Hesperian Health Guides
Sehemu ya tano: Kuirudishia ardhi uhai wake na kupanda miti
HealthWiki > Mwongozo wa jamii juu ya afya ya mazingira > Sehemu ya tano: Kuirudishia ardhi uhai wake na kupanda miti
Katika sura hii:

Baada ya kusoma sehemu ya tano, utakuwa umejifunza: |
|
Jamii zenye afya huwa na uhakika wa huduma ya maji safi na salama, ardhi yenye rutuba, na miti -pamoja na mazao na manufaa yake mengine. Ili kudumisha na kuboresha afya ya jamii, ni muhimu kujifunza namna ya kuponya ardhi iliyoharibiwa na kuitumia kwa uendelevu. Ardhi inapokuwa imeharibiwa, miti yake kuwa imekatwa hovyo na kupoteza udongo wake kupitia mmomonyoko unaosababishwa na upepo na maji, zipo njia nyingi za kuirudishia ardhi hiyo uhai wake na kuiwezesha kuzalisha tena.
Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Juni 2022