Hesperian Health Guides

Njia ambazo hazisaidii

Njia zifuatazo hazisaidii au zina madhara:

  • Kukojoa mkojo baada ya tendo la ngono siyo hatari, lakini hakusaidii kuzuia mimba. Mkojo hutokea kupitia tobo tofauti na siyo uke.
  • Kuweka madawa ya mitishamba, mimea, kemikali, au kitu chochote ambacho hukausha uke haviwezi kuzuia mimba. Lakini vinaweza kuathiri uke, na kurahihisha mwanamke kupata maambukizi.
  • Kusafisha uke na maji kwa kupiga bomba baada ya kufanya tendo la ngono hakuwezi kuzuia mimba. Kitendo cha kupiga bomba ya maji kusafisha uke kinaweza kusukumzia shahawa ndani zaidi kwenye kizazi.
  • Kuva bangili au kufanya sala hakuwezi kuzuia mimba. Wanawake ambao hutegemea njia hizi hupata mimba kwa urahisi.