Hesperian Health Guides

Kuimarisha usafi katika jamii na kutumia vizuri taka ngumu

Katika sura hii:

Kulinda jamii zetu kutokana na taka zenye madhara na kubadilisha taka kuwa rasilimali huboresha afya ya jamii, afya ya mazingira na huokoa fedha. Kwa mfano, kundi la wakusanyaji taka nchini Ajentina waligundua kuwa iwapo taka zote za asili ya karatasi katika jiji la Buenos Aires zingekusanywa na kurejeshewa thamani, hatua hiyo ingeokoa dola za Kimarekani milioni 10 kila mwaka. Iwapo fedha hii ingetumika kuwalipa wakusanyaji taka wote katika jiji hilo, kila mtu angepata zaidi ya dola 150 kwa mwezi.

Kila mtu na kila jamii inaweza kuchukua jukumu la kupunguza uzalishaji taka na uondoaji taka hizo kwa usalama. Lakini japokuwa jamii zinaweza kufanya mengi zenyewe, taka ni suala la kisiasa ambalo linaweza kutatuliwa tu pale serikali, wenye viwanda na jamii watakapofanya kazi pamoja, wakiwa na lengo la kuboresha afya za watu. Serikali haina budi kuchukuwa hatua ili kupunguza mzigo wa taka kwa watu na mazingira, kwa kuvitaka viwanda kutengeneza bidhaa zinazozalisha taka kidogo tu kadri inavyowezekana. Juhudi za Serikali kusaidia mipango au miradi inayowezesha watu kutumia taka tena, kuzirejeshea thamani, na kuziondoa kwa usalama zinaweza kuokoa fedha, kuzalisha ajira, na kusaidia kutatua matatizo ya kijamii. (Soma “Jamii yajipatia riziki kutokana na biashara ya taka,” “Jinsi ya kutengeneza mboji kwa kutumia minyoo ya ardhini,” “Vituo vya jamii vya usimamizi wa rasilimali taka,” na “Jinsi mji ulivyopambana na taka ngumu na kufanikiwa”).




Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Juni 2022