Hesperian Health Guides

Sura ya 2: Kutatua matatizo ya afya

HealthWiki > Pale ambapo Wanawake hawana Daktari > Sura ya 2: Kutatua matatizo ya afya

Wanawake 2 wakisoma kitabu pamoja

Baadhi ya matatizo ya afya lazima yatibiwe na wafanyakazi wa afya wenye uzoefu. Lakini matatizo mengi ya afya yanaweza kutibiwa nyumbani au kuzuilika kwa kuishi maisha yanayozingatia afya.

Mwanamke anapokuwa na dalili za tatizo la afya, anahitaji taarifa ili kutatua tatizo hilo. Anahitaji kujua tatizo hilo ni nini, sababu zake, ni nini kinaweza kufanyika kulitibu, na namna ya kuzuia lisitokee tena.

Katika sura hii tunasimulia hadithi ya mwanamke mmoja aitwaye Juanita, jinsi alivyoweza kutatua tatizo lake la afya. Ingawaje ufafanuzi unamhusu Juanita, namna anavyofikiria kuhusu tatizo lake na jitihada za kulitatua, lakini inaweza pia kutumika kwa matatizo mengine ya afya. Unaweza kutumia njia hii wewe mwenyewe kutatua tatizo la afya au kufanya maamuzi kuhusu kupata matibabu mazuri zaidi.

Juanita aligundua kwamba suluhisho la kudumu kwa tatizo lake la afya ni kuwa na mtizamo mpana zaidi ya kuangalia hali yake mwenyewe. Pia alihitaji kuainisha kiini cha tatizo katika jamii na nchi yake. Kama Juanita, wewe na jamii yako mnaweza kutumia njia hii kuainisha sababu zote za afya duni ya wanawake – na kupanga njia za kuifanya jamii yako kuwa sehemu yenye afya bora zaidi kwa wanawake.Ukurasa huu ulihuishwa: 05 Feb 2018