Hesperian Health Guides

Kutibu kidole tumbo na maambukizi ya ngozi ya fumbatio (Peritonitisi)

Maumivu tumboni, kuhara, na minyoo: Madawa

Idadi kadha ya antibiotiki zinaweza kutumika kutibu peritonitisi, lakini tumia kila mara angalau antibiotiki 2 kuua aina nyingi zaidi za bakteria. Kutibu peritonitisi, ni bora zaidi kuchoma sindano ya antibiotiki kwa sababu mfumo wa chakula hautaichakata vizuri dawa ambayo inatumiwa kwa njia ya mdomo. Kama njia ya mdomo itatumika, tumia kiasi cha maji ya kutosha tu kumezea vidonge hivyo. Mgonjwa hapaswi kula au kutumia vinywaji zaidi.

Toa dawa hizi hadi mgonjwa atakapofikishwa hospitali:
METRONIDAZO miligramu 500, mara 4 kila siku
     NA
SIPRO miligramu 500, mara 2 kila siku AU
SEFTRIAKSONI gramu 2, mara moja kwa siku AU
AMPISILINI gramu 2, mara 4 kila siku NA JENTAMAISINI miligramu 1.5 kwa kila kilo moja ya uzito, mara 3 kila siku.