Hesperian Health Guides

Credits

The Swahili Translation Team:

Note: The first five chapters was lead by this team the rest of the book is a project of COBIHESA.
Project Coordinator: Felicity Louise Wales
Translator: Callistus Mshauri & Brenda Kiwia
Editor: David Katusabe and the COBIHESA team
Art & Design Coordinator: Felicity Louise Wales
Proofreaders: Brenda Jubilant & Emma Sway
Field Testers: Emma Sway & Stella Simeon Lomayani
Donors/Fundraisers: Felicity Louise Wales

Shukrani nyingi kwa wote waliotajwa hapo juu na wote ambao wametia moyo na kuunga mkono mradi huu kuanzia mwanzo wa kutafsiri hadi hatua ya kutoa nakala ya kwanza na sasa kinapatikana kwa lugha ya Kiswahili kuweza kutumika maeneo ya Afrika Mashariki. Shukrani za pekee ziende kwa wote waume kwa wake, na watoto wa boma la Masai la ndugu Lucumay Laizer Oltovuai ambao walituruhusu kuwashirikisha katika kufanya majaribio ya kazi hii. Bila ya ridhaa yao ya kukubali kukaa na kusikiliza kitabu hiki katika toleo la Kiswahili, tusingeweza kuelewa ni mambo gani yanayopaswa na yasiyopaswa kujumuishwa katika kitabu hiki. Hili kwa kweli lilikuwa jambo la ajabu na zuri sana kwao kwani wengi walivutiwa kushiriki na hata kufanya tasfiri kwa lugha ya kimasai kwa ajili ya wale ambao hawakuelewa Kiswahili na hivyo kuwezesha kushiriki pamoja. Tuligundua kwamba tafsiri iliweza kueleweka kirahisi na kwamba ni mambo yaliyohusu maisha yao ya kila siku ya jamii. Pia kama siyo wao tusingeweza kugundua ni jinsi gani taarifa hii ni ya manufaa kwao na kwamba tayari ilikwisha anza kuleta mabadiliko katika maisha yao na kuathiri namna ambavyo huwatenda wanawake na wasichana katika jamii zao. Kukiwa na mipango ya kujenga kituo kidogo cha jamii cha mafunzo chenye zahanati katika boma lao, tunatumaini kwamba tutaweza kusambaza hii kazi nzuri kuweza kwenda mbali zaidi katika jamii nyingine na hata maeneo yote ya Afrika Mashariki.