Hesperian Health Guides
Kwa ajili ya matibabu ya maambukizi ya kuvu au ukungu
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Watoto wachanga na unyonyeshaji > Kwa ajili ya matibabu ya maambukizi ya kuvu au ukungu
Jiivi au methrosaniliamu kloraidi
Jiivi ni dawa isiyo ghali kwa ajili ya matibabu ya maambukizi ya kuvu au ukungu mdomoni, kwenye chuchu za mama ambaye ananyonyesha, ndani ya mkunjo wa ngozi, au kwenye mlango wa uke au ndani ya uke. Dawa hiyo pia hutumika kupambana na maambukizi yanayosababishwa na bakteria kwenye ngozi.

Dawa ya Jiivi inaweza kuathiri ngozi na kusababisha vidonda inapotumika mdomoni au ukeni. Simamisha matumizi kama upele au vidonda vitatokea.

Jiivi hugeuza kila kitu kuwa rangi ya zambarau. Hupungua baada ya siku chache lakini inaweza kutia nguo madoa ya kudumu.

Iwapo maambukizi hayataanza kupona ndani ya siku chache, jaribu dawa nyingine.
Nistatini (Nystatin)
Nistatini hufanya kazi vizuri kama tiba ya maambukizi mengi ya fangasi mdomoni, kwenye chuchu au ngozi au ukeni. Kwa ajili ya matumizi ya mdomoni, nistatini inakuwa katika mfumo wa majimaji, poda ambayo huchanganywa na maji, au pipi. Kwa ajili ya ngozi, nistatini inakuwa katika mfumo wa losheni au mafuta, matone au poda. Kwa ajili ya maambukizi ya kuvu au ukungu ukeni, nistatini huwa katika mfumo wa vidonge vya kuingiza ukeni au mafuta yanayoingizwa ukeni.

Ngozi inaweza kuanza kuwasha mahali nistatini inapotumika. Jambo hili hujitokeza mara kwa mara. Simamisha matumizi kama utapata upele. Dawa ya nistatini wakati mwingine pia husababisha kuharisha.

Maambukizi ya aina ya fangasi ambayo hayapungui baada ya kutumia nistatini, au ambayo hutoweka na kurudi tena, huenda yakawa dalili ya VVU.

Kwa mtoto mchanga mwenye ukungu/kuvu mdomoni