Hesperian Health Guides

Jinsi ya kuangamiza kwa usalama taka zisizohitajika

Katika sura hii:

Chochote kile ambacho hakiweza kutumiwa tena, kurejeshewa thamani au kutumika kutengeneza mboji inabidi kiondolewe au kuangamizwa kwa usalama. Kwa baadhi ya watu, kuchoma taka ndiyo njia bora zaidi. Wengine huamua kuchimba shimo na kuzifukia ili kuepuka moshi kutokana na uchomaji taka. Ukweli ni kwamba njia zote hizi mbili zina matatizo.

Mahali ambapo karatasi nyepesi na karatasi ngumu haziwezi kutumika tena, kurejeshewa thamani au kutengeneza mboji, zinaweza kukatwakatwa vipande na kutumika kuwashia jiko, au kuchomwa wakati wa kupika kama chanzo cha nishati. Lakini uchomaji, hata kiasi kidogo, wa plastiki au mpira huachia kemikali zenye sumu ikiwemo dioksini, furans na PCB ambazo husababisha matatizo mengi ya kiafya.

3 people talk as they toss trash into a fire.
Huwa nachoma taka zangu ili kuweka nyumba yangu safi na kuzuia panya.
Lakini moshi wa taka za plastiki ni hatari zaidi hata kuliko panya
Panya au moshi vyote ni hatari. Ni bora tusingezalisha uchafu mwingi kiasi hiki.

Taka ambazo haziwezi kushughulikiwa kwa njia yoyote ile zinaweza kufukiwa katika mashimo madogo au kupelekwa kwenye shimo maalum la kuhifadhi taka kwa usalama (sanitary landfill). Kama ni kuzifukia kwenye mashimo madogo ya kawaida, cha kufanya ni:

  • chimba shimo mbali na vyanzo vya maji,
  • weka taka kwenye shimo hilo, na
  • fukia na udongo.


Pale taka zenye kemikali ya sumu zinapofukiwa aridhini, kemikali hizi zinaweza kuvuja ardhini na kuchafua maji ya kunywa. Kama hakuna njia salama ya kuondoa taka zenye kemikali ya sumu (kwa mfano kuzirudisha kwa mtengenezaji au kuzitibu hadi zitakapokuwa salama), angalau zipelekwe kwenye shimo maalum la kuhifadhi taka kwa usalama lenye tabaka la kinga sakafuni na kutani kwa ajili ya kuzuia mvujo wa sumu kuingia kwenye vyanzo vya maji.


Ukurasa huu ulihuishwa: 04 Juni 2022