Hesperian Health Guides

Kwa nini baadhi ya wanawake hutoa mimba?

Katika sura hii:

Kutoa mimba kawaida ni uamuzi mgumu. Baadhi ya dini hufundisha kuwa utoaji mimba siyo sahihi na katika nchi nyingi utoaji mimba hauruhusiwi kisheria na siyo salama. Lakini kuna sababu nyingi kwa nini mwanamke anaweza kujaribu kutoa mimba. Hapa chini ni mifano kadhaa:

  • Tayari anapokuwa na watoto ambao anaweza kuwahudumia.
  • Ujauzito huo unapokuwa hatari kwa afya au maisha yake.
  • Hana mwenzi wa kumsaidia kumhudumia mtoto atakayezaliwa.
  • Anataka kwanza kumaliza shule.
  • Hataki kupata watoto.
  • Alipata mimba baada ya kubakwa.
  • Kuna mtu ambaye anamlazimisha kuitoa mimba.
  • Mtoto atazaliwa na matatizo makubwa ya kiafya au kimaumbile.
  • Ana VVU au UKIMWI.


Njia za Uzazi wa Mpango wakati wa dharura

Mwanamke ambaye amefanya ngono pasipo kutumia kinga ndani ya siku 3 anaweza kuzuia kupata ujauzito kama atachukua hatua haraka. Angalia Njia za dharura za uzazi wa mpango.


Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Mei 2017