Hesperian Health Guides
Jinsi ya kuangamiza kwa usalama taka zisizohitajika
HealthWiki > Mwongozo wa jamii juu ya afya ya mazingira > Sehemu ya kwanza: Kubadili hatari ya kiafya kuwa fursa > Jinsi ya kuangamiza kwa usalama taka zisizohitajika
Mahali ambapo karatasi nyepesi na karatasi ngumu haziwezi kutumika tena, kurejeshewa thamani au kutengeneza mboji, zinaweza kukatwakatwa vipande na kutumika kuwashia jiko, au kuchomwa wakati wa kupika kama chanzo cha nishati. Lakini uchomaji, hata kiasi kidogo, wa plastiki au mpira huachia kemikali zenye sumu ikiwemo dioksini, furans na PCB ambazo husababisha matatizo mengi ya kiafya.
Taka ambazo haziwezi kushughulikiwa kwa njia yoyote ile zinaweza kufukiwa katika mashimo madogo au kupelekwa kwenye shimo maalum la kuhifadhi taka kwa usalama (sanitary landfill). Kama ni kuzifukia kwenye mashimo madogo ya kawaida, cha kufanya ni:
- chimba shimo mbali na vyanzo vya maji,
- weka taka kwenye shimo hilo, na
- fukia na udongo.
Pale taka zenye kemikali ya sumu zinapofukiwa aridhini, kemikali hizi zinaweza kuvuja ardhini na kuchafua maji ya kunywa. Kama hakuna njia salama ya kuondoa taka zenye kemikali ya sumu (kwa mfano kuzirudisha kwa mtengenezaji au kuzitibu hadi zitakapokuwa salama), angalau zipelekwe kwenye shimo maalum la kuhifadhi taka kwa usalama lenye tabaka la kinga sakafuni na kutani kwa ajili ya kuzuia mvujo wa sumu kuingia kwenye vyanzo vya maji.