Hesperian Health Guides

Sehemu ya nne: Kutumia sheria kupigania haki za kimazingira

HealthWiki > Mwongozo wa jamii juu ya afya ya mazingira > Sehemu ya nne: Kutumia sheria kupigania haki za kimazingira

Katika sura hii:

A group of people circle around a book of laws.

Haki za binadamu, na wakati mwingine haki za kimazingira (haki ya kuwa katika mazingira salama na yenye afya), hulindwa na sheria za nchi nyingi.

Jamii ambazo zinapigania kulinda mazingira yao na afya zao kawaida hukumbana na upinzani, na hata matumizi ya nguvu kutoka makampuni au serikali ambazo zinataka kuchukua maliasili zao, au kuanzisha miradi ya maendeleo bila kuzingatia madhara ambayo yanaweza kutokea. Miradi hii inaweza kulazimisha watu kuhamishwa kutoka kwenye maeneo yao, kusababisha uchafuzi wa mazingira, kuhatarisha usalama wa jamii, au kuzalisha sumu ambazo zinaweza kuleta madhara ya kiafya. Mambo hayo yote ni ukiukwaji wa haki za binadamu na haki za kimazingira.

Wakati mwingine, makampuni na mashirika makubwa yana fedha na nguvu nyingi kiasi cha kuweza kuizuia serikali kutambua au kutekeleza sheria ambazo zimewekwa kulinda watu. Iwapo sheria za eneo fulani au taifa siyo imara, kuna sheria za kimataifa ambazo zinaweza kutumika kulinda jamii.

Baada ya kusoma sehemu ya nne, utakuwa umejifunza:
  1. Maana ya tathmini ya athari kwa mazingira na faida zake.
  2. Namna ya kufungua kesi mahakamani kutetea haki za kimazingira.



Ukurasa huu ulihuishwa: 05 Jan 2024