Hesperian Health Guides

Watoto wachanga na unyonyeshaji: Madawa

Watoto wachanga na unyonyeshaji: Madawa

Dawa za antibiotiki (viua vijasumu) hupambana na maambukizi

Ampisilini na amoksilini


Ampisilini na amoksilini ni dawa za penisilini zenye tiba pana, maana yake ni kwamba zinaweza kuwa aina nyingi za bakteria. Dawa hizi mbili mara nyingi hutumika kama mbadala wa nyingine. Ukiona pendekezo la kutumia ampisilini katika kitabu hiki, kawaida unaweza kutumia amoksilini katika nafasi yake, kwa kuzingatia kipimo sahihi (angalia chini).

Ampisilini na amoksilini ni salama sana na msaada mkubwa hasa kwa watoto wachanga na watoto wenye umri mkubwa zaidi. Dawa zote mbili husaidia katika kutibu kichomi (nimonia) au maambukizi sikioni. Ampisilini pia ni muhimu katika kutibu homa ya uti wa mgongo na maambukizi mengine makali kwa watoto wachanga.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Dawa zote hizi mbili, lakini hasa ampisilini, huwa na mwelekeo wa kusababisha kichefuchefu na kuharisha. Epuka kuwapa watoto ambao tayari wanaharisha. Unaweza kuwapa dawa nyingine.

Madhara mengine ya pembeni ni upele. Lakini uvimbe vimbe unaowasha kwenye ngozi ya mwili ambao huja na kutoweka ndani ya saa kadhaa huenda ni dalili ya mzio wa dawa ya penisilini. Simamisha matibabu ya dawa hiyo mara moja na usimpe mtoto huyu dawa ya penisilini tena. Madhara ya baadaye kutokana na mzio yanaweza kuwa mabaya zaidi na hata kutishia maisha. Kwa ajili ya matatizo kama hayo, dawa ya erithromaisini inaweza kutumika baada ya kuanza kutumia dawa na kuchukua siku kadhaa kutoweka, siyo lazima iwe dalili ya mzio. Lakini haiwezekani kujua bayana kama upele huo umetokana na mzio au la. Hivyo ni bora zaidi kusimamisha matumizi ya dawa hiyo.

MuhimuNBgrnimportant.png

Usugu wa mwili dhidi ya dawa hizi unazidi kuwa jambo la kawaida. Kutegemea na mahali unapoishi, dawa hizi zinaweza kutofanya kazi tena dhidi ya magojwa kadhaa yakiwemo maambukizi ya bakteria kwenye ngozi au sehemu za ukeni /umeni na njia ya mkojo, na ugonjwa wa kuhara ukichanganyika na damu unaosababishwa na bakteria ya, shigella, na maambukizi mengine.

Jinsi ya kutumiaNBgrninjectpill.png

Ampisilini na amoksilini hufanya kazi vizuri zinapotumiwa kwa njia ya mdomo. Ili kumpa vidonge mtoto, saga vidonge hivyo au toa unga kwenye ganda na kugawanya ili kupata kiasi cha dawa unachohitaji. Halafu changanya unga huo wa dawa katika maziwa kidogo kutoka titi la mamake. Mpatie mtoto maziwa yaliyochanganywa na dawa kwa kutumia kikombe au kijiko. Ampisilini inaweza kutolewa pia kwa njia ya sindano, lakini inapaswa kutumika tu dhidi ya magonjwa makali kama vile homa ya uti wa mgongo, au wakati mgonjwa anatapika au hawezi kumeza.

Kama zilivyo antibiotiki zingine, toa dawa hii kwa muda wa siku chache kama ilivyopendekezwa hapa. Kama mgonjwa bado anazo dalili za maambukizi, aendelee kutumia kiasi kile kile cha dawa hadi saa 24 baada ya dalili zote kutoweka. Kama mgonjwa ametumia dawa hiyo kwa muda wa juu zaidi uliopendekezwa na bado anaonesha dalili za maambukizi, simamisha dawa hiyo na tafuta msaada wa daktari. Kwa watu wenye VVU, kila mara mpe dawa kwa muda wa siku zote kama ilivyoorodheshwa. Vilevile, kiwango cha antibiotiki anachopewa mgonjwa hutegemea umri na uzito wake na ukali wa maambukizi. Kwa ujumla, toa dozi ya chini iliyopendekezwa kwa mtu mwembamba au kwa ajili ya maambukizi ambayo siyo makali sana, na dozi kubwa zaidi iliyopendekezwa kwa mtu mwenye uzito mkubwa zaidi au dhidi ya maambukizi makali zaidi.

AMOKSILINI
Kwa ajili ya maambukizi mengi ya watoto wachanga.
Toa miligramu 62, mara 3 kwa siku, kwa siku moja hadi siku 7. Kila dozi:
¼ ya kidonge chenye ganda cha miligramu 250 AU
½ kijiko cha chai (mililita 2.5) cha dawa ya maji ya miligramu 125 au mililita 5 AU
¼ kijiko cha chai (miligramu 1.25) chaa dawa ya maji ya miligramu 250 au mililita 5.
AMPISILINI
Kwa ajili ya maambukizi mengi ya watoto wachanga
Mpe miligramu 125, mara 3 kwa siku kwa muda wa siku 3 hadi 7. Kila dozi ni:
½ ya kidonge chenye ganda chenye miligramu 250 AU
Kijiko 1 cha chai (miligramu 5) cha dawa ya maji ya miligramu 125/mililita 5.

Kwa ajili ya maambukizi makali kwa watoto wachanga kama vile uti wa mgongo
Choma sindano yenye mchanganyiko wa dawa ya ampisilini na jentamaisini (gentamicin) pembeni kwenye msuli wa paja. Angalia Dawa, vipimo na matibabu (kinaadaliwa) jinsi ya kuchoma sindano. Changanya kichupa cha ampisilini cha miligramu 500 na mililita 2.5 za maji yaliyotakaswa. Hii itatengeneza mchanganyiko wenye ukali wa miligramu 500 kwa kila milita 2.5.

Tumia kichupa cha gentamaisni miligramu 2 ambayo haijachanganywa kwa kiwango cha miligramu 40 kwa kila mililita.

MuhimuNBgrnimportant.png

Dawa ya Jentamaisini lazima itolewe kwa kuzingatia usahihi wa dozi kamili. Kipimo cha dawa kikizidi huweza kusababisha uharibifu wa figo au uziwi wa kudumu na hivyo inapaswa kutumika kwa dharura wakati unatafuta msaada wa daktari. Kama mtoto amepungukiwa na maji mwilini, mpe maziwa ya mama na kinywaji maalum cha kumuongezea maji mwilini haraka.

Kwa mtoto mwenye chini ya umri wa wiki moja
AMPISILINI: Choma miligramu 50 kwa kilo, mara 2 kwa siku, angalau kwa siku 5,
NA
JENTAMAISINI: Choma miligramu 5 kwa kilo, mara moja kwa siku, angalau kwa siku 5. Usitoe kwa zaidi ya siku 10.
Kwa mtoto mwenye umri wa wiki 1 hadi mwezi 1
AMPISILINI: Choma miligramu 50 kwa kilo, mara 3 kwa siku, angalau kwa siku 5,
NA
JENTAMAISINI: Choma miligramu 7.5 kwa kila kilo ya uzito, mara moja kwa siku, angalau kwa siku 5. Usitoe kwa zaidi ya siku 10.

Erithromaisini


Erithromaisini hufanya kazi dhidi ya maambukizi mengi kama penisilini na inaweza kutumika kama mbadala kwa wale wote wanaopata mzio kutokana na penisilini. Kwa maambukizi mengi inaweza kutumika kama mbadala wa tetrasaikilini. Inaweza pia kutumika dhidi ya dondakoo na kifaduro (aina ya kikohozi kikali kinachosababishwa na bakteria ambao huwaandama sana watoto).

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Erithromaisini mara nyingi husababisha kichefuchefu na kuharisha, hasa miongoni mwa watoto. Usitumie kwa zaidi ya wiki 2 kwa sababu inaweza kusababisha nyongo ya manjano.

Jinsi ya kutumiaNBgrnspoon.png
Kwa watoto wachanga hadi mwezi 1
Toa miligramu 30 hadi 50 kwa kila kilo ya uzito wa mwili kila siku, ikigawanywa katika dozi 3 kwa siku. Toa dawa kwa siku 10 hadi 14.
Kwa mtoto mchanga wa uzito wa wastani wa kilo 3, kila dozi inapaswa kuwa:
Miligramu 0.75 (hii ni zaidi kidogo ya theluthi nane - ⅛ ya kijiko cha chai) ya dawa ya maji ya enthromaisini yenye miligramu 250/mililita 5, AU
Miligramu 62 ¼ ya kidonge cha miligramu 250) kilichosagwa na kuchanganywa kwenye maziwa kutoka titi la mama au kwenye maji.
Kwa maambukizi ya titi (uvimbe wa titi) kwa mama ambaye ananyonyesha
Mpe miligramu 250 hadi 500 (kidonge 1 au 2 vya miligramu 250), mara 4 kwa siku, kwa siku 10.

Seftriakzoni (ceftriaxone)


Seftriakzoni ipo katika kundi la antibiotiki za sefalosporini (cephalosporin). Kundi hili la antibiotiki hufanya kazi dhidi ya aina nyingi za bakteria. Kawaida ni ghali na hazipatikani kila mahali. Hata hivyo, huwa zina athari na madhara ya pembeni kidogo kuliko aina nyingi za antibiotiki na ni muhimu katika kutibu magonjwa makali kadhaa ukiwemo sepsisi (maambukizi ya sumu ya kidonda kwenye damu) na homa ya uti wa mgongo, na maambukizi mengine ambayo ni sugu kwa penisilini. Tumia tu seftriakzoni kutibu maambukizi mahsusi mabyo yamependekezwa katika eneo lako. Hii itasaidia kuzuia usugu na dawa hiyo kuendelea kutumika kwa ufanisi.

Seftriakzoni ni dawa kali ambayo inaweza kutumika kutibu sepsisi na homa ya uti wa mgongo. Seftriakzoni hasa husaidia sana katika kutibu kisonono, yakiwemo maambukizi ya kisonono machoni mwa watoto wachanga, lakini wasipewe watoto wachanga chini ya wiki 1 na ni bora kuiepuka kwa watoto chini ya mwezi 1.

MuhimuNBgrnimportant.png

Usitoe dawa ya seftriakzoni kwa mtoto mwenye chini ya wiki moja. Epuka pia kuwapa watoto ambao walizaliwa njiti au wakiwa na uzito mdogo. Usitoe dawa hii iwapo kuna dalili ya nyongo ya manjano (jaundice).

Jinsi ya kutumiaNBgrninject.png

Seftriakzoni hutolewa tu kupitia sindano au kwa njia ya dripu (kwenye mshipa wa damu). Uchomaji wa sindano ya seftriakzoni unaweza kuambatana na maumivu. Changanya na asilimia moja ya lidokeni (lidocaine) kama unajua jinsi ya kuichanganya.

Kwa ajili ya matibabu ya maambukizi ya kisonono machoni kwa watoto wachanga wenye umri wa siku 7 au zaidi
Choma kupitia sindano miligramu 50 kwa kila kilogramu ya uzito wa mwili, mara moja tu. Usitoe zaidi ya miligramu 125.
Kwa maambukizi makali kwa mtoto mchanga au mtoto zaidi ya siku 7 iwapo dawa zingine za antibiotiki hazipo
Toa kwa njia ya sindano miligramu 75 kwa kila kilogramu moja ya uzito wa mwili, mara moja kwa siku, kwa siku 7 hadi 10 . Hivyo:
Kwa mtoto mchanga mwenye kilogramu 3, choma miligramu 225 mara moja kwa siku.
Kwa mtoto mkubwa zaidi mwenye kilogramu 6, choma miligramu 450 mara moja kwa siku.