Hesperian Health Guides

Kupata msaada kutoka kwa wazazi

Kuongea na mama au baba yako wakati mwingine ni jambo gumu. Wazazi wako wanaweza kutaka uishi kwa kuzingatia mila na tamaduni, lakini wakati unabadilika. Unaweza kuhisi kuwa wazazi wako hawakusikilizi au kujitahidi kukuelewa. Au unaweza kuogopa kuwa watakasirika.

Familia yako inaweza kuendelea kukupenda bila kukubaliana na wewe juu ya kila kitu unachosema. Wanaweza kukasirika kwa sababu wanajali — siyo kwamba hawakupendi. Jaribu kuongea nao kwa heshima na kuwasaidia kukuelewa vizuri zaidi.

Jinsi mama wazazi wanaweza kuwasaidia binti zao

Unaweza kuwa ulikulia katika kipindi ambacho wasichana walikuwa hawaruhusiwi kupata elimu, kupanga familia zao, au kufanya maamuzi juu ya maisha yao. Maisha ya binti yako yanaweza kuwa tofauti. Kama utamsikiliza, mweleze uzoefu wako na kumpa taarifa muhimu, unaweza kumsaidia kufanya maamuzi mazuri yeye mwenyewe. Unaweza kumsaidia kuona mambo mengi mazuri ya kuwa msichana na mwanamke.Ukurasa huu ulihuishwa: 05 Feb 2018