Hesperian Health Guides

Minyoo

Katika sura hii:

Minyoo ndani ya utumbo wetu huishi kwa chakula tunachokula na damu yetu. Husababisha tumbo kukata na kuhara, na hutunyonya lishe na nishati. Mtoto mwenye maambukizi makubwa ya minyoo anaweza kupatwa na ugonjwa wa anemia (upungufu wa madini chuma) au upungufu wa vitamini A. Hupata shida shuleni na katika kufanya kazi za kawaida nyumbani, kutokana na maumivu ambayo huathiri umakini wake kimasomo.

Aina tofauti ya minyoo huingia kwenye miili yetu kwa njia tofauti, huishi muda tofauti, husababisha matatizo tofauti, na inaweza kuhitaji dawa tofauti. Jaribu kutafiti njia bora zaidi zinazotumika kuzuia na kutibu minyoo katika eneo lako. (Na kama utatafsiri au kutumia kitabu hiki kwa ajili ya kuelimisha katika mazingira yako, ingiza maelezo zaidi kuhusu aina halisi ya minyoo inayoathiri sana eneo lako). Lakini kwa ujumla, maambukizi yanaweza kuzuiwa kwa:

  • Kutumia vyoo ili kuboresha usafi wa mazingira.
  • Kunawa mikono kwa maji safi na sabuni. Tunza kucha zako zikiwa fupi ili zisihifadhi uchafu ndani.
  • Kuchemsha nyama vizuri kabla ya kula. Usiwalishe mifugo wako nyama mbichi au kinyesi.
  • Kuvaa viatu au sendo.
  • Kuwapatia watoto chini ya mwaka 1 dawa za minyoo za albendazo au mebendazo kila baada ya miezi 3 hadi 6.

Minyoo inayoenea kutoka kinyesi hadi mdomoni: askarisi (roundworm), mchangokiboko (whipworm), mchangouzi (pinworm)

Askarisi
(Roundworm)
mnyoo mrefu na mnene
Urefu wa sentimeta 20 hadi 30, rangi ya pinki au nyeupe.
Mchangokiboko (Whipworm, Trichuris, Trichocephalus)
mnyoo mdogo na mwembamba sana kwenye ncha ya upande mmoja
Urefu wa sentimeta 3 hadi 5, rangi ya pinki au grei.
Mchangouzi
(Pinworm, threadworm, seatworm (Enterobius)
minyoo midogo na miembamba 3
Sentimeta 1 kwa urefu, mieupe, miembamba sana na inafanana na uzi.

Jinsi minyoo hii inavyoenea

Kawaida, kiinyesi kidogo hubaki mkononi mtu anapojitawaza au kujipangusa baada ya kujisaidia, au anapojikuna baada ya kuwashwa nyuma. Au kinyesi kilichotupwa au kuachwa hovyo juu ya ardhi kinaweza kusafirishwa na kuingizwa ndani ya nyumba na wanyama, watoto, au kwenye miguu, viatu au kandambili. Baada ya hapo, minyoo, au mayai yaliyopo kwenye kinyesi, huingia chini ya kucha au kwenye ngozi. Minyoo hiyo na mayai yake huingia mdomoni pale:

NWTND bag Page 32-4.png
NWTND bag Page 32-5.png
NWTND bag Page 32-6.png
Mtoto anapoingiza mikono au vidole vyake mdomoni. Mtu anapokamata chakula wakati wakupika au kuandaa chakula cha familia au wateja. Mtu yoyote anapogusa mdomo wake au mdomo wa mtu mwingine.

Mayai ya minyoo ni madogo sana na hayawezi kuonekana kwa macho-hii ndiyo sababu huenezwa kwa urahisi


Matibabu

Tibu askarisi (roundworm), mchangokiboko (trichuris, whipworm), safura(hookworm), au mchangouzi (pinworm), kwa mebendazo kwa muda wa siku 3. Katika maeneo yanayoathiriwa sana na minyoo ya aina hii, rudia matibabu kila baada ya miezi 3 hadi 6.

Epuka kutumia sibendazo (thiabendazole) kutibu askarisi. Dawa hii inaweza kusababisha minyoo hiyo kupanda hadi puani au mdomoni na kumkaba, na shida katika kupumua.

Unaweza kutibu minyoo hii kwa kutumia dawa zilizotengenezwa nyumbani. Kula kitunguu-saumu kidogo au mbegu za papai zilizosagwa kila siku husaidia kuua minyoo.

Kuzuia
katuni ikionesha choo kikifukuza minyoo
mtoto akijikuna kwenye unyeo wakati akimpa mtoto mwenzake kipande cha chakula

Mkakati muhimu na bora zaidi dhidi ya minyoo ni kuzuia maambukizi. Bila hatua za uzuiaji pamoja na kuzingatia usafi, maambukizi ya minyoo yatamrudia mtu mara kwa mara.

Minyoo: Jenga choo kisafi na chenye faragha ya kutosha kwa ajili ya kujisaidia mbali na nyumba na chanzo cha maji ya kunywa. Ukifanya hivyo watoto na wanyama hawataweza kubeba na kungiza kinyesi ndani ya nyumba. Bonyeza hapa kuhusu jinsi ya kujenga vyoo rahisi na salama.

Nawa mikono yako kwa maji safi na sabuni, na kuwasaidia watoto pia kunawa mikono yao: Nawa vizuri kwa kutumia maji safi na sabuni, au majivu. Nawa kabla ya kuandaa chakula na kabla ya kula, na kila baada ya kujisaidia.

Wasaidie watoto kunawa mikono yao mara nyingi zaidi hata kuliko watu wakubwa-kwa kuwa hupenda kukamata kila kitu na mara nyingi kuweka vidole vyao mdomoni.

Kama mtoto anajikuna unyeo kwa sababu ya minyoo, ni rahisi kujiambukiza au mkuwaabukiza wengine. Kuzuia hali hii:

  • Kata kucha za mtoto ili kinyesi na mayai ya minyoo yasijibanze chini yake.
  • Mnawishe mikono mtoto vizuri asubuhi kila siku, kabla hajala, na baada ya kujisaidia.
  • Mvalishe mtoto chupi wakati wa mchana. Mvalishe nepi au chupi kabla hajaenda kulala — ili asijikune kwenye unyeo anapokua amelala.
  • Zuia muwasho kwa kutumia mafuta ya Vaseline kwenye unyeo kabla hajalala.


Nawa mikono baada ya kugusa kinyesi: Kama unawahudumia watoto au mtu mzima mgonjwa, tupa kinyesi chao chooni. Wanawishe sehemu zao za nyuma baada ya kujisaidia. Na wewe nawa mikono yako kwa uangalifu. Kwa taarifa zaidi juu ya jinsi ya kuzuia minyoo na magonjwa mengine, angalia Maji na usafi wa mazingira.

Baadhi ya matatizo yanayosababishwa na minyoo

mvulana mdogo mwenye tumbo ambalo limevimba
Mtoto mwenye minyoo mingi anaweza kuwa na tumbo gumu ambalo limevimba.

Askarisi (Roundworm): Maambukizi makali ya minyoo aina ya askarisi yasiyotibiwa yanaweza kusababisha matatizo kwenye utumbo na katika kupumua. Minyoo michanga huchimba ndani ya mapafu, na kusababisha sauti kama ya filimbi wakati wa kupumua , kikohozi kavu, au nimonia ikiambatana na kukohoa damu. Mtu mwenye hali kama hiyo anahitaji msaada wa kiafya haraka.

Mtu anapokua na homa, au anapoanza kutumia dawa ya minyoo, minyoo inaweza kutoka kupitia kinyesi au kujivuta yenyewe na kutokea mdomoni au puani. Mara chache, hali hii husababisha msongo wa pumzi.

Kwa nadra, minyoo ya askarisi husababisha utumbo kuziba. Tafuta msaada wa kiafya. Wakati ukitafuta msaada wa daktari, mpatie mebendazo au albendazo.

Mchangokiboko (Whipworm): Mchangokiboko unaweza kusababisha kuhara, wakati mwingine ukiambatana na damu. Katika maambukizi makali, hali hii inaweza kuchangia ugonjwa wa anemia (ukosefu wa madini chuma kwenye damu).

Mchangokiboko unaweza kusababisha mtoto kutumia nguvu nyingi kusukuma kinyesi wakati wa kujisaidia. Hali hii inaweza kusababisha sehemu ya utumbo wa mtoto kutoka nje ya unyeo. Ukimwagiwa maji baridi unaweza kurudi ndani. Kama hii itashindikana, sukuma polepole urudi ndani.

Minyoo ambayo huenea kwa kula nyama ambayo haijapikwa na kuiva vizuri:
tegukamba(tapeworm) na trichina

vipande vya aina mbalimbali za tegu
cmnyoo aina ya trichina uliojiviringisha husababisha trikinosisi(trichinosis
Tegu, na vipande vya tegu. Minyoo hii ina rangi inayoelekea kwenye weupe au njano na urefu wa mitaa kadhaa. Kutegemea na aina ya tegu, unaweza kuviona vipande vya aina hii ya minyoo kwenye kinyesi. Minyoo aina ya trichina hauwezi kuonekana kwenye kinyesi, lakini kama ungeweza kuonekana ungekuwa na sura hii ukiwa umejichimbia kwenye misuli ya binadamu.

Minyoo ya tegu na trichina huenezwa kwa kula nyama ambayo haijaiva – hasa nyama ya nguruwe. Samaki, ng’ombe, na wanyama wanaokula wanyama wengine wanaweza pia kueneza aina tofauti za minyoo hii.

Tegu

Mduara wa maisha ya tegu ni kama ifuatavyo::

Mayai ya tegu katika kinyesi cha binadamu huendelea na kutengeneza vifuko vyenye viluwiluwi ndani ya mwili wa nguruwe

1. Mtu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri. Vijidudu vya tegu kwenye nyama hugeuka kuwa minyoo ndani ya utumbo wake.
2. Minyoo ya tegu hutaga maelfu ya mayai ndani ya utumbo wake.
3. Nguruwe hula kinyesi cha mwanadamu na mayai ndani ya kinyesi hicho.
4. Mayai hayo huenea kwenye mwili mzima wa nguruwe, yakitengeneza vifuko vyenye viluwiluwi vya minyoo ndani ya misuli yake.
Mayai ambayo huingia mdomoni wa mwanadamu (kwa mfano, kama ana tabia ya kutonawa mikono yake baada ya kujisaidia), yanaweza kutengeneza vifuko vyenye viluwiluwi vya minyoo hata kwenye ubongo wake. Hali hii inaweza kusababisha maumivu ya kichwa, shambulio (tukutiko), au kifo.
vipande vya minyoo
mayai
vifuko vyenye viluwiluwi vya minyoo

Kama utakuta kipande bapa kidogo cheupe cha tegu kwenye kinyesi au nguo ya ndani, anza matibabu ya tegu mara moja.

Matibabu (maambukizi ya mnyoo aina ya trichina )
mwanaume ambaye amepoteza fahamu akiwa amelala chini

Tibu kwa kutumia dawa ya niclosamide au praziquantel. Kama shambulio(tukutiko) litatokea , tafuta msaada wa daktari haraka. Mgonjwa atahitaji dawa za za kupambana na shambulio na zingine kutoka kundi la steroidi (steroid).

Trikinosisi (ugonjwa ambao husababishwa na mnyoo aina ya trichina)

Ndani ya wiki ya kula nyama yenye maambukizi, mtu mwenye trikinosisi anaweza kuanza kupata maumivu tumboni, kichefuchefu, na kuhara. Kama kila mtu aliyekula nyama hiyo anaumwa tumbo ndani ya wiki mmoja ya kula nyama hiyo, tafuta tiba kwa ajili ya trikinosisi.

Baada ya wiki moja, maambukizi yanaweza kuenea kwenye misuli au ubongo na kusababisha:

  • Homa na baridi.
  • Maumivu ya misuli au kwenye maungo.
  • Uvimbe kuzunguka macho na wa miguu.
  • Uvujaji kwenye sehemu nyeupeya macho, maumivu machoni, au matatizo katika kuona.
  • Michubuko midogomidogo.
Matibabu

Tibu kwa kutumia dawa ya albendazo au mebendazo. Dawa za steroidi pia zinaweza kuhitajika.

Kuzuia tegu na trikinosisi
nguruwe akila kinyesi
  • Weka banda la nguruwe mbali na nyumba – ili kinyesi chao kisiingie ndani ya nyumba au kuguswa na watoto.
  • Usiwalishe nguruwe nyama mbichi au kinyesi, au maambukizi yatafuatia.
  • Pika nyama iweze kuiva vizuri, hasa nyama ya nguruwe. Kupika vizuri huua vifuko vyenye viluwiluwi vya minyoo vilivyoko kwenye nyama.
  • Nawa mikono yako baada ya kujisaidia na kabla ya kupika chakula au kula.
minyoo 2 midogo
miekundu na yenye urefu wa sentimeta 1

Safura (hookworm)

Safura ni miongoni mwa magonjwa hatari zaidi ya utotoni, kwa sababu huishi kwa damu ya mtoto na hivyo inaweza kusababisha anemia. Mtoto mwenye anemia, ambaye rangi yake imefifia, au anakula uchafu anaweza kuwa na minyoo aina ya tegu. Kama inawezekana kinyesi chake kinapaswa kupimwa kujua iwapo ana minyoo hii au la.

Jinsi minyoo ya safura inavyoenea (anza na 1 chini)

mwili mtupu wa mvulana ukionesha miguu, mapafu, koo, tumbo, na utumbo
1.
Minyoo ya safura huingia kupitia miguu isiyovalishwa viatu. Hii inaweza kusababisha alama nyekundu kwenye miguu na muwasho.
2. Katika siku chache, minyoo hiyo hufika kwenye mapafu kwa njia ya damu. Hii inaweza kusababisha kikohozi kikavu (kwa nadra kikiwa na damu).
3. Mgonjwa anaweza kukohoa minyoo midogo na baadaye kuimeza.
4. Siku chache baadaye, mgonjwa anaweza kuanza kuhara au kupatwa na maumivu ya tumbo.
5. Minyoo ya safura hujibanza kwenye kuta za utumbo.Minyoo mingi inaweza kusababisha udhaifu na anemia kali.
6. Mayai ya minyoo ya safura hutoka kwenye mwili wa binadamu kupitia kinyesi. Mayai hayo huangua katika udongo wenye unyevu.


Matibabu

Tumia mebendazo kutibu safura.

Tibu anemia kwa kula vyakula vyenye chuma kwa wingi na pia tumia vidonge vya madini chuma.

mtoto akijisaidia chooni Wakinge watoto dhidi ya safura: Jenga vyoo na kuvaa sendo au viatu.
miguu iliyovalishwa viatu na sendo