Hesperian Health Guides

Jinsi mwili wa mwanamke unavyobadilika

Katika sura hii:

michoro kwenye mduara inaonesha msichana akibadilika kuwa mwanamke, mama, na mwanamke mwenye umri zaidi
Mduara wa Maisha


Mwili wa mwanamke hupitia mabadiliko mengi muhimu katika kipindi cha uhai wake – wakati wa kupevuka,wakati wa balehe, wakati wa ujauzito na unyonyeshaji, na wakati hedhi inapokomaa-umri wa kutoweza kuzaa tena.

Zaidi ya hayo, wakati wa umri wa kuzaa, mwili wake hubadilika kila mwezi – kabla, wakati na baada ya hedhi ya kila mwezi. hedhi yake ya kila mwezi. Sehemu za mwili ambapo mabadiliko haya hutokea ni ukeni, mji wa mimba(kizazi), ovari, mirija ya mayai ya uzazi, kwenye matiti-sehemu zote hizo huitwa mfumo wa uzazi. Mabadiliko haya mengi husababishwa na kemikali za asili maalum ziitwazo homoni.

Ukurasa huu ulihuishwa: 05 Feb 2018