Hesperian Health Guides

Mfumo wa matibabu


Katika sura hii:

ngazi tofauti za utoaji huduma za afya kwenye jamii
Wasaidizi wa afya (mapromota, wahamasishaji nk)
wasaidizi wa afya
na wauguzi
madaktari na wauguzi
Siyo kila jamii ina ngazi zote za utoaji huduma za afya. Hata hivyo, huduma tofauti zilizopo, zikiwa na uratibu mzuri, zitawasaidia wanawake (na wagonjwa wengine) kupata huduma bora zaidi za afya.
WWHND Ch3 Page 34-2.png
madaktari,wauguzi,
na wataalam katika tasnia mbalimbali za afya

Huduma muhimu za afya

Mfumo wa utoaji huduma za afya hutoa huduma mbalimbali tofauti. Baadhi ya huduma kama vile upasuaji, "X-ray au Ultrasound" , eksirei, na upimaji magonjwa kwa kutumia mashine za mawimbi sauti yasiyosikika kwa sikio la binadamu (Ultrasound) hupatikana tu kwenye hospitali. Lakini huduma zifuatazo ambazo wanawake wanazihitaji zinapaswa kutolewa kwa gharama nafuu katika ngazi zote za jamii:

  • Elimu na taarifa za afya ili kila mmoja aweze kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya yake , kuweza kutafuta tiba sahihi kwa matatizo ya afya na kuzuia maradhi.
  • Chanjo inayoweza kuzuia maradhi mengi, yakiwemo pepopunda, surua, dondakoo, kifaduro, kupooza, kifua kikuu, na homa ya ini (hepatitis).
  • Huduma kwa ajili ya wajawazito (kabla ya kujifungua) ili kumsaidia mwanamke aweze kugundua na kutibiwa matatizo ambayo yanaweza kuwa yanamdhuru yeye na mtoto wake aliye tumboni kabla hayajawa makubwa.
  • Huduma ya uzazi wa mpango na nyenzo zake . Huduma ya uzazi wa mpango inaweza kuwasaidia wanawake na wanaume kudhibiti idadi ya watoto watakaowazaa, na pia kuacha muda wa kutosha kati ya mtoto mmoja na mwingine.
  • Uchunguzi wa afya afya ili kusaidia kugundua na kutibu magonjwa mapema yakiwemo upungufu wa damu (anemia), shinikizo la juu la damu, na maambukizi kwa njia ya ngono vikiwemo VVU.


Vipimo huweza kutoa taarifa zaidi juu ya chanzo cha tatizo la afya. Baadhi ya vipimo kama kipimo cha saratani (pap test) huhitaji mafunzo ya kitaalam lakini hakihitaji vifaa ghali. Kipimo hiki kinapaswa kutolewa katika ngazi zote za jamii. Baadhi ya vituo vya afya vina maabara zenye vifaa vyenye uwezo wa kutoa majibu ya vipimo vya matatizo ya afya tofauti. Hata hivyo, mara nyingi mwanamke hutakiwa kwenda hospitali kubwa kupata huduma hii. Baadhi ya huduma za afya hupatikana hospitalini tu. Kama mwanamke atakuwa na ugonjwa mkubwa, matatizo kuhusiana na kujifungua au mimba kutoka, au kama atahitaji upasuaji, mara nyingi atahitaji kupelekwa hospitalini haraka.


Ukurasa huu ulihuishwa: 05 Feb 2018