Hesperian Health Guides
Kwa ajili ya matibabu ya kuvu au ukungu
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Sura ya 27: Watoto wachanga na unyonyeshaji > Kwa ajili ya matibabu ya kuvu au ukungu: Watoto wachanga na unyonyeshaji
Watoto Wachanga na Unyonyeshaji: Dawa
Jentiani ya zambarau, au GV, au methrosaniliamu kloraidi
Jentiani ya zambarau au kwa umaarufu wake GV (Gentian violet) ni dawa isiyo ghali kwa ajili ya matibabu ya maambukizi ya fangasi mdomoni, kwenye chuchu za mama ambaye ananyonyesha , ndani ya mikunjo ya ngozi, au kwenye mlango wa uke au ndani ya uke. Dawa hiyo pia hutumika kupambana na maambukizi yanayosababishwa na bakteria kwenye ngozi.

Dawa ya Jentiani ya zambarau au GV inaweza kuathiri ngozi na kusababisha vidonda inapotumika mdomoni au ukeni. Simamisha matumizi kama upele au vidonda vitatokea.

Jentiani ya zambarau au GV hugeuza kila kitu kuwa cha zambarau. Hupungua baada ya siku chache lakini inaweza kutia nguo madoa ya kudumu.

Iwapo maambukizi hayataanza kupona ndani ya siku chache, jaribu dawa nyingine.
Nistatini (Nystatin)
Nistatini hufanya kazi vizuri kama tiba ya maambukizi mengi ya aina ya fangasi mdomoni, kwenye chuchu au ngozi au ukeni. Dawa hiyo inakuwa katika mfumo wa majimaji kwa matumizi ya mdomoni, mafuta , poda au unga, au bomba maalum kwa ajili ya kuingiza ukeni.

Ngozi inaweza kuanza kuwasha mahali nistatini inapotumika. Jambo hili hujitokeza mara kwa mara. Simamisha matumizi kama utapata upele. Dawa ya nistatini wakati mwingine pia husababisha kuharisha.

Maambukizi ya aina ya fangasi ambayo hayapungui baada ya kutumia nistatini, au ambayo hutoweka na kurudi tena, huenda yakawa dalili ya VVU.

Kwa mtoto mchanga mwenye ukungu/kuvu mdomoni