Hesperian Health Guides
Kutumia sheria za kimataifa
HealthWiki > Mwongozo wa jamii juu ya afya ya mazingira > Sehemu ya nne: Kutumia sheria kupigania haki za kimazingira > Kutumia sheria za kimataifa
Mikataba ya kimataifa
Mikataba mingi ya kimataifa hulinda haki za binadamu na mazingira. Kwa bahati mbaya, mtu au kikundi hakiwezi, kwa kawaida, kufungua kesi au shauri mahakamani pale mikataba hiyo inapokiukwa. Ni nchi tu zenye mamlaka ya kidola, na ambazo zilitia saini mikataba hiyo, ambazo zinaweza kulalamika, na hata hivyo ni mara chache hufanya hivyo. Na mikataba hiyo inaweza kutekelezwa dhidi ya serikali lakini siyo mashirika au makampuni ya kimataifa. Hata hivyo, katika nchi nyingi, sheria za kimataifa zinaweza kutumika kwenye mahakama za nchi hizo. Kujifunza kuhusu msimamo ya mikataba hiyo ya kimataifa kunaweza kukusaidia kuelewa misimamo ya jamii ya kimataifa kuhusu masuala mbalimbali ya kimazingira, na kusaidia kuimarisha kampeni za kulinda haki za binadamu.
Iwapo watu watafahamu haki zao na mikataba ambayo nchi nyingi zimeafikiana, wataweza kutekeleza haki zao vizuri na kuzifanya serikali zao kuwajibika.
Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya mikataba ya kimataifa ambayo inalinda haki za binadamu na mazingira, pamoja na tovuti zao ambapo utaweza kupata nakala ya mikataba hii na taarifa zaidi kuhusu jinsi inavyotumika
The United Nations Charter |
The Convention on Biological Diversity
|