Hesperian Health Guides

Fuatilia hali ya mtoto mara kwa mara katika miezi yake 2 ya mwanzo

NWTND Newb Page 11-2.png


Mkunga au mfanyakazi mwingine wa afya aendelee kutoa uangalizi wa karibu kwa mama na mtoto baada ya kuzaliwa. Akina mama na watoto wao wanaweza kwenda kliniki kwa ajili ya uchunguzi wa maendeleo yao. Lakini pale inapowezekana, upimaji wa mara ya kwanza ufanyike nyumbani ili kuepuka usumbufu wa kusafiri na hatari ya maambukizi kutoka kwa wagonjwa wengine katika sehemu ya kutolea huduma. Mchunguze mtoto na mama yake siku inayofuata baada ya kuzaliwa, siku 3 baada ya kuzaliwa, na wiki 1 baada ya kuzaliwa. Ziara nyingine ya kumpatia huduma ya uchunguzi anapofikisha wiki 6 husaidia pia. Mtembelee mara nyingi zaidi na kuwa karibu zaidi kama kuna dalili zozote za matatizo. Kumtembelea mtoto na mama yake ndiyo njia bora zaidi ya kugundua matatizo ya kiafya kabla hali haijawa mbaya zaidi.