Hesperian Health Guides
Mfumo wa uzazi wa mwanamke
HealthWiki > Pale ambapo Wanawake hawana Daktari > Sura ya 4: Kuielewa miili yetu > Mfumo wa uzazi wa mwanamke
Mchoro ufuatao unaonesha jinsi mlango wa uke unavyoonekana na namna sehemu tofauti zinavyojulikana. Lakini kila mwili wa mwanamke ni tofauti. Kuna tofauti katika ukubwa, sura, na rangi ya viungo, hasa mikunjo ya nje na ndani.
Matiti
Matiti yameumbika kwa umbo na ukubwa tofauti. Matiti huanza kuota binti anapofikisha umri kati ya miaka 10 na 15, anapobadilika kutoka usichana kuwa mwanamke kwa kuanza kupata hedhi. Matiti hutengeneza na kutoa maziwa kwa ajili ya mtoto baada ya kujifungua. Yakitomaswa kimapenzi, mwili wa mwanamke husisimka na uke hutoa ute au majimaji tayari kwa ajili ya tendo la ngono.
Ndani ya titi:
Tezi hutengeneza maziwa.
Mirija hupitisha maziwa kwenda kwenye chuchu.
Mifuko yakuhifadhi maziwa hadi mtoto atakapoyanyonya.
Chuchu hutoa maziwa nje. Wakati mwingine umbo la chuchu huchomoza kwa nje na nyingine ni bapa.
Ngozi nyeusi yenye vituta vidogo vidogo kuzunguka chuchu. Vituta vidogo vidogo hivyo hutengeneza mafuta ambayo husaidia kutunza chuchu ikiwa laini na katika hali ya usafi.
Ukurasa huu ulihuishwa: 05 Jan 2024