Hesperian Health Guides
Dawa za kudhibiti mzio (antihistamines)
Muwasho,chafya, na upele kutokana na mzio kawaida hutibika kwa kutumia dawa za mzio (antihistamines). Dawa ya mzio yoyote hufanya kazi vizuri kama dawa ya aina hiyo nyingine. Hivyo, kama huna krolofeniramini (chlorpheniramine) ambayo imeelezewa chini, tumia difenihidramini (diphenhydramine) au dawa nyingine ya mzio katika dozi sahihi (dozi itatofautiana kutegemea dawa na dawa). Dawa zote za mzio hulevya lakini huzidiana.
Dawa hizi hazisaidii kwa ajili ya homa ya mafua ya kawaida.
Kwa madhara makali ya mzio ambapo upumuaji ni wa shida, epinefrini (epinephrine)inahitajika sambamba na dawa za kudhibiti mzio. Angalia Huduma ya kwanza: Madawa.
Klorofeniramini (Chlorpheniramine, chlorphenamine)
Klorofeniramini ni dawa ya kupambana na mzio ambayo hupunguza muwasho, chafya, upele, na matatizo mengine yanayotokana na mzio. Inaweza kutumika baada ya kuumwa na mdudu, mzio wa kawaida au kutokana na chakula, au homa ya mzio - chafya ambazo zinambatana na kutokwa na machozi na kamasi kutokana na kuwepo chavua kwenye hewa (hay fever).
Kusinziasinzia (lakini tatizo hili halijitokezi sana kama ilivyo kwa dawa zingine za kupambana na mzio).
Miaka 3 hadi 5: toa miligramu 1, kila saa 4 hadi 6 hadi mgonjwa atakapopata nafuu.
Miaka 6 hadi 12: toa miligramu 2, kila saa 4 hadi 6 hadi mgonjwa atakapopata nafuu.
Zaidi ya miaka 12: toa miligramu 4, kila saa 4 hadi 6 hadi mgonjwa atakapopata nafuu.
Miaka 6 hadi 12: choma miligramu 5 hadi 10, kila saa 4 hadi 6, hadi dalili za madhara ya mzio zitoweke.
Zaidi ya miaka 12: choma miligramu 10 hadi 20 (isizidi miligramu 40 ndani ya saa 24), kila saa 4 hadi 6 hadi dalili zote za madhara ya mzio zitoweke.