Hesperian Health Guides

Watoto wachanga na unyonyeshaji

HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Watoto wachanga na unyonyeshaji

Katika sura hii:

Huduma mara baada ya kuzaliwa

Ndani ya saa 1 baada ya kuzaliwa, unaweza kumsaidia mtoto kuishi na pia afya yake ya baadaye ya muda mrefu:

  1. Hakikisha mtoto anapumua vizuri.
  2. Mweke penye joto la kutosha na pakavu akiwa amegusana moja kwa moja na ngozi ya mama yake.
  3. Msaidie aanze unyonyeshaji.

Je, mtoto anapumua vizuri?

Mtoto anapokuwa anazaliwa, na unapokuwa unamkausha na kumweka kwenye ziwa la mama yake, angalia kama anapumua vizuri. Ukichukuwa hatua haraka, unaweza kunusuru maisha ya mtoto ambaye hapumui vizuri.

NWTND Newb Page 1-1.png
Miguu na mikono ina nguvu
Rangi yake ni nzuri

Anapumua vizuri, au analia
NWTND Newb Page 1-2.png
Mlegevu na hana nguvu
Rangi yake ni wekundu mzito sana au zambarau, au anageuka kuwa bluu, bluu hafifu au kijivu

Anapumua kwa shida, au hakuna dalili za kupumua au kulia
Mtoto huyu anaonekana mwenye afya. Mtoto huyu anahitaji msaada wa haraka.


Iwapo mtoto amelegea, rangi yake inaelekea kwenye bluu, au hapumui

Usimpigepige.

  1. Ondoa kamasi kutoka kwenye mdomo wa mtoto kwa kuyafuta taratibu ukitumia kidole chako kilichozungushwa na kitambaa kisafi. Au tumia bomba la sindano maalum au kifaa cha kuvuta kamasi.
  2. illustration of the above: kuondoa kamasi kwa kidole.
    mtoto akiwa amelala kifuani mwa mamake miili yao ikigusana
  3. Sugua kwa nguvu kiasi mgongo wa mtoto-ukianzia juu kwenda chini. Tumia taulo au kitambaa kisafi kumtia joto na kumkausha kwa wakati mmoja. Pangusa pia sehemu za chini za unyayo wake. Hayo yatamsisimua vya kutosha na kumsaidia kuchukua pumzi nzuri yenye nguvu.

    Iwapo mtoto bado hapumui, au anaacha kupumua, unalazimika kumpatia pumzi ya dharura ya kumnusuru.

Pumzi ya kunusuru

  1. Mlaze mtoto sehemu ngumu: mezani au sakafuni. Weka kitambaa chini yake na kumfunika sehemu ya mwili wake ili aweze kupata joto.
  2. Inua kidogo kidevu cha mtoto, ili kiwe kimeinuka kidogo kuangalia juu kwenye dari. Unaweza kukunja kitambaa kidogo na kukiweka chini ya mabega yake. Hi hulifanya koo lake kubaki wazi kwa ajili ya kupumua.
  3. Kidevu cha mtoto kikiwa kimeinuliwa juu
    baby with chin touching her chest.
    Mtoto anapaswa kuwezeshwa kuangalia juu kama ilivyoelekezwa pichani. Siyo hivi.
  4. Fungua mdomo wako wazi. Kwa kutumia mdomo wako funika mdomo na pua ya mtoto.
  5. Mchoro wa mtoto ukionyesha sehemu ya kufunika na mdomo wako na kifaa maalum kwa ajili ya kumsaidia mtoto kupumua.
    Sehemu ya kufunika na mdomo wako.
    Unaweza kutumia kifaa maluum chenye mfuko wa kifunika mdomo na pua badala ya mdomo wako.
  6. Puliza hewa ndani ya mdomo na pua ya mtoto. Puliza kidogo kidogo tu. Mpulizie kidogo mara 1 lakini kwa haraka kila baada ya sekunde moja au 2. Kuwa mwangalifu kutopuliza sana kupita kiasi, kwani unaweza kuharibu mapafu laini ya kichanga hicho.

    Mara kila unapompumlia, subiri kidogo ili mtoto naye aweze kurudisha pumzi nje.
    a woman counting to herself between breaths.
    Moja na...
    a woman thinking while she puffs air into the baby.
    Pumua.

    Iwapo hewa inaonekana kutomuingia mtoto, simamisha. Inua kidevu cha mtoto ukihakikisha kinaangalia juu na koo lake liko wazi. Halafu jaribu tena.

    Iwapo mtoto ataanza kulia, au atapumua angalau mara 30 kila dakika kwa nguvu zake mwenyewe, ni salama angalau kwa sasa. Mweke kifuani mwa mamake, na hakikisha anapata joto la kutosha. Huenda akajisikia vizuri. Lakini kuwa mwangalifu sana saa chache zijazo. Je mtoto ana rangi nzuri? Anapumua kwa urahisi? Kama mtoto atabadilika na kuwa rangi ya bluu kwenye mwili au mdomo, au ataanza kupumua kwa shida, tafuta msaada.

    Iwapo baada ya dakika 20 za kumsaidia kupumua mtoto hajaanza kupumua peke yake, huenda akapoteza maisha. Kaa karibu na familia katika kipindi hiki chenye majonzi. Watahitaji uangalizi na huduma yako.

Hakikisha mtoto anapata joto kutoka kwenye mwili wa mamake



mtoto amefunikwa na blanketi akiwa kifuani mwa mamake.
Mweke mtoto kwenye mwili wa mamake
Funika kichwa cha mtoto na kofia au blanketi.

Nafasi bora zaidi kwa mtoto ambaye amezaliwa ni kwenye mwili wa mamake.


Mtoto ambaye amezaliwa punde anapaswa kuwekwa katika hali ya vuguvugu na yenye ukavu. Joto kutoka kwenye mwili wa mamake litasaidia kumpa joto analolihitaji. Usimtenganishe mtoto na mamake kumchunguza au kumuogesha. Mtoto ambaye ndiyo amezaliwa hahitaji kuogeshwa mara anapozaliwa-na kumuogesha kunaweza kusababisha mtoto kuingiwa na baridi hatari. Hakuna sababu ya kumtenganisha mama na mtoto-isipokuwa pale ambapo unahitaji kumpatia pumzi ya dharura.

  • Mkaushe mtoto unapokuwa unamweka kwenye mwili wa mamake.
  • Mpatie joto la kutosha kwa kumweka uchi kwenye kifua wazi cha mamake. Halafu wafunike wote wawili na blanketi au shuka. Haraka badili blanketi zote zilizolowa na kuweka zilizo kavu kwa sababu nguo zenye unyevu zitamzidishia mtoto baridi.


Iwapo mama anapaswa kupelekwa hospitalini, au hawezi kumbeba mtoto wake mara moja, baba yake au mwanafamilia mwingine anaweza kumpakata mtoto, akimshikilia kwenye mwili wake.

mwanamke akiwa amemweka mtoto wake kifuani chini ya gauni lake

Anza kunyonyesha

Watoto wachanga wana tabia ya kulala usingizi ndani ya saa 1 baada ya kuzaliwa. Mtoto anapaswa kunyonyeshwa kabla ya kulala. Hivyo, kama hatakuwa na hamu ya kunyonya mara moja, jaribu kukamulia matone ya maziwa ya kwanza ya mamake kwenye midomo yake ili kumshawishi kunyonya. Au tingisha shavu lake kidogo na chuchu ya mamake. Hakuna kitu kinachomhakikishia mtoto afya njema kama kunyonyeshwa. Kwa taarifa zaidi juu ya unyonyeshaji na umuhimu wa kumpa mtoto maziwa ya kwanza kutoka kwenye titi la mama yake baada ya kujifungua, bonyeza hapa.