Hesperian Health Guides

Saratani na ukosefu wa usawa katika upatikanaji huduma

HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Saratani na ukosefu wa usawa katika upatikanaji huduma

Katika sura hii:

Saratani ni tatizo gumu kwa kila mtu, lakini ni gumu zaidi kwa watu maskini. Watu wenye hali duni au ambao hawapati huduma za msingi wako katika hatari kubwa ya kupatwa na saratani, kwani huishi mahali ambapo uchafuzi wa mazingira umekithiri. Hufanya kazi hatarishi, na hukabiliwa na msongo zaidi. Kula mchanganyiko wa vyakula vizuri (matunda na mbogamboga kutoka shambani, protini, na nafaka ambazo hazijasindikwa) vinaweza kusaidia kuzuia saratani, lakini baadhi ya watu hawawezi kumudu kula vizuri. Na watu wenye hali duni kawaida hawawezi kumudu gharama za uchunguzi wa afya, dawa, na huduma za afya zenye uwezo wa kubainisha na kutibu saratani zao.

Kwa sababu zote hizi, tunaweza kusema umasikini na ukosefu wa usawa katika upatikanaji huduma huchangia tatizo la saratani.