Hesperian Health Guides
Kiambatisho: Chati za maendeleo ya mtoto
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Kuwatunza watoto > Kiambatisho: Chati za maendeleo ya mtoto
In this chapter:
Jinsi ya kutumia chati hizi za maendeleo ya mtoto
Watoto hukua katika nyanja kuu zifuatazo: kimwili, kiakili, kimawasiliano (kutoa ishara au kuongea), na kijamii (kuhusiana na watu wengine). Baadhi ya stadi ambazo mtoto hujifunza hujumuisha nyanja zote hizi. Kwa mfano, mtoto anapotoa mikono wake kwa mtu mwingine, anakuwa anatumia:
- stadi ya kimwili – kuinua mikono yake.
- stadi ya kiakili – anakutambua.
- stadi ya mawasiliano – anakuambia kile anachotaka.
- stadi ya kijamii – anafurahia kubebwa na wewe.
Chati zifuatazo zinaonesha baadhi ya stadi ambazo watoto hujifunza na lini hujifunza. Unaweza kutumia chati hizi kupata taarifa za jumla kuhusu jinsi gani watoto huendelea kutoka hatua moja hadi nyingine na kukusaidia kuamua stadi gani ambazo mtoto anahitaji kujifunza.
Kukusaidia kuamua stadi gani ambazo watoto wanahitaji kujifunzaChagua chati ambayo inakaribia sana umri wa mtoto. Kwenye chati, chora na kuzugushia mdwara stadi ambazo mtoto wako alizonazo. Unaweza kugundua kuwa mwanao hana baadhi ya stadi ambazo watoto wengine wenye umri kama wake wanazo. Kulijua hili kunaweza kukusaida kuamua mazoezi gani ambayo unataka kumshirikisha mtoto.
![]() Miaka
2
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili
hutumia maneno 2 na sentensi zenye maneno 3
Cheza mpira
![]() Baba
Baba
![]() ![]() hutumia maneno mepesi
huiga neno mojamoja au ishara
kikombe
![]() hulinganisha vitu mbalimbali
![]() hutumia vitu mbalimbali vinavyohusiana
![]() hujishughulisha kwa makini na jambo fulani kwa muda mrefu
![]() hucheza pembeni na watoto wengine
![]() humuiga mtoa huduma/mlezi
![]() hutoa rai kwa wengine anapohitaji msaada
![]() hupanga pamoja vitu vikubwa vikubwa
![]() hutembea
![]() huchotama Katika chati iliyooneshwa juu,mama amezungushia midwara stadi ambazo mtoto wake wa miez 20 anaweza kuzifanya. Mtoto wake anahitaji shughuli za kumsaidia kupata stadi za kimwili na mawasiliano.
Kila sehemu ya mdwara huu inaonesha nyanja tofauti ya maendeleo. Picha na maneno ni mifano ya stadi ambazo watoto wengi wanakuwa nazo wanapofikisha miezi 3.
![]() Miezi
3
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili
![]() huonyesha hisia kwa sauti au nyuso alizozizoea
![]() huonyesha hisia kwa sauti au matendo ya ghafla
![]() huwatambua wanaomhudumia
![]() hulia anapokuwa na njaa au kutojisikia vizuri
![]() huweza kutulizwa kwa sauti au mguso/kupapaswa
![]() hutabasamu anaposhirikishwa kwenye mchezo
![]() anatambua mikono
![]() hunyonya ziwa
![]() huinua kichwa juu akiwa amelalia tumbo lake Watoto ambao hawawezi kutenda stadi 2 katika sehemu mojawapo kwenye mduara watanufaika kutokana na shughuli ambazo huwasidia watoto kuendelea katika nyanja hiyo. Lakini picha hizi ni mifano tu ya stadi. Kwa mfano, katika sehemu ya mawasiliano kwenye mduara: siyo lazima upulize zumari! Swali la kujiuliza ni iwapo mtoto wako huitikia sauti ya ghafla(isiyo ya kawaida). Usisahau kwamba mtoto atajifunza vizuri zaidi kwa kufanya shughuli ambazo watoto wengine wa umri wake hufanya katika jamii yako.
Kila sehemu ya mdwara huu inaonesha nyanja tofauti ya maendeleo. Picha na maneno ni mifano ya stadi ambazo watoto wanakuwa nazo wanapokuwa na umri wa miezi 6.
![]() Miezi
6
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili
![]() hutoa sauti na tendo rahisi kuonesha hisia
aaah
![]() hugeuza kichwa kuelekea sauti au tendo
![]() huokota vitu na kuviweka mdomoni
![]() hucheza na vidude vya kuchezea kwa njia mbalimbali
![]() huvutiwa na vitu
![]() huonesha woga mbele ya watu wapya kwake
![]() huonesha rai kutaka uangalizi au huduma
![]() hutambua watu kadhaa
![]() hujiviringisha kutoka tumboni hadi mgongoni na kutoka mgongoni kurudi kulalia tumbo
![]() huweza kukaa kwa msaada
![]() huchezesha na kurusha mikono na miguu Watoto ambao hawawezi kufanya stadi 2 kutoka sehemu mojawapo ya mdwara watanufaika na shughuli za kumsaidia mtoto kuendelea katika Nyanja hiyo. Lakini picha hizi ni mifano tu ya stadi. Kwa mfano, katika sehemu ya stadi za kimwili kwenye mdwara: mtoto wako siyo lazima achezee kinya’nga. Swali la kujiuliza ni iwapo mto wako huchezesha na kurusha viungo vyake. Kumbuka kwamba mtoto atajifunza vizuri zaidi kwa kufanya shughuli amnbazo watoto wengine wenye umri kama wake wanazofanya katika jamii hiyo.
Kila sehemu ya mdwara huonyesha nyanja tofauti ya maendeleo. Picha na maneno ni mifano tu ya stadi ambazo watoto wanakuwa nazo wanapokuwa na umri wa miezi 12.
![]() Miezi
12
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili
huelewa maneno na ishara nyepesi
Nipatie mimi
![]() ![]() ![]() huanza kutamka majina ya vitu
huunganisha sauti
ba-ba
ga-ga wa wa
![]() hujifunza kwamba vitu vipo hata kama havioni kwa macho
![]() hujibidisha kutatua matatizo mepesi
![]() huanza kuelewa sababu (chanzo) na matokeo yake
![]() hutumia matendo au ishara kuonesha hisia
![]() hulia mhudumu wake anapoondoka
![]() huanza kufurahia kucheza na watu wengine
![]() hukaa mwenyewe bila msaada
![]() hutambaa
![]() hujivuta na kusimama mwenyewe
Kumbuka kuwa mtoto atajifunza vizuri kwa kufanya shughuli ambazo watoto wengine wenye umri wake katika jamii yake wanafanya.
Kila sehemu ya mduara huu inaonesha nyanja tofauti ya maendeleo. Picha na maneno ni mifano ya stadi ambazo watoto wengi wanakuwa nazo wanapokuwa na umri wa miaka 2.
![]() Miaka
2
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili
hutumia maneno 2 na sentensi zenye maneno 3
Cheza mpira
![]() Baba
Baba
![]() ![]() hutumia maneno mepesi
huiga neno mojamoja au ishara
kikombe
![]() hulinganisha vitu mbalimbali
![]() hutumia vitu mbalimbali vinavyohusiana
![]() hujishughulisha kwa makini na jambo fulani kwa muda mrefu
![]() hucheza pembeni na watoto wengine
![]() humuiga mtoa huduma/mlezi
![]() hutoa rai kwa wengine anapohitaji msaada
![]() hupanga pamoja vitu vikubwa vikubwa
![]() hutembea
![]() huchotama Watoto ambao hawawezi kutenda stadi 2 kutoka mojawapo ya sehemu kwenye mduara watanufaika kutokana na shughuli ambazo husaidia watoto kuendelea katika nyanja hiyo. Lakini picha ni mifano tu. Kwa mfano, katika sehemu ya stadi za kiakili katika mduara: mtoto wako halazimiki kupiga ngoma. Swali ni iwapo mtoto wako anaweza kutumia vitu 2 kwa mpigo. Kumbuka kuwa mtoto atajifunza vizuri kwa kufanya shughuli ambazo watoto wengine wenye umri wake katika jamii yake wanafanya.
Kila sehemu ya mduara huu inaonesha nyanja tofauti za maendeleo. Picha na maneno ni mifano ya stadi ambazo watoto wengi wanakuwa nazo wanapokuwa na umri wa miaka 3.
![]() Miaka
3
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili
![]() Onesha mdomo wako?
![]() huwasiliana kwa kueleweka
Nataka kwenda na Baba
huelewa sehemu kubwa ya lugha nyepesi
![]() huchomeka vipande vya vitu kwenye mashimo au nafasi zinazoendana
![]() huchambua vitu
![]() hutenganisha vitu na baadaye kuviunganisha pamoja
![]() hupenda kusifiwa baada ya kufanya kazi nyepesi
Ahsante kwa kusaidia
![]() hufurahia kusaidia na kazi za nyumbani
![]() anatambua hisia za watu
![]() hukimbia, huruka na hupanda
![]() hutumia mikono yake kwa kazi zisizo rahisi
![]() hurusha mpira Watoto wadogo ambao hawawezi kutenda stadi 2 kutoka sehemu mojawapo sehemu kwenye mduara watanufaika kutokana na shughuli ambazo husaidia watoto kuendelea katika nyanja hiyo. Lakini picha hizi ni mifano tu ya stadi. Kwa mfano, katika nyanja ya stadi za kijamii: mtoto wako halazimiki kufagia. Swali la kujiuliza ni iwapo mtoto wako anafurahia kusaidia na kazi za nyumbani. Kumbuka kuwa mtoto atajifunza vizuri kwa kufanya shughuli ambazo watoto wengine wenye umri wake katika jamii yake wanafanya.
Kila sehemu ya mduara huu inaonesha nyanja tofauti ya maendeleo. Picha na maneno ni mifano ya stadi ambazo watoto wengi wanakuwa nazo wanapokuwa na umri wa miaka 5.
![]() Miaka
5
Stadi za mawasiliano
Stadi za kiakili
Stadi za kijamii
Stadi za kimwili
![]() Nilianguka kwenye maji.
![]() huuliza maswali mengi
Nani wapo kule? Wanafanya nini ?
huzungumzia au kuonesha ishara ya kile alichokifanya
![]() hufuata malekezo rahisi
![]() hutanzua chemshabongo nyepesi
![]() huelewa kuhesabu
![]() huelewa kanuni au amri
![]() hucheza na watoto wengine
![]() Nasikitika.
Pole sana.
huonesha hisia nyingi
![]() hunakili na kuchora sura au umbo rahisi
![]() huweza kutembea kinyumenyume kwa urahisi
![]() huruka kwa mguu mmoja
Watoto wadogo ambao hawawezi kutenda stadi 2 kutoka sehemu mojawapo sehemu kwenye mduara watanufaika kutokana na shughuli ambazo husaidia watoto kuendelea katika nyanja hiyo. Lakini picha hizi ni mifano tu ya stadi. Kwa mfano, katika nyanja ya stadi za kijamii: mtoto wako hapaswi kufanya tendo la kumsikiliza mwalimu. Swali la kujiuliza ni iwapo mtoto wako anaelewa kanuni au amri kama ilivyo kwa watoto wengine. Kumbuka kuwa mtoto atajifunza vizuri kwa kufanya shughuli ambazo watoto wengine wenye umri wake katika jamii yake wanafanya.
|