Hesperian Health Guides

Sehemu ya tatu: Matatizo ya kiafya kutokana na maji yasiyo salama

HealthWiki > Mwongozo wa jamii juu ya afya ya mazingira > Sehemu ya tatu: Matatizo ya kiafya kutokana na maji yasiyo salama

Katika sura hii:

Waste from a hotel, latrine, livestock and people contaminates a stream through a village.
Baada ya kusoma sehemu ya tatu, utakuwa umejifunza:
  1. Njia kuu za uchafuzi wa maji
  2. Magonjwa yanavyoambukizwa kuhusiana na maji
  3. Jinsi ya kuzuia uchafuzi wa maji na kudhibiti maambukizi ya magonjwa


Hakuna anayeweza kuishi bila maji. Ili kuwa na afya njema, watu wanahitaji maji ya kutosha na salama.Maji yanakuwa siyo salama pale vijidudu vya magojwa na minyoo kutokana na kinyesi cha binadamu na wanyama (kinyesi na mkojo) vinapoingia kwenye maji hayo. Vijidudu vya magonjwa na minyoo vinaweza kuambukiza kupitia kwenye maji au kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, na kusababisha matatizo mengi ya kiafya ambayo yanaweza kuiathiri jamii nzima.

Vile vile, kemikali zenye sumu zinazotumika mashambani, viwanda, katika uchimbaji madini, na kutokana na utupaji taka hovyo zinaweza pia kuchafua maji yetu na kusababisha magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya ngozi, saratani na matatizo mengine makubwa ya kiafya.

Uhaba wa maji ya kunywa, kupikia na kuoshea pia unaweza kusababisha magonjwa. Hasa kama hakuna namna ya kunawa mikono baada ya kujisaidia chooni, magonjwa ya kuhara husambaa haraka kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Uhaba wa maji kwa ajili ya kufanya usafi binafsi unaweza pia kusababisha uambukizo kwenye macho na ngozi. Ukosefu wa maji unaweza pia kusababisha mwili kupungukiwa maji na hatimaye kifo.

Kawaida uhaba wa maji katika jamii unaweza kusababishwa na hali ya ukame wa muda mrefu, gharama kubwa ya maji au vyanzo vya maji kutotunzwa vizuri. Wakati uchafuzi wa maji husababisha hali ya uhaba wa maji kuwa mbaya zaidi, vile vile uhaba huo huchangia uchafuzi wa maji kukithiri. Soma sehemu ya pili ya moduli hii.



Ukurasa huu ulihuishwa: 05 Jan 2024