Hesperian Health Guides
Jinsi mwanamke anavyopata mimba
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Uzazi wa mpango > Jinsi mwanamke anavyopata mimba
Mifuko ya mayai ya kike (Ovari): baada ya wastani wa mwezi mmoja, mojawapo ya mifuko ya mwanamke ya mayai huachia yai la kike la uzazi lililopevuka kwenye njia au mirija ya kusafirisha mayai. |
Mrija wa kusafirisha mayai : yai la uzazi lilopevuka husafiri kwenye mrija huo na kuelekea kwenye mji wa mimba au tumbo la uzazi.
Mji wa mimba (tumbo la uzazi): mahali ambapo mtoto hukulia baada ya mwanamke kupata mimba.
Mlango wa mji wa mimba
Uke |
Mwanaume anapofikia kilele na kuachia shahawa ndani au karibu na uke, shahawa kutoka kwenye ume huingia kwenye mji wa mimba au kizazi cha mwanamke na kwenye njia za kusafirisha mayai ya kike ya uzazi. Kama ni wakati wa kipindi cha rutuba(kipindi cha mwanamke kushika mimba), mbegu ya kiume inaweza kuungana na yai la kike lililopevuka. Kama mbegu ya kiume itarutubisha yai hilo, basi hujibanza kwenye ukuta wa mji wa mimba(kizazi). Hapo mimba itakuwa imetunga. Njia za uzazi wa mpango huzuia mimba kwa kuzuia mbegu za kiume kuingia kwenye uke, au kusimamisha mwili wa mwanamke usiachie mayai ya uzazi, au kuzuia mbegu za kiume kukutana na yai.