Hesperian Health Guides

Kuwatunza watoto: Madawa

Kuwatunza watoto: Madawa

Dawa za maumivu na homa

Dawa kwa ajili ya maumivu ya kawaida na kupunguza homa ni pamoja na parasetamo (dawa ambayo ni salama zaidi kwa watoto), asprini, na ibrofeni. Aspirini na ibrofeni pia hupunguza uvimbe (uvimbe). Hivyo, kwa mfano, ukijisokota kifundo cha mguu kwa bahati mbaya, dawa hizi hazitasaidia tu kuondoa maumivu, lakini pia kupunguza uvimbe. Hii husaidia kupona haraka. Lakini watoto wenye homa na maambukizi ya aina ya virusi hawapaswi kutumia asipirini.

Usitoe zaidi ya dozi ya dawa iliopendekezwa. Dawa zote hizi zinaweza kuwa na madhara iwapo utazidisha kiwango. Kwa mfano, matumizi makubwa ya asipirini na ibrofeni yanaweza kusababisha vidonda vya tumbo. Parasetamo ikizidi hugeuka kuwa sumu. Kwa ajili homa kali au maumivu, unaweza kuepuka kutumia kiasi kikubwa kwa kuchanganya parasetamo na iburofeni.

Parasetamo, asetaminofeni


Parasetamo ni dawa nzuri, na yenye gharama nafuu kwa ajili ya homa na maumivu ya kawaida.

MuhimuNBgrnimportant.png

Usitumie zaidi ya kiwango cha dawa kilichopendekezwa. Dawa ikizidi, hutengeneza sumu kwenye ini na inaweza kuua. Weka dawa mbali na watoto, hasa kama ni ya maji na tamutamu.

Dawa baridi mara nyingi huwa na parasetamo ndani yake, hivyo usitoe dawa hizo iwapo pia unatoa parasetamo ama sivyo utazidisha kiwango.

Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png
Toa miligramu 10 hadi 15 kwa kilo, kila baada ya saa 4 hadi 6. Usitoe dawa zaidi ya mara 5 ndani ya saa 24. Kama huwezi kumpima mtoto, toa dozi kwa kuzingatia umri:
Chini ya mwaka 1: toa miligramu 62 (⅛ ya kidonge cha miligramu 500), kila saa 4 hadi 6.
Mwaka1 hadi 2: toa miligramu 125 (¼ ya kidonge cha miligramu 500), kila saa 4 hadi 6.
Miaka 3 hadi 7: toa miligramu 250 (½ ya kidonge cha miligramu 500), kila saa 4 hadi 6.
Miaka 8 hadi 12: toa miligramu 375 (¾ ya kidonge cha miligramu 500), kila saa 4 hadi 6.

Ibuprofeni


Ibuprofeni huondoa maumivu ya misuli, maungo (jointi), na kichwa, na hupunguza homa.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Ibuprofeni inaweza kusababisha maumivu tumboni, lakini kutumia dawa hiyo pamoja na maziwa au chakula hupunguza tatizo hilo.

MuhimuNBgrnimportant.png

Usitumie ibuprofeni iwapo una tatizo la mzio kutokana na aspirini. Baadhi ya watu wanaopata mzio kutokana na dawa moja pia hupata mzio wanapotumia dawa hiyo nyingine. Usitoe ibuprofeni kwa watoto wenye umri chini ya miezi 6.

Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png
Mpe miligramu 5 hadi 10 kwa kilo. Kama huwezi kumpima mtoto, mpe dozi kulingana na umri.
Miezi 6 hadi mwaka 1: mpe miligramu 50, kila saa 6 hadi 8.
Mwaka 1 hadi 2: mpe miligramu 75, kila saa 6 hadi 8.
Miaka 2 hadi 3: mpe miligramu 100, kila saa 6 hadi 8.
Miaka 4 hadi 5: mpe miligramu 150, kila saa 6 hadi 8.
Miaka 6 hadi 8: mpe miligramu 200, kila saa 6 hadi 8.
Miaka 9 hadi 10: mpe miligramu 250, kila saa 6 hadi 8.
Miaka 11: mpe miligramu 300, kila saa 6 hadi 8.
Zaidi ya miaka 12: mpe miligramu 200 hadi 400, kila saa 4 hadi 6.

Usitoe zaidi ya miligramu 40 kila kilo kwa siku. Usitoe zaidi ya dozi 4 kwa siku, na usitoe kwa zaidi ya siku 10.