Hesperian Health Guides

Wanaume na wanawake wana mahitaji tofauti

Katika sura hii:

Wanawake na wanaume wana mahitaji na taratibu tofauti katika matumizi ya choo. Ni rahisi kwa wanaume kujisaidia katika sehemu za wazi au kwenye vyoo vya umaa kuliko wanawake. Wanawake ndiyo wanaobeba majukumu makubwa ya familia kama vile kuangalia watoto, kuchota maji, kutafuta kuni, kupika na kufanya usafi. Hii huwapunguzia fursa ya kutumia vyoo ambavyo ni salama, safi, bora na vyenye faragha.

As women wait at a bus stop, a man urinates against a nearby wall.
Kawaida ni rahisi zaidi kwa wanaume kujisaidia kuliko wanawake.


Kupanga ujenzi wa vyoo ambavyo vinazingatia mahitaji ya wanawake

A woman and girl at a toilet shelter.

Kutowashirikisha wanawake katika maandalizi ya mipango ya vyoo huwaweka katika hatari kubwa ya matatizo ya kiafya, kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa mahitaji yao kutozingatiwa. Wanaume wanapaswa pia kukumbuka mahitaji ya wanawake pale mabadiliko yanapofanyika katika huduma ya vyoo katika jamii ili mabadiliko hayo yawe na manufaa ya kiafya kwa kila mtu.

Ili kurahisisha ushiriki wa wanawake katika maandalizi ya mipango ya vyoo kwa jamii bila kuwaongezea mzigo zaidi:

  • Andaa mikutano katika muda ambao utawawezesha wanawake kushiriki.
  • Hakikisha wanawake wamealikwa na wanajisikia huru kutoa maoni yao.
  • Andaa mikutano maalum kwa ajili ya wanawake pekee iwapo hii itawawezesha kuwa huru zaidi.
  • Kila mtu achangie katika kufanya maamuzi.


If you teach a man, you teach one person. If you teach a woman, you teach a whole nation - African proverb.

Kawaida wanawake huwafundisha na kuwalea watoto. Pale ambapo mahitaji ya wanawake hayakutimizwa, mahitaji ya watoto pia yanaweza kutotimizwa. Hivyo, wanawake wasiposhirikishwa katika maandalizi ya mipango ya vyoo nyumbani na katika jamii, jamii nzima huathirika.


Kuondoa vizuizi kwa wanawake kunufaika na huduma ya vyoo bora

Lengo la zoezi hili ni kuwezesha kikundi kuamua mababiliko ambayo yanaweza kuwa yanahitajika ili kuboresha afya kwa kila mtu.

Zoezi hili husaidia watu kujadili maswala mbalimbali ambayo yanaweza kuwazuia wanawake kutumia vyoo bora na salama. Baada ya zoezi hili kufanywa na wanawake pekee, zoezi linaweza kufanywa tena na wanawake na wanaume kwa pamoja. Muda: saa 1.00 hadi 1.30. Vifaa: Karatasi kubwa za kuchorea, kalamu na gundi ya karatasi.

  1. Andika kauli kadhaa juu ya vyoo kwenye karatasi kubwa. Halafu soma kila kauli kwa wanakikundi, na kuuliza kila mtu iwapo anakubaliana na kauli hiyo au la. (Waambie wanakikundi kunyosha juu mkono iwapo wanakubali au kutonyoosha iwapo hawakubali). Kwa kila jibu la ndiyo, weka alama pembeni ya kauli hiyo. Zifuatazo ni baadhi ya kauli ambazo zinaweza kutumika:

  2. illustration of the below; 5 women sit and discuss by wall with a large piece of paper reading: "Too far from my house. Safer to go in the bush. No way to wash after. The toilet is dirty and I am the person who must clean it. I do not want to be seen entering or leaving the toilet. Pregnant women are not permitted to use toilets. During monthly bleeding we are not permitted to use the toilets. The toilets are not safe for children."
    Wakati wa siku za hedhi haturuhusiwi kutumia vyoo.
    Vyoo vyetu siyo salama kwa watoto
  3. Hesabu alama pembeni ya kila kauli. Chagua matatizo ambayo yalitajwa sana na anzisha mjadala juu ya masuala hayo. Nini chanzo cha tatizo hilo? Ugonjwa gani unaweza kutokana na tatizo hilo? Nini kinaweza kufanyika kuboresha hali hiyo? Kuna vikwazo gani katika kuboresha hali hiyo?
  4. Hitimisha kwa kuwezesha kikundi kuamua hatua kadhaa ambazo zinaweza kuchukuliwa na wanawake pamoja na wanaume kuhakikisha kwamba mahitaji ya kila mtu yanatimizwa.

Kufanya vyoo viwe rahisi kutumika

A person holding onto a hand support made of sticks squats to defecate over a pot.

TKuna njia nyingi za kufanya vyoo viwe rahisi kutumika kwa watoto, watu wazima, na wenye ulemavu. Vyoo vinatakiwa kurekebishwa kutegemea na hali zao. Hivyo ni muhimu kuhusisha makundi hayo katika kupanga huduma ya vyoo. Ubunifu unahitajika ili kutafuta njia zinazokidhi mahitaji ya kila mtu.

A toilet chair.
Chuma kinachowekwa na kutolewa kinaweza kuwekwa iwapo kitahitajika.

Kama mtu ana matatizo ya kuchuchumaa, basi itengenezwe sehemu ya kushika kwa mkono, au kiti kilichoinuliwa ili aweze kukaa.

Au, iwapo choo kimefungwa sakafuni, tengeneza tundu kwenye kalio la kiti au meza ndogo (stuli) na kuiweka juu ya choo.

Iwapo mtu atakuwa na matatizo ya kudhibiti mwili wake, tengeneza sehemu ya kuegemeza mgongo wake, mbavu na miguu na mkanda wa kiti au chuma cha kuzuia asianguke.

Tumia kamba au jenga uwa au ukingo kuongoza watu wenye upofu kutoka kwenye nyumba hadi chooni.

Kama mtu ana matatizo ya kuvaa nguo, rekebisha nguo zake ziwe pana au mtafutie nguo zenye asili ya kuvutika. Tengeneza sehemu safi na kavu kwa ajili ya kulala chini na kuvaa. Kama mtu ana matatizo ya kukaa, anaweza kutengenezewa papi za ngazi za kujishikizia.

Kumbuka mtu mwenye ulemavu ana mahitaji sawa ya huduma ya choo, pamoja na faragha, kama watu wengine.

Choo kilichorekebishwa kwa ajili ya kiti cha magurudumu

illustration of the below:A woman in a wheelchair uses a toilet shelter.
nafasi ya kutosha kuruhusu kiti cha magurudumu kuingia ndani
kengele au chochote kile kutoa sauti iwapo msaada unahitajika
sehemu ya kuegemeza mgongo wakati mtu amekaa
papi za ngazi kurahisisha kutoka kwenye kiti kwenda kwenye choo
sehemu ya kukalia kwenye choo na kiti cha magurudumu kwenye usawa
mlango mpana ambao hufunguka kwa nje kurahisisha kuingia
kitasa cha mlango kikiwa na kamba ya kuvuta
njia ya kwenda chooni ni tambarare na rahisi kwa ajili kwenda na kutoka ndani ya nyumba
Kumbuka, mtu mwenye ulemavu anahitaji faragha kama mtu mwingine yoyote na anapaswa kupata faragha anayohitaji..
A curtain with a sign reading "In Use."


Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Juni 2022