Hesperian Health Guides

Sura ya 7: Kulinda afya ya wanawake kwa kutumia uzazi wa mpango

HealthWiki > Juhudi za Afya kwa Wanawake > Sura ya 7: Kulinda afya ya wanawake kwa kutumia uzazi wa mpango

Katika sura hii:


3 families with different numbers of children.
Upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango ni sehemu muhimu ya juhudi za kuboresha afya ya wanawake, na ni sehemu ya haki zao za kiafya. Wanawake wanakuwa na afya bora zaidi wanapokuwa na uwezo wa kujiamulia juu ya suala la ngono na iwapo wanataka kupata watoto na lini. Uzazi wa mpango na njia za kudhibiti uzazi au kuzuia mimba huwawezesha wanawake kufanya maamuzi hayo.

Huduma za uzazi wa mpango siyo jambo jipya. Wanawake kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia njia ya kutofanya tendo la ngono na kuendelea kunyonyesha ili kuzuia kupata mimba. Baadhi ya wanawake hutumia ufahamu wao wa mizunguko yao ya hedhi na tarehe za uwezekano mkubwa wa kupata mimba katika kuepuka kupata mimba au kuwasaidia kupata mimba. Siku hizi, kuna njia nyingi za kuzuia kupata mimba. Njia hizi ni pamoja na kodom za kike au kiume, njia za homoni, kama vile vidonge vya majira, sindano za majira na vijiti. Njia zingine ni kuingiza vizuia mimba (IUDs -intrauterine devices) kwenye kizazi cha mwanamke; na hata kufunga uzazi kabisa. Matumizi ya njia yoyote kati ya hizi husaidia kupanga uzazi au kuzuia mimba.