Hesperian Health Guides

Dawa za kupunguza maumivu

Huduma ya kwanza: Madawa

Dawa kwa ajili ya kupunguza maumivu ya kawaida na homa ni pamoja na parasetamo (dawa bora na salama sana kwa watoto), aspirini, na iburofeni. Aspirini na ibuprofeni pia hupunguza uvimbe uliotunga damu. Hivyo,kwa mfano, ukipata ajali na kifundo chako cha mguu kikijisokota, hazitasaidia tu kwa ajili ya kupunguza maumivu, lakini zitapunguza uvimbe pia. Hii husaidia kupona haraka. Lakini watu wenye homa na maambukizi ya virusi wanapaswa kuepuka asipirini.

Usitoe zaidi ya dozi ya dawa iliyopendekezwa. Dawa zote hizi zinaweza kuwa na madhara mabaya zinapozidishwa kiasi kinachohitajika. Kwa mfano, matumizi ya asipirini kupita kiasi kinachohitajika na ibuprofeni yanaweza kusababisha vidonda vya tumbo. Kiasi kikubwa cha parasetamo huzaa sumu. Kwa ajili ya homa kali au maumivu, chukua tahadhari kutozidisha dawa kwa kutumia parasetamo na ibuprofeni kwa kupokezana.

Parasetamo, asetaminofeni


Parasetamo ni dawa nzuri na yenye bei nafuu kwa ajili ya homa na maumivu ya kawaida.

MuhimuNBgrnimportant.png

Usitumie zaidi ya dozi iliyopendekezwa. Ikizidi husumunisha ini na inaweza kuua. Weka dawa hii mbali na watoto, hasa kama ni sirapu zenye ladha tamu.

Dawa nyingi baridi mara nyingi huwa na parasetamo ndani yake. Hivyo usitoe dawa hizi kama unatoa pia parasetamo au utakuwa unazidisha kiasi cha dawa.

Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png
Toa miligramu 10 hadi 15 kwa kilo, kila baada ya saa 4 hadi 6. Usitoe zaidi ya mara 5 ndani ya saa 24. Kama huwezi kumpima mtu, mpe dozi kuzingatia umri:

Chini ya mwaka 1: toa miligramu 62 (nusu ya ¼ ya kidonge cha miligramu 500), kila saa 4 hadi 6.
Mwaka 1 hadi 2: toa miligramu 125 (¼ kidonge cha miligramu 50), kila saa 4 hadi 6.
Miaka 3 hadi 7: mpe miligramu 250 (½ ya kidonge cha miligramu 500), kila saa 4 hadi 6.
Miaka 8 hadi 12: mpe miligramu 375 (¾ ya kidonge cha miligramu 500), kila saa 4 hadi 6.
Zaidi ya miaka 12: mpe miligramu 500 hadi 1000, kila saa 4 hadi 6, lakini usitoe zaidi ya miligramu 4000 kwa siku.

Ibuprofeni (ibuprofen)


Ibuprofeni hupunguza maumivu ya misuli, viungo, na kichwa, na homa.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Ibuprofeni inaweza kusababisha maumivu ya tumbo, lakini kuitumia pamoja na maziwa au chakula hupunguza tatizo hilo.

MuhimuNBgrnimportant.png

Usitumie ibuprofeni kama una mzio na asipirini. Baadhi ya watu ambao wana mzio na asipirini pia hupata mzio wanapotumia ibuprofeni. Usitoe ibuprofeni kwa ajili ya maumivu ya tumbo au ya kumeng’enya chakula tumboni. Ibuprofeni ina asidi na hili linaweza kuzidisha matatizo hayo. Kwa sababu hiyo hiyo, watu wenye vidonda vya tumbo kamwe wasitumie asipirini. Usitoe ibuprofeni kwa watoto wachanga chini ya miezi 6, na usitoe kwa wanawake wajawazito katika miezi yao 3 ya mwisho.

Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png
Mpe miligramu 5 hadi 10 kwa kilo. Kama huwezi kumpima mtu, toa dozi kwa kuzingatia umri.
Miezi 6 hadi mwaka 1: toa miligramu 50, kila saa 6 hadi 8.
Mwaka 1 hadi miaka 2: toa miligramu 75, kila saa 6 hadi 8.
Miaka 2 hadi 3: toa miligramu 100, kila saa 6 hadi 8.
Miaka 4 hadi 5: toa miligramu 150, kila saa 6 hadi 8.
Miaka 6 hadi 8: toa miligramu 200, kila saa 6 hadi 8.
Miaka 9 hadi 10: toa miligramu 250, kila saa 6 hadi 8.
Miaka 11: toa miligramu 300, kila saa 6 hadi 8.
Zaidi ya miaka 12: toa miligramu 200 hadi 400, kila saa 4 hadi 6.

Usitoe zaidi ya miligramu 40 kwa kilo, kwa siku moja. Usitoe zaidi ya dozi 4 kwa siku, na usitoe kwa zaidi ya siku 10 mfululizo.

Aspirini


Aspirini ni dawa nzuri na yenye gharama nafuu kwa ajili ya homa na maumivu ya kawaida.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Aspirini inaweza kusababisha maumivu ya tumbo au kiungulia. Ili kuepeuka hali hii, tumia asipirini pamoja na maziwa, kiasi kidogo cha magadi bikaboneti (bicarbonate of soda), au maji mengi-au pamoja na chakula.

MuhimuNBgrnimportant.png
  • Usitoe asipirini kwa ajili ya maumivu ya tumbo au tumbo kutomeng’enya vizuri chakula. Asipirini ina asidi ndani yake na inaweza kuzidisha tatizo. Kwa sababu hiyo hiyo, watu wenye vidonda vya tumbo kamwe wasitumie asipirini.
  • Usitoe zaidi ya dozi 1 ya asipirini kwa mtu ambaye amepungukiwa na maji mwilini hadi atakapoanza kukojoa vizuri.
  • Ni bora kutowapa asipirini watoto chini ya miaka 12, hasa watoto wachanga (parasetamo ni bora zaidi) au mtu mwenye pumu (hii inaweza kusababisha shambulio). Usiwape watoto wenye dalili za mafua, kwani hii inaweza kusababisha matatizo.
  • Weka asipirini mbali na watoto. Kutumia kiasi kikubwa husababisha sumu.
  • Usitoe kwa wanawake wajawazito.
Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png
Mwaka 1 hadi miaka 2: toa miligramu 75, kila saa 6.
Miaka 3 hadi 7: toa miligramu 150, kila saa 6.
Miaka 8 hadi 12: toa miligramu 300, kila saa 6.
Zaidi ya miaka 12: toa miligramu 300 hadi 600, kila saa 4 hadi 6.

Usitoe zaidi ya miligramu 2400 kwa siku moja. Usitoe kwa watoto zaidi ya mara 4 kwa siku.

Kwa ajili ya mshituko wa moyo
Toa miligramu 300 hadi 325 kwa njia ya mdomo. Tafuna na kumeza.

Kodeini (codeine/codeine sulfate)


Kodeini ni dawa ya kupunguza maumivu kutoka kundi la dawa kali zenye asili ya afyuni (opiate). Tumia tu kodeini pale dawa za kawaida za kupunguza maumivu zinaposhindwa kufanya kazi.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Inaweza kusababisha choo kigumu au kutopata choo na kushindwa kwa muda kukojoa. Inaweza pia kusababisha kichefuchefu, kutapika, mwasho, na maumivu.

MuhimuNBgrnimportant.png
  • Kodeini ni dawa yenye uwezo wa kujenga ‘kiu’ cha kuendelea kuitumia. Epuka matumizi ya muda mrefu au matumizi ya mara kwa mara.
  • Usinywe pombe wakati unatumia kodeini kwa vile inaweza kusababisha madhara hatari na hata kifo.
  • Kodeini inaweza kuathiri namna unavyofikiri na mwitiko wako kwa mambo mbalimbali wakati unaitumia. Chukua tahadhari unapokuwa unaendesha gari au kufanya mambo mengine ambayo yanahitaji uangalifu mkubwa.
  • Punguza dozi taratibu kadri utakavyokua unaendelea kuitumia ili hatimaye kuacha kuitumia kabisa. Kuacha mara moja kunaweza kusababisha kero za kukatisha matumizi.
  • Usitumie kodeini kama umewahi kupatwa na mzio kutokana na mofini.
  • Usitumie kodeini kama una mimba au unanyonyesha.
Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png
Toa kodeini pamoja na chakula.
Miaka 3 hadi 6: toa ½ miligramu hadi miligramu 1 kwa kilo kwa njia ya mdomo, kila saa 4 hadi 6.
Miaka 7 hadi 12: mpe miligramu 15 hadi 30 kwa njia ya mdomo, kila saa 4 hadi 6.
Zaidi ya miaka 12: mpe miligramu 15 hadi 60 kwa njia ya mdomo, kila saa 4 hadi 6. Usitoe zaidi ya miligramu 360 kwa siku.

Mofini (morphine), mofini salfeti (morphine sulfate) au mofini haidrokloraidi (morphine hydrochloride)


Mofini pia ni dawa ya kupunguza maumivu kutoka kundi la dawa yenye asili ya afyuni (opiate). Hutumika kwa ajili ya kutibu maumivu ya kawaida hadi maumivu makali.

MuhimuNBgrnimportant.png
  • Mofini pia hujenga tabia ya kutaka kuendelea kuitumia. Epuka matumizi ya muda mrefu au ya mara kwa mara.
  • Usitumie pombe unapokuwa unatumia mofini kwa sababu inaweza kusababisha madhara ya pembeni makali na hata kifo.
  • Mofini inaweza kuathiri uwezo wako wa kufikiri na utendaji wako unapokuwa unaitumia. Chukua tahadhari unapokuwa unaendesha gari au unapofanya mambo mengine ambayo yanahitaji uangalifu mkubwa.
  • Punguza dozi taratibu na hatimaye kuacha kutumia. Kusimamisha matumizi mara moja kunaweza kusababisha kero za kukatisha matumizi.
  • Usitumie mofini kama uliwahi kupatwa na mzio kutokana na kodeini.
  • Usitumie mofini kama ni mjamzito au unanyonyesha.
Jinsi ya kutumiaNBgrnpill-inject-drop.png

Kwa maumivu ya kawaida hadi maumivu makali

Chini ya miezi 6: mpe miligramu 0.1 kwa kilo kwa njia ya mdomo, kila saa 3 hadi 4. Kama huwezi kumpima mtoto, mpe miligramu 0.5 kwa njia ya mdomo, kila saa 3 au 4.
Zaidi ya miezi 6: mpe miligramu 0.2 hadi 0.5 kwa kilo kwa njia ya mdomo, kila saa 4 hadi 6 kadri inavyotakiwa.
Kama huwezi kumpima mtu, mpe dozi kwa kuzingatia umri:
Miezi 6 hadi mwaka 1: mpe miligramu 2 kwa njia ya mdomo, kila saa 4 hadi 6.
Mwaka 1 hadi miaka 5: mpe miligramu 3 kwa njia ya mdomo, kila saa 4 hadi 6.
Miaka 6 hadi 12: mpe miligramu 8 kwa njia ya mdomo, kila saa 4 hadi 6.
Zaidi ya miaka 12: mpe miligramu 10 hadi 30 kwa njia ya mdomo, kila saa 4 kadri itakavyohitajika.


Kwa ajili ya mshituko wa moyo
Choma miligramu 10 polepole kwa dakika 5 (miligramu 2 kwa dakika). Choma miligramu zingine 5 hadi 10 kadri itakavyohitajika.