Hesperian Health Guides

Dawa zingine za kutibu kuhara

Maumivu tumboni, kuhara, na minyoo: Madawa

Furoti Diloksanaidi (Diloxanide furoate)


Diloksanaidi (Diloxanide) hutumika pamoja na antibiotiki kutibu ameba. Kama huwezi kupata dawa hii, jaribu paromomaisini (paromomycin) au iodokino (iodoquinol) badala yake.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Kwa nadra dawa hii husababisha gesi tumboni, maumivu tumboni, au kichefuchefu. Tumia na chakula.

MuhimuNBgrnimportant.png

Usitumie diloksanaidi (diloxanide) ndani ya miezi 3 ya kwanza ya ujauzito. Epuka dawa hii wakati unapokuwa unanyonyesha.

Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png

Baada ya kumaliza dozi ya metronidazo au tiba nyingine ya ameba, anza kutumia diklosanaidi (diloxanide).

Tumia miligramu 20 kwa kila kilo ya uzito, ikigawanywa katika dozi 3 kila siku kwa siku 10. Kama huwezi kumpima mgonjwa, toa dozi kulingana na umri.
Chini ya miaka 3: toa miligramu 62 (⅛ ya kidonge cha miligramu 500), mara 3 kila siku kwa siku 10.
Miaka 3 hadi 7: toa miligramu 125, mara 3 kila siku kwa siku 10.
Miaka 8 hadi 12: toa miligramu 250, mara 3 kila siku kwa siku 10.
Zaidi ya miaka 12: toa miligramu 500, mara 3 kila siku kwa siku 10.

Kwinakrini (Quinacrine)


Dawa ya Kwinakrini (Quinacrine) hufanya kazi vizuri katika kutibu giardia, lakini huwafanya watu kujisikia vibaya zaidi. Hutumika kwa sababu siyo ghali sana.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Maumivu ya kichwa, kizunguzungu, na kutapika ni madhara ya kawaida.

Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png
Kwa matibabu ya giardia
Chini ya miaka 10: toa miligramu 50, mara 3 kila siku kwa wiki 1.
Zaidi ya miaka 10: toa miligramu 100, mara 3 kila siku kwa wiki 1.

Zinki


Zinki husaidia watu wanaoharisha kupata nafuu haraka. Inapaswa kutolewa pamoja na kinywaji cha kuuongezea mwili maji.

Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png

Kwa watoto wachanga, vidonge vinaweza kusagwa na kuchanganywa na maziwa ya mama au maji kidogo. Unaweza kupata kidonge ambacho huyeyuka haraka kwenye maji au kimiminika kingine.

Watoto wanaotoka kuzaliwa hadi miezi 6: toa miligramu 10, mara moja kwa siku 10 hadi 14.
Zaidi ya miezi 6: toa miligramu 20, mara moja kila siku kwa siku 10 hadi 14.