Hesperian Health Guides

Maji na usafi wa mazingira: Funguo za kudumisha afya

HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Maji na usafi wa mazingira

Katika sura hii:

Matatizo mengi yanayotufanya tuugue yanaweza kuzuilika. Baadhi ya njia za kuzuia magonjwa huhitaji muda, juhudi na fedha zaidi mwanzoni, lakini hunusuru muda na fedha baadae kwa kutuepeusha na magonjwa.

Sura hii inaelezea jinsi ya kuzuia kuharisha na magonjwa mengine yanayosababishwa na vijidudu vilivyomo kwenye kinyesi cha binadamu na wanyama. Matatizo mengi yanayoathiri tumbo na matumbo yanaweza kuepukwa kwa kunawa mikono, kuzingatia usafi katika kuandaa na kuhifadhi chakula, kutumia vyoo kwa usahihi, na kunywa maji safi na salama.

Ili kujifunza jinsi ya kuzuia:

  • utapiamlo, kisukari, ugonjwa wa moyo, na matatizo mengine yanayosababishwa na lishe duni, angalia Lishe bora hutengeneza afya bora.
  • nimonia au kichomi,kifua kikuu, na matatizo mengine ya kupumua angalia Matatizo katika kupumua na kikohozi (kinaandaliwa).
  • matatizo ya kiafya yanayosababishwa na utupaji hovyo wa taka za kawaida na taka zingine, angalia Taka za kawaida, taka za hospitalini na uchafuzi wa mazingira (kinaandaliwa).
  • malaria, homa ya denge, na magonjwa mengine yanayoambukizwa kupitia mbu, angalia Baadhi ya magonjwa hatari ya kuambukizwa (kinaandaliwa).

Jinsi ugonjwa wa kuharisha unavyoenea

Vijidudu na minyoo hueneza ugonjwa wa kuharisha kwa kusafiri njia zifuatazo kutoka kwenye kinyesi cha binadamu na wanyama:

mishale ikionesha njia zinazofuatwa na vijidudu kutoka kwenye kinyesi hadi mdomoni
vidole
nzi
mashamba
kinyesi
chakula
mdomo
majimaji


Vijidudu vya magonjwa pia husambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa kuwa wanafamilia huishi pamoja, vijidudu na magonjwa yanaweza kuenea kwa urahisi kwa familia nzima.

mbwa akiwa amesimama kwenye maji
 mtoto akimgusa mbwa
mama amechuchumaa karibu na mtoto
1. Mvua kubwa zinaweza kusababisha mfereji wazi wa maji machafu kutoka chooni kufurika. Mbwa anayepita mitaani kwenye maji hayo anaweza kubeba kinyesi kwenye miguu yake.
2. Mbwa anaweza kuingia ndani ya nyumba, mtoto kucheza naye na kujipaka kinyesi kwenye mikono yake.
3. Baadaye mtoto analia na mama yake kumbembeleza. Mtoto anakamata sketi ya mama yake na kuichafua na kinyesi.
mtu akisindika chapati
mwanaume, mwanamke na watoto wao wawili wakionekana wanaumwa
4. Mama mwenye majukumu mengi anaanza kuandaa chakula cha jioni. Anatumia sketi yake iliyochafuliwa kukinga mikono yake isiungue wakati wa kuepua chakula.
5. Familia inakula na baada ya muda mfupi kila mtu anaanza kuharisha.


Kitu gani kingezuia familia isiugue?

Kama hali mojawapo ingekuwepo, ugonjwa huu ungedhibitiwa usienee:

  • Kama jamii isingekuwa na mifereji iliyowazi ya maji machafu kutoka chooni.
  • Kama mbwa hakuruhusiwa kuingia ndani ya nyumba.
  • Kama familia ingemsaidia mtoto kunawa mikono yake.
  • Kama mtoto asingejipangusia mikono yake kwenye sketi ya mama yake.