Hesperian Health Guides
Dawa za kupambana na mashambulio (seizures)
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Kuwatunza watoto > Dawa za kupambana na mashambulio
Diazipamu
Diazipamu inaweza kutumika kulegeza misuli na kupunguza maumivu. Inaweza pia kutumika kuzuia shambulio moja. Kwa watu wanaopata mashambulio endelevu (kifafa) tumia dawa tofauti, dawa ambayo inaweza kutumika kila siku.
Kusinziasinzia.
- Diazipamu ikizidi hupunguza kasi ya kupumua au husimamisha kabisa kupumua. Usitoe zaidi ya dozi iliyopendekezwa na usitoe zaidi ya dozi 2.
- Diazipamu ni dawa yenye tabia ya kumkolea mtumiaji ambaye hujikuta na kiu ya kutaka kuitumia tena na tena. Epuka matumizi ya muda mrefu au matumizi ya mara kwa mara.
- Usitoe dawa hii kwa mjamzito au mama ambaye ananyonyesha ispokuwa kama mwanamke amepata shambulio (kwa mfano kuhusiana na kifafa cha mimba)
- Usichome sindano ya diazipamu isipokuwa tu kama una uzoefu au umepitia mafunzo ya kukuwezesha kufanya hivyo. Ni vigumu sana kutoa dawa hii kwa njia ya sindano. Badala yake, wakati wa shambulio, unaweza kuiweka dawa hii ndani ya njia ya haja kubwa.
Kulegeza misuli iliokakamaa na kupunguza maumivu
Toa vidonge vya diazipamu kwa njia ya mdomo dakika 45 kabla ya kufanya zoezi lenye maumivu makali kama vile kurudisha ndani henia au kunyosha mfupa. Toa miligramu 0.2 hadi 0.3 kwa kilo. Kama huwezi kumpima uzito mtoto, toa dozi kuzingatia umri:
Zaidi ya miaka 5: toa miligramu 2.
Tumia dawa ya diazipamu ya maji kwa ajili ya sindano, au saga kidonge 1 na kuchanganya na maji. Tumia bomba la sindano (bila sindano) kunyonya dawa na kuingiza kwenye njia ya haja kubwa. Au tumia mafuta ya daizipamu ambayo yametengenezwa maalum kwa ajili ya matumizi kwenye njia ya haja kubwa. Mlaze mgonjwa upande na tumia bomba la sindano (bila sindano) kuingiza dawa ndani kabisa ya njia yake ya haja kubwa. Halafu shikilia makalio yake pamoja kwa dakika 10 ili dawa ibaki ndani.
Miaka 7 hadi 12: toa miligramu 3 hadi 5, mara moja.
Zaidi ya miaka 12: toa miligramu 5 hadi 10, mara moja.
Kama shambulio halitadhibitiwa dakika 15 baada ya dawa kutolewa, rudia dozi. Usirudie dozi zaidi ya mara moja.