Hesperian Health Guides

Sura ya 5: Masuala ya afya yahusuyo wasichana

HealthWiki > Pale ambapo Wanawake hawana Daktari > Sura ya 5: Masuala ya afya yahusuyo wasichana

wanawake wenye umri mdogo 2 wakimsikiliza mama mwenye umri mkubwa

Kati ya umri wa miaka 10 na 15, mwili wa msichana huanza kukua na kubadilika kuwa mwili wa mtu mzima. Miaka hii inaweza kuwa kipindi cha kusisimua sana lakini pia kipindi kigumu. Mwanamke kijana anaweza kutojisikia kuwa msichana halisi au mwanamke kamili kwani mwili wake bado upo katikati na anafanya mambo mapya ambayo alikuwa hafanyi zamani. Kitakachofanya mambo yawe magumu zaidi ni pale ambapo hakuna mtu anayeyazungumzia mabadiliko hayo na hivyo msichana hajui ni kitu gani atarajie. Sura hii inazungumzia mabadiliko haya, na kuelezea jinsi msichana anaweza kuendelea vizuri kiafya kadri anavyokua, na kutoa elimu ya kumsaidia kuweza kufanya maamuzi sahihi juu ya maisha yenye afya.


Ukurasa huu ulihuishwa: 05 Feb 2018