Hesperian Health Guides

Njia za uzazi wa mpango

Katika sura hii:

Sura hii inaelezea njia tofauti za uzazi wa mpango. Kwa ajili ya taarifa juu ya njia zingine za uzazi wa mpango, na zile ambazo hazitumiki sana, angalia Sura ya 13 ya kitabu Mahali wanawake hawana daktari (Where Women Have No Doctor) au Sura ya 17 ya Kitabu kwa ajili ya wakunga (A Book for Midwives) ambavyo vinapatikana kutoka Hesperian.

Jinsi ya kuchagua njia ya uzazi wa mpango

Njia zote tofauti za uzazi wa mpango zina manufaa na mapungufu. Ni muhimu kuongea na mwenzi wako, wanawake wengine, au mfanyakazi wa afya juu ya njia tofauti kukusaidia kuchangua njia inayokufaa. Baadhi ya mambo ambayo unatakiwa kuzingatia katika kuchagua njia ya uzazi wa mpango ni pamoja na:

  • Ina ufanisi kiasi gani katika kuzuia mimba?.
  • Ina ufanisi kiasi gani katika kukinga dhidi ya magonjwa ya ngono?.
  • Kama mwenzi wako anaafiki matumizi ya njia hiyo ya uzazi wa mpango, au kama unapaswa kuficha asijue.
  • Kama njia hiyo inapatikana kwa urahisi, na mara ngapi unatakiwa kiutumia katika muda fulani.
  • Inagharimu kiasi gani ?.
  • Kama ina madhara ya pembeni.
  • Kama una mahitaji na wasi-wasi mwingine. Kwa mfano: unanyonyesha? Bado unahitaji watoto zaidi ?
padri akiongea na mwanamke ambaye anafikiria jambo.
Una haki wewe mwenyewe kufanya maamuzi yanayohusu uzazi wa mpango.


NJIA YA UZAZI WA
MPANGO
Uwezo wa
kuzuia
mimba
Uwezo wa
kukinga
dhidi ya
maambukizi
kupitia
ngono
Matumizi
yake
Maelezo mengine muhimu
Kondom

FPChart-1.png
Mkubwa Mkubwa zaidi Wakati wote Hufanya kazi kwa ufanisi zaidi inapotumika na dawa ya kuua mbegu za kiume na kilainishi cha asili ya maji. Kondom hutakiwa kutumika kila mara unapofanya tendo la ngono.
Vidonge vya majira-Vidonge mseto

HAW Ch7 Page 191-6.png
Mkubwa sana Sifuri Kila siku Hufanya kazi vizuri zaidi inapotumika muda ule ule kila siku. Wanawake wenye matatizo ya kiafya yafuatayo hawapaswi kutumia njia hii.
Vidonge vya majira (vyenye homoni moja-siyo mseto)

HAW Ch7 Page 191-6.png
Mkubwa sana Sifuri Kila siku Hufanya kazi pale tu inapotumiwa saa ile ile kila siku. Inaweza kutumiwa hata na wanawake wanaonyonyesha (anza angalau baada ya mtoto kufikisha wiki 6).
Vijiti

FPChart-6.png
Mkubwa zaidi Sifuri Miaka 3 hadi 5 Lazima vingizwe na kutolewa na mfanyakazi wa afya ambaye amepitia mafunzo maalum na kubadilishwa kila baada ya miaka 3 au 5 kutegemea na aina ya vijiti.
Sindano

HAW Ch7 Page 191-5.png
Mkubwa sana Sifuri Mwezi 1, 2, au 3 Inatakiwa kurudiwa kila baada ya mwezi 1, 2, au 3 (kutegemea na aina ya sindano).
Kitanzi

FPChart-7.png
Mkubwa zaidi Sifuri Miaka 5 au 12 Hufanya kazi kwa muda wa miaka 5 au 12 (kutegemea na aina ). Lazima kiingizwe na kutolewa na mfanyakazi wa afya ambaye amepitia maafunzo maalum.
Kuchomoa uume mwanaume anapofikia kileleni

FPChart-13.png
Mdogo sana Sifuri Wakati wote Mwanaume anatakiwa kuchomoa uume wake haraka anapofika kileleni kila mara mnapofanya tendo la ngono. Hata kama atachomoa uume, majimaji kidogo kutoka umeni yanaweza kuingia ukeni wakati wa tendo la ngono na kusababisha mimba kutunga, hali ambayo pia inaweza kusababisha maambukizi yanayopitia ngono.
Unyonyeshaji (wakati wakati wa miezi miezi 6 tu ya kwanza) Mkubwa sana Sifuri Mara kadhaa mchana na usiku Njia hii hufanya kazi tu kama mwanamke ananyonyesha mtoto wake maziwa ya mama tu na kama hedhi zake hazijaanza tena.
Njia ya kuhesabu siku (kushika mimba)

FPChart-10.png
Mkubwa Sifuri Kila mara Njia hii haifanyi kazi vizuri kwa wanawake wenye mzunguko wa hedhi unaobadilika.
Tendo la ngono lisilohusisha uume kuingizwa kwenye uke Mkubwa zaidi Inategemea Kila mara Kama uume haugusi uke, mwanamke hawezi kupata mimba. Ngono kwa njia ya haja kubwa inaweza kusababisha maambukizi kwa urahisi. Ngono kwa njia ya mdomo ina uwezekano mdogo wa kusababisha maambukizi ya magonjwa yanayopitia ngono. Mguso tu wa kingono bila kuingiliana ni nadra kusababisha maambukizi yoyote.
Kufunga kizazi kabisa Mkubwa zaidi Sifuri Mara moja Mara mwanamke au mwanaume anapofunga kizazi kabisa, hatabeba mimba au kusababisha mimba tena.


Mara nyingi watu hutumia njia tofauti kutegemea na mazingira yao.


mwanamke akiongea
Sitaki kulazimika kufanya kitu kila siku.
mwanamke akiongea
Sitaki kuwa naweka vitu kwenye uke wangu.
Unaweza kuchagua : Njia ya vijiti, sindano, kitanzi Unaweza kuchagua : Vidonge vya majira, njia ya vijiti, kondomu za kiume, kuhesabu siku
Unaweza kuepuka: Njia ya vidonge vya majira, njia ya kuhesabu siku Unaweza kuepuka: Kondomu ya kike, kitanzi
mwanamke akiongea
Sitaki wazazi
wangu kujua kwamba natumia njia za uzazi wa mpango.
mwanamke na mwanume wakiongea
Sihitaji watoto zaidi.
Kulea watoto 2 inatosha kwangu.
Unaweza kuchagua: sindano, kondomu Unaweza kuchagua: Njia ya vijiti, njia ya sindano, kitanzi, mwanaume au mwanamke kufunga kizazi kabisa
Unaweza kuepuka: Vidonge vya majira Unaweza kuepuka: Njia ya kuhesabu siku
Mwanamke akiongea
Nataka kupata mtoto baada ya mwaka mmoja, lakini siyo sasa.
Mwanaume akiongea
Nimefanya ngono na wanawake wengine na nataka kumkinga mke wangu dhidi ya VVU.
Unaweza kuchagua: Kondomu, vidonge vya majira na kuhesabu siku Unaweza kuchagua: Njia ya kutumia kondomu kila mara
Unaweza kuepuka: Njia ya vijiti, sindano, kitanzi, kufunga kizazi kabisa Epuka : Kufanya ngono bila kutumia kondomu
Mtu anaweza kutumia zaidi ya njia moja.
mwanamke akiongea.
Tunatumia njia ya kuhesabu siku, na kwenye siku zangu zenye uwezekano mkubwa wa kupata mimba, huwa tunatumia kondomu kuzuia mimba.
mwanamke akiongea
Mpenzi wangu wa kike hutumia njia ya sindano na huwa tunatumia kondomu kuzuia uwezekano wa maambukizi kupitia ngono.

Kondomu

NWTND FP Page 8-1.png

Kondomu ni kimfuko laini chembamba ambacho mwanaume huvaa kwenye uume wake wakati wa kufanya tendo la ngono. Shahawa za mwanaume hubaki ndani ya kondomu, na hivyo haziwezi kuingia ukeni na kusababisha mimba. Kondomu ni salama na hazina madhara ya pembeni.

Kondomu ni njia yenye uwezo mkubwa zaidi wa kuzuia maambukizi ya magonjwa ya ngono, ukiwemo VVU. Hata kama unatumia njia nyingine ya uzazi wa mpango, unaweza wakati huohuo kutumia kondomu kwa ajili ya kujikinga wewe na mwenzi wako dhidi ya magonjwa yanayoambukizwa kupitia ngono.

NWTND FP Page 8-2.png

Kondomu ndiyo njia pekee ya uzazi wa mpango ambayo inaweza, kwa kiwango kikubwa, kuzuia mimba na kukinga dhidi ya maambukizi kupitia ngono kwa wakati mmoja. Lakini mwanaume lazima awe tayari kutumia kondomu kila mara atakapofanya ngono.

NWTND FP Page 8-3.png

Minya ncha ya kondomu na kuivalisha kwa kuviringisha juu ya uume uliosimama. Ncha ya chini yenye nafasi hupokea shahawa za mwanaume baada ya kuachiwa. (Kama hutaacha nafasi kwa ajili ya shahawa, kondomu inaweza kupasuka.)

Baada ya kufikia kileleni, ume ungali bado umesimama, shikilia kondomu kwa juu ili ibaki kwenye ume wakati ukichomoa ume kutoka ukeni. Baada ya hapo, toa kondomu kwenye ume. (Tupa kondomu kwenye chombo cha taka – usitupe kondomu hovyo ili watu wengine wasiiguse au kuiokota!) Tumia kondomu mpya kila mara unapofanya tendo la ngono.

Kondomu ya kike

MW Ch17 Page 303-7.png
Pete la mpira huingizwa ndani ya uke.
Pete la nje hubaki nje ya uke.

Kondomu ya kike hufitishwa kwenye uke na kufunika mlango wa uke. Ni kubwa kuliko kondomu ya kiume na uwezekano wa kuvunjika ni mdogo sana. Kondomu za kike hutoa kinga dhidi ya VVU na maambukizi mengine ya ngono.Usitumie kondomu ya kiume na ya kike kwa pamoja katika tendo la ngono.

NWTND FP Page 8-4.png
NWTND FP Page 8-5.png
NWTND FP Page 8-6.png

Dawa za kuua mbegu za kiume (Spermicide)

Dawa za kuua mbegu za kiume kwenye shahawa zinaweza kuwa katika mfumo wa povu, vidonge, mafuta ya krimu, jeli au vidonge ambavyo huyeyuka kwenye uke na kuua mbegu za kiume ili zisiweze kurutubisha yai.

Kifaa cha kuingizia dawa Sw NWTND FP Page 9-1.png
NWTND FP Page 9-2.png
NWTND FP Page 9-3.png


Dawa za kuua mbegu huingizwa ukeni mara kabla ya tendo la ngono. Dawa haifanyi kazi vizuri ikitumika peke yake, lakini hutoa kinga zaidi dhidi ya mimba inapotumika pamoja na kondomu. Dawa za kuua mbegu za kiume hazitoi kinga dhidi ya maambukizi yanayopitia kwenye ngono au VVU.

Vidonge vya kuzuia mimba (vidonge vya majira)

Vidonge vya kuzuia mimba vina homoni ambazo zinafanana na homoni za asili kwenye mwili wa mwanamke. Huzuia mimba kwa kusimamisha ovari za mwanamke kuachia yai. Kuna aina kuu 2 za vidonge vya majira: vidonge mseto vyenye homoni 2, estrojeni na projestini, na vidonge vidogo ambavyo vina homoni moja tu ya projestini. Baadhi ya majina ya kibiashara maarufu yanaoneshwa kwenye sehemu ya Vidonge vya majira vya kumeza. Vidonge vya majira havitoi kinga dhidi ya VVU au maambukizi mengine kupitia ngono. Ili uweze kujilinda dhidi ya magonjwa hayo, unapaswa kutumia pamoja na kondomu.

Baadhi ya wanawake huamua kutumia vidonge vya majira kwa sababu vidonge hivyo husaidia kuweka vizuri mpangilio wa hedhi, ili waweze kujua lini siku zao za hedhi zitaanza. Vidonge vya majira pia hupunguza wingi wa damu ya hedhi, na mabonge ya damu na maumivu wakati wa hedhi.

Vidonge vya majira havisabishi saratani.

Vidonge vya majira mseto (vyenye homoni za estrojeni na projestini)

NWTND FP Page 10-1.png

Aina tofauti za vidonge mseto vya majira vina dozi tofauti za homoni hizi mbili. Kuna mseto wenye dozi za kawaida kama vile miligramu 1 au chini yake ya projestini na maikrogramu 30 au 35 za estrojeni (ethinyl estradiol), au maikrogramu 50 ya estrojeni nyingine iitwayo mestranol.

Baadhi ya vidonge vya majira vina homoni ya projestini tu.

Vidonge vya majira hufanya kazi vizuri kuzuia mimba vinapotumika kila siku na muda ule ule. Ni salama kwa wanawake walio wengi.

Jinsi ya kutumia vidonge mseto vya majira

mwanamke akitumia vidonge vya majira.

Kama una uhakika kuwa huna ujauzito, unaweza kuanza kutumia vidonge vya majira wakati wote. Vidonge vya majira havitazuia mimba hadi uwe umekua ukivitumia angalau kwa wiki. Hivyo katika siku 7 za mwanzo baada ya kuanza kutumia vidonge vya majira, tumia kondomu au epuka ngono.

Unatakiwa kutumia kidonge 1 cha majira kila siku kuzuia mimba, hata kama hutafanya tendo la ngono siku hiyo. Jitahidi kutumia kidonge muda ule ule kila siku. Kuweka vidonge mahali unapolala, kunaweza kukusaidia kukumbuka kumeza kidonge kila siku kabla hujalala. Aina nyingi za vidonge vya majira mseto huwa katika paketi ya vidonge 28 au 21.

Madhara ya pembeni ambayo yanaweza kuhusiana na vidonge mseto vya majira

Madhara ya pembeni siyo hatari sana lakini mengine yanaweza kukera. Kawaida hupungua au kutoweka baada ya miezi 3. Wakati mwingine unaweza kujaribu aina nyingine ya vidonge vya majira.

Mabadiliko katika hisia kama vile kuhisi huzuni au kuudhika kwa urahisi NWTND FP Page 10-3.png Maumivu ya kichwa NWTND FP Page 10-4.png Kutokwa na damu kidogo katikati ya vipindi vya kawaida vya hedhi.
NWTND FP Page 10-7.png
Matiti kuvimba na kuuma NWTND FP Page 10-5.png Kichefuchefu NWTND FP Page 10-6.png

Vidongo mseto vya majira vinaweza kutumika kupitia njia 3

Kutumia siku 28: Tumia vidonge vyenye homoni kwa siku 21 na baada ya hapo, kwa siku 7, tumia vidonge vilivyobaki. (Vidonge vya ziada kwenye paketi havina homoni), au usitumie tena vidonge. Utakuwa unapata hedhi kila mwezi wakati wa siku hizo 7 kama hedhi nyingine ya kawaida.

mwanamke akitumia vidonge vya majira.
NWTND FP Page 11-2.png
Kama una paketi ya siku 28, tumia kidonge 1 kila siku. Vidonge 7 vya mwisho ni kwa ajili ya kukukumbusha kuwa havina homoni – Vimewekwa kukusaidia kukumbuka kutumia kidonge cha majira kila siku. Vidonge 7 vya mwisho kwenye paketi vitakuwa vya rangi tofauti.
NWTND FP Page 11-3.png
Kama una paketi ya siku 21, tumia kidonge 1 kila siku kwa siku 21 – paketi nzima. Basi usitumie kidonge kwa siku 7. Anza paketi nyingine.


Matumizi ya muda mrefu: Tumia vidonge vyenye homoni kwa siku 84 vinavyofuatana na baada ya hapo pumzika kwa siku 7. Wakati mwingine vidonge huwa kwenye paketi zenye vidonge 91 (84 vyenye homoni na 7 kwa ajili ya kukumbusha tu ambavyo havina homoni). Wakati wa siku hizo 7, utakuwa unapata hedhi kama inavyokuwa katika hedhi ya kawaida lakini mara moja tu katika kipindi cha miezi 3. Matone ya damu (hedhi nyepesi sana) yanaweza kutokea lakini hutoweka baada ya miezi michache.

Matumizi endelevu: Tumia vidonge vyenye homoni kila siku bila kuacha. Kama utaona usumbufu na hedhi isiyotabirika, acha kutumia vidonge kwa siku 3 au 4 ili kupata siku chache za hedhi ya kawaida, halafu endelea kutumia kidonge tena kila siku.

Utaratibu wote huu wa kutumia vidonge mseto ni salama. Mtu yeyote ambaye anatumia vidonge mseto vya majira anatakiwa kujua afanye nini kama ataruka kemeza kidonge kimoja au viwili:

Kama utasahau kumeza kidonge 1 au 2, tumia kidonge 1 haraka mara utakapokumbuka. Baada ya hapo tumia kidonge kinachofuata katika muda wa kawaida. Hii inaweza kumaanisha kwamba utatumia vidonge 2 katika siku moja.

Kama utasahau kutumia vidonge 3, siku 3 zinazofuatana, tumia kidonge 1 mara moja. Baada ya hapo, tumia kidonge 1 kila siku katika muda ule ule. Tumia kondomu hadi utakapoanza hedhi yako, au usifanye ngono hadi utakapokuwa umetumia kidonge kila siku kwa siku 7 mfululizo.

Kama hedhi yako haitakuja muda wake wa kawaida na umesahau kumeza baadhi ya vidonge, endelea kutumia vidonge vyako, lakini pata kipimo cha mimba. Kama utakuta una mimba, simamisha kutumia vidonge.

Kusitisha matumizi ya vidonge mseto vya majira

Unaweza kusimamisha matumizi ya vidonge wakati wote. Unaweza kupata mimba mara moja, hivyo iwapo unataka kuepuka kupata mimba, tumia kondomu au njia nyingine.

Nani hapaswi kutumia vidonge mseto vya majira

Baadhi ya wanawake wana matatizo ya kiafya na matumizi ya vidonge mseto vya majira vinaweza kuhatarisha maisha yao. Usitumie vidonge mseto vya majira iwapo:

  • Una tatizo la presha kubwa ya juu (160/110 au juu zaidi). Angalia Magonjwa ya moyo (kinaandaliwa) kwa ajili ya taarifa zaidi juu ya tatizo la Shinikizo la Presha ya Juu.
  • Ugonjwa wa kisukari kwa zaidi ya miaka 20.
  • Kama una zaidi ya miaka 35 na ni mvutaji wa sigara.
  • Tatizo la maumivu makali ya kichwa (maumivu ya kichwa makali yakiambatana na kichefuchefu) kama yakiambatana na kufa ganzi au na matatizo makubwa katika kuona.
  • Saratani ya matiti, saratani ya ini, au saratani ya kibofu cha mkojo.
  • Ugonjwa wa kibofu cha nyongo.
  • Uliwahi kupatwa na kiharusi.
  • Damu kuganda kwenye mshipa (hali hii kawaida husababisha joto na maumivu kwenye mguu mmoja).
  • Ugonjwa wa ini au homa ya manjano au hepatitis.


Wanawake wengi wenye tatizo moja la kiafya wanaweza kutumia kwa usalama vidonge vya majira vyenye projestini tu au njia ya vijiti au sindano za projestini tu. Wanawake wenye ugonjwa wa saratani ya matiti au saratani ya tumboni hawapaswi kutumia njia za uzazi wa mpango zenye homoni, na badala yake watumie njia nyingine.

Dawa ambazo zinaingiliana na vidonge mseto vya majira

Rifampicin (dawa ya kifua kikuu), ritonavir (dawa ya VVU) na baadhi ya dawa za kifafa huathiri utendaji wa vidonge vya majira. Kama utatumia dawa hizi, chagua njia tofauti ya uzazi wa mpango. Wanawake wanaotumia insulini kwa ajili ya kisukari wanaweza kuhitaji kurekebisha kiasi cha insulini baada ya kuanza kutumia vidonge vya majira.

Nani wanapaswa kufikiria njia zingine kama zipo

Kuna matatizo machache ya kiafya ambayo hufanya njia ya vidonge vya mseto vya majira kutofaa baadhi ya watu. Ni bora zaidi kwa wanawake wenye matatizo haya kutumia njia nyingine ya kupanga uzazi:

  • Tatizo la shinikizo la juu la damu-presha ya juu (zaidi ya 140/90). Angalia Ugonjwa wa moyo (kinaandaliwa) kwa taarifa zaidi juu ya shinikizo la juu la damu.
  • Kama una zaidi ya miaka 35 na una matatizo ya kuumwa kichwa (maumivu ya kichwa yanayoambatana na kichefuchefu).


Kama mwanamke mwenye matatizo atatumia vidonge mseto vya majira, angaliwe kwa karibu kuhakikisha matatizo hayo ya kiafya yasizidi. Kama hakuna mabadiliko, basi ni bora kuendelea kutumia vidonge mseto vya majira. Kama matatizo yataongezeka, asimamishe mara moja kutumia vidonge hivyo haraka.

Kidonge kidogo chenye projestini tu

Kidonge hiki cha majira hakina homoni ya estrojeni, kina projestini tu. Ni salama kwa wanawake wengi ambao hawawezi kutumia vidonge mseto vya majira na vina madhara ya pembeni kidogo kuliko vidonge mseto. Kidonge kidogo cha majira hakipunguzi maziwa kwa wanawake wanaonyonyesha. Wanawake wanaotumia kidonge kidogo wanaweza kupata mabadiliko katika tarehe za hedhi, damu kidogo kati ya kipindi cha hedhi kimoja na kingine, au kukosa hedhi kabisa.

NWTND FP Page 14-1.png
Vidonge vyote kwenye paketi ya vidonge vidogo vya majira vina kiwango sawa cha homoni. Tumia kidonge 1 kila siku.

Jinsi ya kutumia kidonge kidogo cha majira

Tumia kidonge chako cha kwanza kwenye siku yako ya kwanza ya hedhi. Halafu tumia kidonge kimoja muda huo huo kila siku, hata kama hutafanya tendo la ngono. Utakapomaliza paketi, anza paketi mpya siku inayofuata, hata kama hujapata damu yotote. Usiruke siku. Kila kidonge kina kiasi sawa cha homoni ya projestini.

Kama utatumia kidonge kidogo hata baada ya kuchelewa saa chache, au kama utasahau kidonge cha siku 1, unaweza kupata mimba. Kama utakosa kutumia kidonge, kitumie haraka mara utakapokumbuka. Halafu tumia kidonge kinachofuata katika muda ule wa kawaida, hata kama itamaanisha kutumia vidonge 2 katika siku moja. Tumia kondomu au usifanye ngono kwa siku 7. Unaweza kutokwa na damu kidogo kama hutatumia kidonge chako kidogo au unapokitumia ukiwa umechelewa.

Madhara ya pembeni ya vidonge vidogo vya majira

Madhara ya kawaida kwa vidonge vyenye homoni moja ya projestini (vidonge vidogo) ni mabadiliko katika mpangilio wa hedhi ya kila mwezi. Unaweza kupata damu wakati hutarajii. Hedhi inaweza kutopatikana kabisa. Hii siyo hatari. Madhara mengine yanaweza kujumuisha kuongezeka uzito, kuumwa kichwa, na vipele vidogo mwilini.

Dawa zinazoingiliana na kidonge kidogo cha majira

Rifampicin (dawa ya kifua kikuu), ritonavir (dawa ya VVU) na baadhi ya dawa za kifafa huathiri utendaji wa vidonge vya majira. Kama utatumia dawa hizi, chagua njia tofauti ya uzazi wa mpango. Wanawake wanaotumia insulini kwa ajili ya kisukari wanaweza kuhitaji kurekebisha kiasi cha insulini baada ya kuanza kutumia vidonge vya majira.

Kusitisha matumizi ya vidonge vidogo vya majira

Kama unataka kupata mimba au kubadilisha njia ya kuzuia mimba, unaweza kuacha kutumia vidonge vidogo vya majira wakati wote. Unaweza kupata mimba mara baada kusimamisha vidonge hivyo. Kama unataka kuepuka mimba, anza njia nyingine mara moja.