Hesperian Health Guides

Mfumo wa uzazi wa mwanamke

Katika sura hii:

Mwanamke ana viungo vinavyohusika na ngono au mapenzi nje na ndani ya mwili wake. Huitwa viungo vya uzazi. Sehemu ya nje huitwa mlango wa uke. Wakati mwingine watu hutumia neno uke kumaanisha sehemu yote. Lakini uke ni sehemu inayoanza kama mlango na kuelekea ndani kwenye tumbo la uzazi. Wakati mwingine uke hujulikana kama mfereji wa uzazi.

mwanamke akiwa uchi, amekaa akiwa ametenganisha miguu yake
Mchoro ufuatao unaonesha jinsi mlango wa uke unavyoonekana na namna sehemu tofauti zinavyojulikana. Lakini kila mwili wa mwanamke ni tofauti. Kuna tofauti katika ukubwa, sura, na rangi ya viungo, hasa mikunjo ya nje na ndani.

Matiti

Matiti yameumbika kwa umbo na ukubwa tofauti. Matiti huanza kuota binti anapofikisha umri kati ya miaka 10 na 15, anapobadilika kutoka usichana kuwa mwanamke kwa kuanza kupata hedhi. Matiti hutengeneza na kutoa maziwa kwa ajili ya mtoto baada ya kujifungua. Yakitomaswa kimapenzi, mwili wa mwanamke husisimka na uke hutoa ute au majimaji tayari kwa ajili ya tendo la ngono.

mwili wa mwanamke, ukionesha sehemu vilipo viungo vya uzazi ndani ya mwili
Ndani ya titi:
Kielelezo cha sehemu za titi
Tezi hutengeneza maziwa.
Mirija hupitisha maziwa kwenda kwenye chuchu.
Mifuko yakuhifadhi maziwa hadi mtoto atakapoyanyonya.
Chuchu hutoa maziwa nje. Wakati mwingine umbo la chuchu huchomoza kwa nje na nyingine ni bapa.
Ngozi nyeusi yenye vituta vidogo vidogo kuzunguka chuchu. Vituta vidogo vidogo hivyo hutengeneza mafuta ambayo husaidia kutunza chuchu ikiwa laini na katika hali ya usafi.



Ukurasa huu ulihuishwa: 05 Jan 2024