Hesperian Health Guides

Dawa kwa ajili ya kutibu hali mbaya inayotangulia kifafa cha mimba na mashambulio

Ujauzito na kujifungua: Madawa

Magneziamu salfeti


Magneziamu salfeti ndiyo dawa bora zaidi ya kutibu mashambulio au matikishiko ya maungo miongoni mwa wanawake wajawazito wenye tatizo la kifafa cha mimba. Kama huwezi kupata magneziamu salfeti tumia diazipamu badala yake.

MuhimuNBgrnimportant.png

Tumia magneziamu salfeti pale tu kipimo cha shinikizo la damu kwa mwanamke ni zaidi ya 160/110 (hali mbaya inayotangulia kifafa cha mimba), au kama amepatwa na shambulio.

Hesabu pumzi kabla na baada ya kutoa dawa.Usimpe dawa hii iwapo pumzi zake ni chini ya 12 kwa dakika. Usimpe dozi ya pili kama pumzi zake zitashuka chini ya 12 kwa dakika, au kama mama hawezi kukojoa ndani ya saa 4 baada ya dozi ya kwanza.

Magneziamu salfeti huja katika viwango tofauti vya ukolezaji (idadi ya miligramu za dawa katika kila mililita ya kimiminika(mchanganyiko wa majimaji). Hivyo, chunguza karatasi ya maelezo juu ya dawa kwa makini na uwe na uhakika wa kuchanganya katika kiasi sahihi cha maji yaliyotakaswa kabla ya kutumia.

Jinsi ya kutumiaNBgrninject.png

Choma gramu 10 zenye dawa machanganyiko wa majimaji wa 50% kwenye makalio. Kwa sababu sindano kubwa huumiza, gawanya dawa kwenye sindano 2 gramu 5 kila moja na zichomwe kwenye msuli wa kalio tofauti.

Kama baada ya saa 4 hujapata msaada, unaweza kutoa sindano 1 zaidi ya gramu 5 kwenye kalio moja.

Diazipamu


Diazipamu inaweza kutumika kulegeza msuli na kupunguza maumivu. Inaweza kutumika pia kuzuia shambulio moja. Kwa watu wenye mashambulio yanayojirudia (kifafa), tumia dawa tofauti, dawa ambayo inaweza kutumika kila siku.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Hali ya kusinzia kila mara.

MuhimuNBgrnimportant.png
  • Diazipamu ikizidi kiwango inaweza kusababisha upumuaji kusimama kabisa. Usitoe zaidi ya dozi iliyoelekezwa 2 na usitoe zaidi ya dozi 2.
  • Diazipamu ina tabia ya kumtawala mtumiaji – kila mara hujisikia kutaka kuitumia. Epuka matumizi ya muda mrefu au ya mara kwa kwa mara.
  • Usitoe kwa mjamzito au mama ambaye ananyonyesha isipokuwa tu kama anapata mashambulio (kwa mfano kutokana na kifafa cha mimba).
  • Usichome sindano ya Diazipamu isipokuwa kama una uzoefu au umepata mafunzo ya kufanya hivyo. Ni vigumu sana kutoa dawa hiyo kwa njia ya sindano. Badala yake, wakati wa shambulio, unaweza kuiweka kwenye njia ya haja kubwa.


Jinsi ya kutumiaNBgrninject.png

Kwa matumizi wakati wa ujauzito
Tumia ile yenye mfumo wa majimaji kwa ajili ya sindano au saga vidonge na kuchanganya kwenye maji kidogo. Toa sindano kutoka kwenye bomba lake, halafu fyonza dawa. Au tumia diazipamu ya aina teketeke au jeli kwa ajili ya matumizi kwenye njia ya haja kubwa.

Mlaze upande mmoja halafu tumia bomba lisilokuwa na sindano kuingiza dawa ndani kabisa ya njia yake ya haja kubwa. Makalio yake yashikiliwe pamoja kwa dakika10 ili dawa ibaki ndani.

Kwa ajili ya shambulio
Toa miligramu 20 za diazipamu kwenye njia ya haja kubwa. Kama mashambulio yataendelea dakika 30 baada ya dozi ya kwanza, unaweza kumpa miligramu zingine 10, lakini usimpe zaidi ya hapo.