Hesperian Health Guides
Jinsi mwili wa mwanamke unavyobadilika
HealthWiki > Pale ambapo Wanawake hawana Daktari > Sura ya 4: Kuielewa miili yetu > Jinsi mwili wa mwanamke unavyobadilika
Mwili wa mwanamke hupitia mabadiliko mengi muhimu katika kipindi cha uhai wake – wakati wa kupevuka,wakati wa balehe, wakati wa ujauzito na unyonyeshaji, na wakati hedhi inapokomaa-umri wa kutoweza kuzaa tena.
Zaidi ya hayo, wakati wa umri wa kuzaa, mwili wake hubadilika kila mwezi – kabla, wakati na baada ya hedhi ya kila mwezi. hedhi yake ya kila mwezi. Sehemu za mwili ambapo mabadiliko haya hutokea ni ukeni, mji wa mimba(kizazi), ovari, mirija ya mayai ya uzazi, kwenye matiti-sehemu zote hizo huitwa mfumo wa uzazi. Mabadiliko haya mengi husababishwa na kemikali za asili maalum ziitwazo homoni.