Hesperian Health Guides
Kuhifadhi mikondo ya maji na maeneo oevu
HealthWiki > Mwongozo wa jamii juu ya afya ya mazingira > Sehemu ya tano: Kuirudishia ardhi uhai wake na kupanda miti > Kuhifadhi mikondo ya maji na maeneo oevu
Miti na vijito kwenye majiji na miji mara nyingi hulazimika kutiririka kwa uelekeo wa mstari ili kudhibiti mafuriko, na vilevile kurahisisha shughuli za ujenzi kando kando yake. Lakini kadri mto au kijito kinavyozidi kutirika katika mstari ndivyo kasi ya maji inavyoongezeka.Kuongezeka kwa kasi ya maji husababisha mmomonyoko zaidi chini ya mto na kwenye kingo zake, na hivyo kuchangia hatari ya mafuriko maeneo ya chini mto unapoelekea.
Mafuriko hubeba mawe makubwa na magogo. Hata katika msimu wa kiangazi unaweza kujua iwapo mto huo hufurika kutokana na ukubwa wa mawe, magogo na takataka nyingine zilizoachwa kwenye njia ya maji.
Kama mto usiyo na kasi na wenye kina kifupi una mawe makubwa wakati wa kiangazi, hii ni dalili ya hatari ya mafuriko ambayo hubeba mawe hayo makubwa wakati wa msimu wa mvua.
Mto huu utatiririka taratibu, ukiruhusu maji kuingia ardhini. |
Kuhifadhi uhai wa mimea
Plants that grow along waterways help to slow, spread, and sink rainwater into the ground and hold soil in place.
Njia mojawapo ya kuzuia mmomonyoko wa ardhi kandokando ya mito na vijito ni kupanda miti kuizunguka. Panda katika eneo la mita 20 - 50 upana kwa kila upande wa njia ya maji kutapunguza mmomonyoko.
Miti inayopenda mizizi kuwa katika majimaji inakuwa vema kutokana na kukatwa vijiti. Panda miraba 2 au zaidi ya vijiti na tenganisha na matawi katikati ya miraba. Hii inashikilia ardhi mahali pake na kuanza kutengeneza mazingira muafaka kwa mimea na wanyama wengine kurudi.
Miti, vichaka na majani vinaweza kuanza kuota vyenyewe punde tu kingo zinapoanza kuimarika. Vikishindwa kuota vyenyewe, vinafaa kupandwa.
Ikiwezekana weka uzio wa kuzuia wanyama na watu wanaotafuta kuni hadi miti itakapokua kabisa.