Hesperian Health Guides

Ndani ya saa chache zinazofuata

Katika sura hii:

Saa 1 au 2 baada ya mtoto kuzaliwa, akiwa amekwisha kunyonyeshwa na umehakikisha kuwa mama havuji damu na yu salama, toa dawa zozote zile zinazohitajika na kumchunguza mtoto kwa uangalifu kuanzia kichwa hadi kidole kuona iwapo kuna tatizo lolote linalohitaji kushughulikiwa. Usimfanye mtoto kupigwa na baridi wakati wa kumchunguza.

Dawa kwa ajili ya watoto wachanga

Iwapo mama ana ugonjwa wa kisonono au klamidia (maambukizi mengine ya aina ya bakteria kwenye uke na ume), hali hii inaweza kusababisha maambukizi kwenye macho ya mtoto wakati wa kujifungua, na hata upofu. Ni jambo la kawaida kwa mwanamke kuwa na maambukizi ukeni bila kujijua. Njia bora zaidi ya kuhakikisha maambukizi ya kisonono na Klamidia hayaenezwi machoni kwa mtoto ni pande zote mbili-wanawake na wanaume kupima afya zao na kutibiwa maambukizi hayo ambayo huenezwa kupitia njia ya ngono. Kujifunza zaidi juu ya dalili za maambukizi hayo na tiba zake, rejea Matatizo na maambukizi ya ukeni na umeni (kinaandaliwa). Ili kuzuia maambukizi machoni kutokana na kisonono, weka matone kidogo ya dawa ya erithromaisini (erythromycin) au tetrasaikilini (tetracycline) katika kila jicho la mtoto ndani ya saa moja au mbili baada ya kuzaliwa.

Katika maeneo ambayo magonjwa ya homa ya ini (hepatitis B) au saratani ya ini hujitokeza sana, ni jambo la busara kumpa mtoto chanjo ya homa ya ini siku ya kwanza baada ya kuzaliwa.. Chanjo hii itasaidia kuzuia maambukizi ya homa ya ini kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Ni jambo la kawaida pia kwa mwanamke kuwa na maambukizi ya homa ya ini (hepatitis B) bila kujijua.



Katika maeneo ambayo magonjwa ya homa ya ini (hepatitis B) au saratani ya ini hujitokeza sana, ni jambo la busara kumpa mtoto chanjo ya homa ya ini siku ya kwanza baada ya kuzaliwa. Chanjo hii itasaidia kuzuia maambukizi ya homa ya ini kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Ni jambo la kawaida pia kwa mwanamke kuwa na maambukizi ya homa ya ini (hepatitis B) bila kujijua.

Mchunguze Mtoto

NWTND Newb Page 6-1.png
  • Je, mtoto anaonekana kama watoto wachanga wengine?
  • Je, viungo vyake vya mwili sehemu ya kushoto na sehemu ya kulia vinafanana kwa ukubwa, sura/muundo na mahali vilipo?
  • Ngozi yake nzima? Chunguza hasa sehemu ya chini mgongoni. Wakati mwingine huwa kuna tundu dogo ambalo huhitaji operesheni mara moja.
  • Uke au ume wake ni wa kawaida? (Kuvimba siku ya kwanza ni kawaida na siyo hatari.)
  • Je, amekojoa? Mtoto anaweza kutokojoa siku ya kwanza. Lakini ataweza kutoa mkojo mara kadhaa siku ya pili na kufanya hivyo kila baada ya saa kadhaa. Iwapo hatakojoa vya kutosha, au kama mkojo wake una rangi nzito na harufu kali, anahitaji kunyonyeshwa zaidi. Au anaweza kuwa na tatizo kwenye figo zake.
  • Je mtoto amejisaidia haja kubwa? Kama hapana, vaa mipira ya mikononi (glovu) na taratibu ingiza kile kidole chako kidogo kwenye njia yake ya haja kubwa kuhakikisha kuwa haijaziba au kufunga. Iwapo hakuna njia au tundu, anahitaji kufanyiwa operesheni.

Baadhi ya tofauti siyo muhimu, lakini zingine zinaweza kuwa dalili za tatizo kubwa. Iwapo mtoto ana tofauti moja, yawezekana akawa na tofauti zingine na wakati mwingine zinakuwa ndani ya mwili wake. Waangalie watoto wachanga kwa karibu kujua iwapo upumuaji wao, rangi yao na utoaji mkojo ni wa kawaida.

Umbo la Kichwa

kichwa cha mtoto kilichovimba

Ni kawaida kichwa cha mtoto kuwa na umbo lililochongeka au lenye uvimbe kama huu. Hasa baada ya kukaa muda mrefu katika uchungu wa uzazi. Baada ya siku chache, uvimbe hutoweka.

NWTND Newb Page 7-3.png
Uvimbe chini ya ngozi kichwani

Baadhi ya watoto huwa na mkusanyiko wa damu chini ya ngozi kichwani. Ukiubonyeza ni laini. Uvimbe kama huo siyo hatari lakini huweza kuchukua mwezi mmoja au zaidi kutoweka.

Ufa kwenye mdomo na ufa kwenye dari ndani ya mdomo

mtoto mwenye mdomo wenye ufa.

Ufa kwenye mdomo huonekana kwa urahisi. Lakini ufa kwenye dari ndani ya mdomo siyo rahisi kuonekana. Ingiza kidole kisafi ndani ya mdomo wa mtoto kuangalia iwapo dari yake imefunga. Hatari kwa mtoto mwenye ufa kwenye mdomo na ufa kwenye dari ndani ya mdomo ni kwamba unyonyeshaji huwa mgumu zaidi.

Katika kunyonyesha, jaribu kufunika ufa kwenye mdomo na kidole ili mdomo uweze kushika na kukaza vizuri ziwa. Katika hali ya ufa kwenye dari ndani ya mdomo, ingiza chuchu na eneo jeusi linaloizunguka ndani sana ya mdomo wa mtoto na kwenye upande mmoja wa ufa. Kama mtoto bado anapata tabu, mpe maziwa ya mama yaliokamuliwa kwa kutumia kijiko kisafi hadi atakapokuwa na uwezo zaidi wa kunyonya. Mnyweshe kila baada ya muda mfupi ili aweze kuendelea vizuri. Kujifunza zaidi jinsi ya kukamua maziwa ya mama kwa ajili ya kumlisha mtoto kwa kijiko, bonyeza hapa.

Mdomo wenye ufa unaweza kurekebishwa kwa njia ya operesheni baada ya miezi 3. Ufa kwenye dari ndari ya mdomo unaweza pia kurekebishwa kwa njia ya operesheni lakini baada ya mwaka 1. Katika nchi nyingi operesheni hizi hufanyika bila kutoza malipo na ni muhimu sana katika maisha ya mtoto. Ulizia kwenye kliniki au hospitalini kwa taarifa zaidi.

Nyonga iliyotenguka, nyonga ilioyochomoka, na ukuaji usio wa kawaida wa misuli, viungo, au chembechembe za mwilini (dysplasia)

Maelezo juu ya picha: kuchunguza nyonga iliyotenguka.

Baadhi ya watoto huzaliwa wakiwa wametenguka nyonga-mguu unakuwa umechomoka nje ya kiunganishi chake kwenye mfupa wa nyonga. Mara nyingi, hali hii hujirekebisha yenyewe baada ya siku au wiki chache.

Pinda miguu ya mtoto ili uweze kukamata paja na sehemu ya chini ya mguu kwa pamoja. Weka ncha ya vidole vyako kwenye nyonga ya mtoto. Halafu tembeza mguu mmoja mmoja kwa wakati polepole-nje, kuuzungusha, chini na urudishe juu. Kama mguu mmoja utasimama, kushtuka, au kutoa sauti kama vile umegongana na kitu, unapoufungua sana, unaweza kuwa umetenguka.

mwanamke akiwa amembeba mtoto wake mgongoni miguu yake ikiwa imetanuka.
Mwambie mama ambebe mtoto wake miguu yake ikiwa imetanuliwa kama ifuatavyo.

Mwangalie mtoto tena baada ya wiki mbili. Kama utahisi au kusikia mshtuko au sauti ya mgongano, tafuta msaada.
mtoto mwenye mguu ambao unaangalia ndani.
mtoto akiwa amefungwa kinyoshamguu.

Mguu uliopinda

Iwapo mguu wa mtoto ambaye ndiyo amezaliwa unaagalia ndani au una muundo usiyo sahihi (kikanyagio chake kimepinda), jaribu kuunyosha ili kuurudisha katika hali yake ya kawaida. Iwapo umeweza kufanya hivyo kwa urahisi, rudia zoezi hili mara kadhaa kila siku.Mguu (au miguu) taratibu itaelekea kwenye hali ya kawaida.Kama huwezi kuunyosha mguu wa mtoto kuurudisha katika hali ya kawaida, mpeleke kituo cha afya ndani ya siku chache baada ya kuzaliwa.Mguu wake utahitaji kunyoshwa kwa kutumia vifaa maalum. Iwapo hili litafanyika mapema, matumizi ya vifaa maalum vya kunyoosha viungo humwepusha mtoto kufanyiwa operesheni au hata ulemavu baadaye.

Vidole vya ziada mkononi au mguuni

kidole kidogo kikiwa kimefungwa kwa kuzungushiwa na kamba.

Kidole kidogo cha ziada, bila mfupa kwa ndani, kinaweza kuondolewa kwa kukizungushia kamba na kukifunga kwa nguvu . Kitakauka na kudondoka. Kama kidole hicho cha ziada ni kikubwa kuliko kawaida au kina mfupa ndani yake, hakina madhara; unaweza kukiachia kikae.

Vidole vya miguu kusongamana kama kwenye mchoro siyo tatizo.
NWTND Newb Page 8-5.png

Hata hivyo, iwapo vidole viwili au zaidi vitakuwa vimeungana kabisa, vitahitaji kutenganishwa kwa njia ya operesheni ili viweze kufanya kazi vizuri.

Uwezo dhaifu wa kuzaliwa (Down syndrome)

Upungufu ambao huathiri uwezo wa kufikiri au kujifunza unaweza kutambulika mara baada ya kuzaliwa, au baadaye mtoto anapokuwa mkubwa zaidi. Uwezo dhaifu wa kuzaliwa ni chanzo cha kawaida cha ubongo kufanya kazi polepole. Watoto wachanga wenye tatizo hili wana baadhi ya dalili zote zifuatazo:

NWTND Newb Page 9-1.png
macho yanaangalia juu
uso bapa
mcharazo mmoja tu kupita katikati ya kiganya
sikio dogo likiwa na mkunjo wa ngozi juu yake
msuli unakuwa haujafungamana vizuri
NWTND Newb Page 9-2.png
Mwanya mpana kati ya kidole cha mguu cha kwanza na cha pili.
mvulana anatembelea magogo akiwa amembeba mtoto wa kike mabegani; mtoto aliyebebwa naye amebeba bango.
Kwa kila Mtoto, Tafuta na Kuibua Vipaji Vyake

Uwezo dhaifu wa kuzaliwa (Down syndrome) hausababishwi na kitu chochote ambacho huenda mama mtoto au mtu mwingine yeyote alifanya. Hata hivyo,iwapo mwanamke mwenye zaidi ya miaka 35 atapata ujauzito, kuna uwezekano mkubwa mtoto wake atapata tatizo hili. Watoto hao huhitaji upendo na uangalizi sawa na watoto wengine,na mazoezi ya kawaida mbalimbali yanaweza kuwasaidia kujifunza. Kwa taarifa zaidi, angalia kitabu cha Hesperian kiitwacho Disabled Village Children, (Watoto Wenye Ulemavu Vijijini), sura ya 32.

Kuwahudumia watoto wenye ulemavu

Tofauti kubwa za kimaumbile ambazo husababisha matatizo kwa mtoto zinaweza kutibika nyumbani na familia kwa msaada wa mfanyakazi wa afya. Lakini huenda muhimu zaidi kuliko tiba ya kiafya, watoto wenye ulemavu huhitaji upendo, uangalizi wa karibu, muda wa kucheza, muda wa kujifunza, na kuwajibika kama watoto wengine. Tafuta zawadi na vipaji ambayo kila mtoto amekuja navyo duniani.

Njia bora zaidi ya kuwalinda watoto ni kuwatunza vizuri mama zao.


Kasoro hatari zaidi anazozaliwa nazo mtoto mchanga

Baadhi ya kasoro ambazo huzaliwa nazo mtoto ni mbaya sana kiasi kwamba husababishakifo chake. Huu unakuwa wakati mgumu sana kwa familia na jamii. Kama mfanyakazi waafya, unaweza kuisaidia familia kuzungumzia huzuni yao na pengo la kumpoteza mtoto wao.

NWTND Newb Page 10-1.png

Kumsafisha na kumvalisha mtoto

NWTND Newb Page 11-1.png
Akina mama wengi hupenda kuwalinda watoto wao dhidi ya hewa mbaya kwa kutumia nguo au blanketi nyingi. Hali hii inaweza kumfanya mtoto kusikia joto kali kupita kiasi. Nguo moja tu ya ziada ya kumfunika inatosha.

Futa damu yoyote ile na kinyesi cha kwanza cha mtoto (cheusi chenye asili ya kugandamana) lakini usimwogeshe. Baada ya siku mbili au tatu, familia imwogeshe mtoto mara kwa mara ili kusafisha maziwa, mcheuo, uchafu, na kinyesi.

Unapomvalisha mtoto, tumia nguo nyingi kama anavyohitaji mtu mzima, halafu ongeza moja ya ziada ya kumfunika. Kwa wiki yote ya kwanza au hata ya pili, mfunike mtoto kichwani kwanihupoteza joto jingi kupitia kichwani. Badilisha nguo au nepi kila mara zinapolowa au kuchafuka na kinyesi. Kama ngozi yake itaanza kuwa nyekundu au kuna upele chini ya nepi, acha sehemu hiyo wazi ili kuruhusu hali hiyo kutoweka.