Hesperian Health Guides

Kusimamisha utokaji damu miongoni mwa watoto wachanga

Vitamini K, fitomenadioni (phytomenadione), fitonadioni (phytonadione)


Mwili hutumia vitamini K kugandisha damu na kusimamisha uvujaji damu. Lakini watoto huzaliwa na kiwango kidogo cha vitamini K. Hivyo uvujaji damu ukitokea kwa sababu yoyote ile, unaweza kushindwa kudhibitiwa. Kama mtoto ataanza kuvuja damu kutoka sehemu yoyote ile ya mwili wake (mdomoni, kwenye kitomvu, njia ya haja kubwa), unaweza kumpa vitamini K kuzuia uvujaji kuongezeka. Unaweza pia kuwapa vitamini K watoto wanaozaliwa na uzito mdogo au watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao (chini ya kilogramu 2) kuzuia uvujaji damu kwa sababu wako katika hatari kubwa ya kuvuja damu. Vitamini K haizui uvujaji damu kwa watoto wenye umri mkubwa zaidi au watu wazima.

Jinsi ya kutumiaNBgrninject.png

Toa kwa njia ya sindano miligramu 1 (miligramu 1, au ½ miligramu 2) za vitamini K kwenye sehemu ya nje ya paja ndani ya saa 2 baada ya kujifungua.

Usichome dawa zaidi, haitawasaidia na inaweza kuwasababishia madhara.