Hesperian Health Guides

Visababishi vya matatizo ya afya ya mazingira

A starving child begs. Njia moja ya kutafakari visababishi vya matatizo ya afya ya mazingira ni kuangalia:

  • Uhaba wa vitu muhimu ambavyo tunahitaji kwa ajili ya maisha bora kiafya kama vile hewa na maji safi, ardhi yenye rutuba na misitu, nyumba bora na salama, na mazingira salama ya kuishi na kufanyia kazi.
  • Kukithiri kwa vitu hatari katika mazingira yetu ambavyo hatuvihitaji, kama vile masalia ya vitu vilivyokwisha kutumika, kemikali za sumu, uchafuzi wa aina mbalimbali na vyakula visivyofaa.


Katika baadhi ya jamii, matatizo ya kiafya husababishwa na uhaba wa mahitaji ya msingi kama vile maji safi na salama, vyoo, na hata miti. Nchini India, Bhopal, matatizo makubwa ya kiafya yalisababishwa na mlipuko katika kiwanda cha kutengeneza kemikali ambao uliachia hewa ya sumu. Katika hali kama hiyo, uboreshaji wa afya ya mazingira ulitegemea uwezo wa watu kudhibiti mambo ambayo yalisababisha uhaba wa huduma za msingi, na uchafuzi uliokithiri. Kwa kulinda jamii zetu na mali asili zetu, tunalinda maisha ya baadae ya watoto wetu na vizazi vijavyo.

Townspeople clean up trash from a waterway.

Je watu ndiyo wengi lakini maliasili ni chache?

Kiasi cha maji, miti, madini na maliasili nyingine duniani ni kidogo wakati idadi ya watu wanaozitumia inaendelea kuongezeka haraka. Lakini tatizo hasa siyo idadi ya watu. Tatizo la msingi ni jinsi gani maliasili hizi zinavyogawanywa na kikundi kinapotumia yake ya maliasili, au kusababisha uchafuzi zaidi wa mazingira, mvurugiko huu wa urari huchangia matatizo ya afya ya mazingira kwa watu wengine.

Usemi wa matajiri kuhusu umaskini na uharibifu wa mazingira:
A fat man with a money sign on his tie points his finger.
Watu ni wengi, lakini ardhi na maliasili ni kidogo.
Crowded stick figures covering a cartoon earth begin to fall off the edges.
A man in a suit smoking a cigar rips a giant cartoon banknote away from a starving family.
Hakuna haki katika mgawanyo wa ardhi na maliasili, maliasili nyingi zipo mikononi mwa wachache.
Usemi wa watu masikini kuhusu uharibifu wa mazingira:


Baadhi ya watu huamini kwamba njia bora ya kuzuia uharibifu wa mazingira ni kupunguza idadi ya watu. Fikra kama hizo ndiyo msingi wa programu za kudhibiti ongezeko la idadi ya watu.

Programu hizi hata hivyo zimeshindwa kuboresha maisha ya watu mahali popote pale kwa sababu hazilengi kutafuta chimbuko la sababu za uharibifu wa mazingira, umasikini na afya duni. Familia zinapokuwa na rasilimali za kutosha, hujitahidi zaidi kutunza afya zao, heshima na nyingi huchagua kuzaa watoto wachache. Hivyo, ni pale ambapo jamii, serikali na mipango ya maendeleo itakapotoa kipaumbele kuboresha uhai wa watoto, na hali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ya wanawake ndipo tatizo la ongezeko la watu litakapodhibitiwa.

Hata hivyo, kupunguza idadi ya watu duniani hakutaondoa tatizo la ukosefu wa usawa katika matumizi ya maliasili na athari za wanadamu kwa mazingira. Njia bora ni kwa matajiri kutumia rasilimali chache na kwa uendelevu, na kutosababisha uchafuzi uliokithiri. Kwa kubadili tabia za hao wanaotumia maliasili nyingi sana kwanza, tunaweza taratibu kuhakikisha kuwepo kwa rasilimali za kutosha kwa afya bora ya kila mtu.

Udhibiti wa maliasili na mashirika au makampuni makubwa haufai kwa afya ya jamii

Baadhi ya matatizo ya kijamii katika nchi mbalimbali huchangiwa na mashirika au makampuni makubwa ya kibiashara. Kwa mfano kampuni kubwa inaweza kulipa watu kufyeka msitu. Siyo tu kwamba jamii inayouzunguka msitu huo itapoteza miti ambayo hutunza ardhi yao na kuilinda dhidi ya mmomonyoko, lakini itapoteza chanzo muhimu cha mahitaji kwa ajili ya uhai wao wa kila siku kama vile chakula, kuni, dawa, kamba na mahitaji mengine. Kwa maliasili muhimu kama vile msitu mkubwa kutoweka, ni sawa na uporaji wa mali hiyo kutoka kwa Muumbaji, jamii zinazoitegemea na hata kwa vizazi vijavyo.

Makampuni makubwa yanapodhibiti maliasili iwe ni mbao, mafuta, maji, mbegu au hata watu wenyewe, wao hupata faida na huwa hawaoni sababu kubwa ya kulinda au kuboresha maisha ya watu wa kawaida wanaoitegemea maliasili hiyo kwa uhai wao. Makampuni yanaweza kutoa ajira au pato la muda mfupi, lakini kama lengo lao ni kusafirisha bidhaa za maliasili hiyo kwenda nchi za nje, maliasili itakapokwisha na wao wataondoka. Jamii itabaki maskini zaidi hata kuliko mwanzo.
Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Juni 2022