Hesperian Health Guides

Mabadiliko katika mwili wako (kubalehe)

Katika sura hii:

Wasichana wote hupitia mabadiliko kwenye miili yao lakini mabadiliko hayo hutofautiana kati ya msichana mmoja na mwingine. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi iwapo mwili wako haufanani kabisa na wa dada yako au rafiki yako.

Kukua. Badiliko kubwa la kwanza huenda likawa ni kukua kwa haraka na mwili kubadilika. Unaweza kurefuka kwa muda kuwazidi vijana wenzio wa umri wako. Kawaida utaacha kukua mwaka 1-3 baada ya kuanza hedhi.

Mabadiliko ya mwili. Pamoja na kukua haraka, mwili wako nao utaanza kubadilika. Kwenye mwili kuna kemikali za asili ziitwazo homoni ambazo huuwambia mwili wako ukue na pia kuchochea mabadiliko haya kufanyika.

Mabadiliko wakati wa balehe hayaji yote kwa wakati mmoja au kwa mpangilio unaofanana.

Ndani ya mwili wako. Kuna mabadiliko mengine ndani ya mwili wako ambayo huwezi kuyaona. Tumbo la uzazi (mji wa mimba), mirija ya mayai, ovari, na uke hukua na kubadili mkao wake.

Hisia utakazopata.Kadri unavyopitia mabadiliko haya utazidi kujielewa zaidi kuhusu mwili wako. Unaweza pia kuvutiwa kukaa zaidi na wavulana au marafiki zako. Kunaweza kutokea wakati ambapo hisia zako zinakuwa vigumu kuzitawala. Siku chache kabla ya hedhi huweza kuwa kawaida kupata hisia kali za kila aina – kwa mfano; hisia ya furaha, hasira, na wasiwasi.

Hedhi ya kila mwezi

Hedhi ya kila mwezi ni dalili kwamba mwili wako unaweza kutunga mimba. Hakuna msichana anayeweza kujua kwa hakika ni lini atapata hedhi yake ya kwanza. Kawaida hutokea baada ya matiti na nywele kwenye sehemu za siri kuanza kuota. Miezi kadhaa kabla ya hedhi ya kwanza, msichana anaweza kugundua unyevunyevu ukimtoka ukeni. Unyevu huo unaweza pia kuchafua au kuweka madoa kwenye nguo zake za ndani. Hili ni jambo la kawaida.

Baadhi ya wasichana hupata furaha wanapopata hedhi yao ya kwanza, kama tayari wana ufahamu na kutarajia kilichotokea. Wasichana ambao hawakuambiwa mapema kuhusu hedhi hupatwa na hofu hedhi inapotokea. Ni jambo linalotokea kwa wanawake wote- unapaswa kulikubali na hata kujivunia. Usikubali mtu yeyote akufanye ufikiri kwamba ni jambo chafu au jambo la aibu.

Kujitunza wakati wa hedhi.

Kuwa msafi. Wasichana wengi hupendelea kutengeneza pedi kwa kutumia kitambaa kilichokunjwa vizuri au pamba ili kupokea na kufyonza damu kadri inavyotoka ukeni. Hizo pedi hushikizwa na mkanda, pini au chupi. Pedi zinapaswa kubadilishwa mara kadhaa kwa siku na kufuliwa vizuri kwa maji na sabuni iwapo zitatumika tena.

pedi kwa ajili ya kupokea damu wakati wa hedhi
pedi
kisodo chenye kamba ya kuning’inia
kisodo

Baadhi ya wanawake huingiza ukeni pedi maalum ya kununua, au ambayo hutengeneza kwa pamba, kitambaa laini au sponji ili kufyonza damu ukeni. Kama utatumia kifaa cha namna hii, hakikisha kinabadilishwa angalau mara 3 kwa siku. Kukiacha ndani ya uke kwa muda mrefu bila kubadilishwa huweza kusababisha maambukizi hatari.

Jisafishe vizuri sehemu zote za uke ili kuondoa mabaki yoyote ya damu. Unaweza kutumia sabuni isiyo kali sana.

Kuhusu kazi. Unaweza kuendelea na kazi zako za kawaida.

wanawake 2 vijana wakinawa kwa kutumia maji kutoka kwenye benseni na sabuni

Ni muhimu kuoga unapokuwa katika siku zako za hedhi
wasichana 3 wakicheza mpira wa kurusha, moja ameketi kwenye kigari cha magurudumu matatu
Mazoezi yanaweza kupunguza maumivu ambayo huwapata wasichana wakati wa hedhi
Ukurasa huu ulihuishwa: 05 Feb 2018