Hesperian Health Guides

Sehemu ya kwanza: Tuhifadhi maliasili kwa manufaa ya wote

HealthWiki > Mwongozo wa jamii juu ya afya ya mazingira > Sehemu ya kwanza: Tuhifadhi maliasili kwa manufaa ya wote

Katika sura hii:

Women balancing water containers on their heads walk in a line.


Baada ya kusoma sehemu ya kwanza, utakuwa umejifunza:
  1. Jinsi mgawanyo mbaya wa maliasili za dunia unavyoathiri afya ya mazingira.
  2. Namna matumizi ya maliasili yasiyo endelevu yanavyoathiri afya ya mazingira.


Matumizi mabaya ya maliasili yanaweza kuathiri afya zetu na afya ya jamii nzima. Kwa sababu kila mtu anahitaji kutumia maliasili hizo, ni wajibu wa jamii kulinda, kuhifadhi na kuweka mgao mzuri wa maliasili hizo.

Kwa bahati mbaya maliasili zenyewe hazigawanywi kwa usawa kwa kila mtu: watu maskini hunufaika kidogo wakati matajiri hunufaika sana. Makampuni makubwa yenye nguvu, serikali na vyombo vyake mara nyingi huchukua sehemu kubwa ya maliasili hizi. Hata katika jamii moja, matajiri hutumia maliasili zaidi kuliko watu wa kawaida. Mara nyingi maskini hulazimika kupigana wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya masalia. Mgawanyo huu wa maliasili usio na usawa huwaathiri sana watu wenye uwezo mdogo.

Bila kuhifadhi maliasili na kuweka mgawanyo unaofaa, ni wachache tu wenye uwezo mkubwa wa kiuchumi na kiserikali ambao watafaidi haki ya afya ya mazingira, na wala siyo wenye uwezo mdogo walio wengi ambao wanahitaji kutumia maliasili hizi kwa uhai wao wa kila siku. Kama alivyosema hayati Mahatma Ghandi, zipo rasilimali za kutosha kukidhi mahitaji ya msingi ya binadamu wote, lakini haziwezi kukidhi tamaa ya kila mtu.


Ukurasa huu ulihuishwa: 05 Jan 2024