Hesperian Health Guides
Wafanyakazi wa afya wanaweza kutoa msaada zaidi kwa watu wenye saratani
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Wafanyakazi wa afya wanaweza kutoa msaada zaidi kwa watu wenye saratani
Msaidie mtu mwenye saratani na familia:
- Kutojisikia wapweke.
- Watambulishe kwa watu wengine ambao nao wamepitia uzoefu unaofanana.
- Wasaidie katika kutafuta vyakula vyenye afya, usafiri, na hata usimamizi wa nyumba na watoto wao, ikiwezekana kwa kushirikisha wanandugu, vikundi vya kijamii, makanisa au misikiti, na huduma za serikali.
- Tunza orodha ya kliniki, madaktari, na taasisi ambazo husaidia watu wenye saratani katika eneo, wilaya, mkoa au nchi yako.
- Msaidie mtu mwenye saratani kudhibiti maumivu, kero au kutojisikia vizuri, na wasiwasi au uoga.
- Wasaidie watu wenye saratani na familia zao kuepuka watu wadanganyifu ambao watachukua fedha zao na kuahidi uponyaji wa kimiujiza ambao haupo au utafanya hali zao kuwa mbaya zaidi.
![mfanyakazi wa afya akiongea na mwanamke.n.](https://pool.hesperian.org/w/images/thumb/f/fd/NWTND_Can_Page_21-1.png/370px-NWTND_Can_Page_21-1.png)
Changia juhudi za kuongeza uelewa na uzuiaji wa saratani:
- Himiza watu kujifunza dalili za mwanzo za saratani na kutoogopa kwenda kupimwa kwa sababu kupima mapema ni muhimu sana.
- Saidia kufundisha makundi kuacha uvutaji wa tumbaku na madawa ya kulevya.
- Elimisha jamii juu ya umuhimu wa chanjo dhidi ya homa ya manjano (hepatitis B) na kirusi cha HPV.
- Himiza wanawake kuchuguzwa saratani ya shingo ya kizazi na saratani zingine kama huduma ya uchunguzi wa saratani inatolewa katika eneo lako.
- Tafuta fursa za mafunzo kwa ajili yako na wafanyakazi wengine kuweza kutibu baadhi ya saratani. Wakunga wanaweza kujifunza kuchunguza na kuzuia baadhi ya saratani.
- Wasaidie watu kujipanga kuzuia kemikali zenye sumu na vichafuzi vingine kuingia kwenye vyanzo vya maji ya jamii, ardhi na hewa.
- Himiza jamii kuwasaidia na kuwatendea watu wenye saratani kwa huruma, na siyo kuwalaumu kwa ajili ya magonjwa yao.