isipokuwa tu kama itachukua zaidi ya saa 12 kufika kwenye kituo cha afya. Halafu mpe maji katika kiasi kidogo kidogo. Au wezesha afyonze kutoka kwenye kitambaa ambacho kimelowekwa kwenye maji.
  • Kama atakuwa na dalili za shambulio kali la mshituko, mtibu kwa ajili mshituko. Hakikisha kuwa hakuna kinachomziba na anaweza kupumua.
  • Mpe dawa kwa ajili ya maambukizi. Kama inawezekana, mpe chanjo ya tetanasi.

Huduma ya faraja baada ya mimba kutolewa

WWHND10 Ch15 Page 258-2.png

Mwanamke anaweza kukumbwa na hisia kali baada ya kutolewa mimba, hata kama anajua alifanya uamuzi sahihi kwa ajili yake na familia yake. Baadhi ya wanawake hukumbwa na mchanganyiko wa hisia: hisia ya kujitua mzigo, uchungu, huzuni, hatia, aibu, hasira, na hata upendo. Ni kawaida wanawake kusikia uchungu na kuhuzunika pale ujauzito unapositishwa. Hisia hizi ni za kawaida lakini kuzificha na kujifanya kwamba hakuna kilichotokea kunaweza kuifanya hali kuwa mbaya zaidi. Wanawake wengi watanufaika na kuongea na wanawake wengine ambao wamepitia hali hiyo.

Kawaida, mwanamke ambaye ana matatizo makubwa ya kiafya kutokana na utoaji mimba huenda hakupata huduma bora. Mtoaji huduma ambaye hakutoa huduma hiyo vizuri anaweza kuwa alishindwa kumheshimu au alikuwa mkatili. Huenda utoaji mimba uliambatana na maumivu makali sana au ulikuwa wa kutisha kwa mwanamke. Vilevile, mahali utoaji mimba hauruhusiwi kisheria, mwanamke anaweza kuogopa kuadhibiwa.

Kutengeneza mwiko juu ya kile kilichotokea kunaweza pia kuwasaidia wanawake kuweka nyuma tukio hilo na kuendelea na maisha. Kwa mfano, kuzika au kuchoma kifaa ambacho kinahusiana na utoaji mimba kunaweza kuashiria mwisho wa tukio hilo la utoaji mimba. Katika baadhi ya jamii, mwanamke anaweza kupanda mti au kwenda sehemu takatifu na kutoa sadaka.



Ukurasa huu ulihuishwa: 12 Juni 2017