Hesperian Health Guides

Kutibu tatizo la asidi nyingi tumboni, kiungulia, na vidonda vya tumbo

Maumivu tumboni, kuhara, na minyoo: Madawa

Kwanza jaribu kutibu kuingulia na tumbo kunguruma kwa kutumia dawa za kawaida za kudhibiti asidi. Kama hali hiyo itakurudia, utahitaji dawa yenye nguvu zaidi ya kudhibiti asidi. Kama maumivu ya tumbo yatakuwa yanasababishwa na kidonda cha tumbo, huenda ukahitaji kutumia dawa 2 kwa pamoja-dawa za kudhibiti asidi na antibiotiki ili kuponya tatizo. Kuhusu dawa hizo, bonyeza hapa.

Dawa za kudhibiti asidi tumboni

Dawa za kudhibiti asidi tumboni hugharimu fedha kidogo na hutoa ahueni ya muda mfupi katika kupunguza maumivu tumboni na kiungulia. Hakuna dawa kati ya hizo inayofanya kazi kwa muda mrefu, lakini husaidia kupunguza maumivu kwa muda mfupi. Huuzwa chini ya majina tofauti ya kibiashara, ikiwa katika mfumo wa maji au vidonge vya kumumunya, na hutengenezwa kutokana na alminiamu haidroksaidi (aluminum hydroxide), magnesiamu haidroksaidi (magnesium hydroxide), na kalsiamu kaboneti (calcium carbonate), au bismasi (bismuth).

Alminiamu haidroksaidi (aluminum hydroxide), magnesiamu haidroksaidi (magnesium hydroxide), milk of magnesia, cream of magnesia


Dawa hizi za kudhibiti asidi zinaweza kutumika mara moja moja kutibu tatizo la asidi tumboni na kiungulia, au kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa kutibu vidonda vya tumbo.

MuhimuNBgrnimportant.png

Dawa hizi huingiliana na tetrasaikilini na dawa kadhaa zingine. Kama unatumia dawa nyingine, subiri hadi baada ya saa 2 kabla ya kutumia dawa hizi dhidi ya asidi.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Dawa za kudhibiti asidi zenye magnesiamu wakati mwingine husababisha kuhara, na zile zenye alminiamu zinaweza kusababisha kupata choo kigumu.

Jinsi ya kutumiaNBgrnpillspoon.png

Tumia dawa ya kudhibiti asidi unapokuwa na maumivu, kawaida saa 1 baada ya kula chakula. Au tumia kabla ya kulala ili kuzuia maumivu utakapokuwa umelala. Tafuna kidonge 1 au 2, au kunywa miligramu 10 (wastani wa vijiko 2 vya chai). Ni sahihi kutumia dawa hizi mara 4 au 5 kwa siku, lakini kama unajikuta unatumia kiasi hiki kwa siku kadhaa mfululizo, huenda unahitaji aina nyingine ya tiba.

Kalsiamu kaboneti


Kalsiamu kaboneti inafanya kazi vizuri kwa matukio ya mara moja moja ya asidi(gesi) nyingi tumboni au kiungulia. Tafuna kidonge 1 cha miligramu 850 au 2 vya miligramu 350 pale dalili zinapojitokeza. Ikibidi, tumia dozi nyingine ndani ya saa 2.

Sodiamu baikaboneti, bicarbonate of soda, baking soda


Sodiamu baikaboneti (sodium bicarbonate) inapaswa kutumika mara moja moja tu kwa ajili mvurugano tumboni unaoambatana na kiungulia au asidi (gesi) nyingi. Usitumie dawa hii kutibu tatizo la ugumu wa choo la muda mrefu au vidonda vya tumbo. Ingawa mwanzoni husaidia, sodiamu baikaboneti husababisha tumbo kuzalisha asidi zaidi, ambayo baada ya muda mfupi huzidisha tatizo hilo. Kama dawa ya kudhibiti asidi au gesi tumboni ambayo itatumika kwa nadra, changanya ½ kijiko cha chai cha dawa hiyo na maji na kunywa.

Alka-Seltzer ni muunganiko wa sodiamu baikaboneti na asipirini. Kama una vidonda vya tumbo, asipirini itazidisha zaidi kidonda hicho.

MuhimuNBgrnimportant.png

Watu wenye ugonjwa wa moyo au miguu au uso uliovimba hawapaswi kutumia sodiamu baikaboneti na bidhaa zingine zenye sodamu ndani yake.

Bismasi (Bismuth)


Bismasi kawaida hupatikana katika muundo wa majimaji yenye rangi ya pinki. Hutumika kutibu kiungulia, maumivu tumboni, kuhara, au gesi (tumbo lililojaa na ambalo linauma, na kulazimika kujamba mara kwa mara). Inaweza kutumika pamoja na dawa zingine za kutibu vidonda vya tumbo. Bonyeza hapa.

Madhara ya pembeniGreen-effects-nwtnd.png

Wakati mwingine dawa hii hubadili rangi ya ulimi au kinyesi kuwa nyeusi. Hii haina madhara na hutoweka baada ya kusimamisha matumizi ya dawa hiyo.

MuhimuNBgrnimportant.png

Usitoe kwa watoto wenye homa. Kama ilivyo asipirini, inaweza kusababisha matatizo ya afya miongoni mwa watoto wenye maambukizi ya virusi.

Jinsi ya kutumiaNBgrnspoon.png

Isitumike ndani ya saa 2 baada ya kutumia tetrasaikilini. Itaingilia kati na kupunguza ufanisi wa dawa zote mbili.

Toa vidonge 2 au miligramu 30 za dawa ya maji, mara 1kwa saa kadri itakavyohitajika Usitoe zaidi ya vidonge 16 au miligramu 240 ndani ya saa 24.

Dawa zenye nguvu zaidi za kupunguza asidi tumboni

Dawa za kisasa zaidi kwa ajili ya kiungulia na vidonda vya tumbo hufanya kazi vizuri kuliko dawa za asidi za zamani, lakini huwa ni ghali zaidi. Kuna aina 2 za dawa za kisasa za kudhibiti asidi: H2 Blockers ambazo hufanya kazi kwa kuziba utendaji wa seli kwenye tumbo katika kuzalisha asidi na Proton Pump Inhibitors (PPIs) ambazo pia hupunguza kiasi cha asidi inayozalishwa na tezi kwenye ngozi ya ndani ya tumbo.

Kati ya makundi hayo 2, PPI hufanya kazi vizuri zaidi lakini ni ghali zaidi. Kwa ujumla dawa kutoka makundi hayo 2 hazina tofauti kubwa katika ubora kiutendaji. Hivyo,chagua dawa yoyote kutoka kundi moja wapo yenye gharama nafuu.

Omeprazo (Omeprazole)


Omeprazo(Omeprazole) ni aina ya PPI. Kama PPI zingine, inaweza kutuliza maumivu na kusaidia kidonda kupona. Kutibu kidonda, jaribu kutumia omeprazo peke yake kwa wiki 8. Kama kidonda na maumivu yatarudi, jaribu omeprazo tena pamoja na antibiotiki. Bonyeza hapa kwa ajili ya tiba yenye muunganiko wa dawa.

Kama hutapata matokeo mazuri kutokana na omeprazo, jaribu aina nyingine ya dawa kutoka kundi la PPI.

Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png
Toa miligramu 20 hadi 40, mara 1 kwa siku.
Anza na miligramu 20, na kama maumivu hayatapungua, ongeza dozi hadi miligramu 40.


Kama kidonda au maumivu yatarudi tena ndani ya miezi 6 baada ya kutumia omeprazo, pia tumia antibiotiki kutibu kidonda. Bonyeza hapa.

Ranitidine


Ranitidini (Ranitidine) inatoka kwenye kundi la H2 blocker. Kama zilivyo dawa zingine kwenye kundi hili, inaweza kupunguza maumivu na kusaidia kidonda kupona. Lakini kama maumivu yatarudi ndani ya miezi 6 ya kutumia ranitidini, pia tumia antibiotiki kutibu kidonda. Bonyeza hapa.

Jinsi ya kutumiaNBgrnpill.png
Toa miligramu 150 mara 2 kila siku, au miligramu 300 pamoja na chakula cha jioni, kwa wiki 4 hadi 8.

Kutibu kidonda

Toa kwa pamoja dawa za kudhibiti asidi na antibiotiki. Kuna aina nyingi ya michanganyiko ambayo hufanya kazi vizuri. Aina nyingi zinajumuisha dawa mojawapo kutoka kundi la PPI na antibiotiki 2. Mara nyingi bismasi (bismuth) nayo huongezwa. Kama huna dawa aina ya PPI, dawa kutoka kundi la H2 blocker inaweza kutumika kama mbadala.

Ifuatayo ni mchanganyiko mojawapo:
Omeprazo miligramu 40, (au aina nyingine ya PPI) mara moja kila siku kwa wiki 1 au 2
NA
Metronidazo miligramu 500, mara 2 kila siku kwa wiki 1 au 2
NA
Amoksilini miligramu 500, mara 3 kila siku kwa wiki 1 au 2.

AU, kuna mchanganyiko mwingine:

Omeprazo miligramu 40, (au aina nyingine ya PPI) mara 1 kila siku kwa wiki 1
NA
Metronidazo miligramu 250, mara 4 kila siku kwa wiki 1
NA
Tetrasaikilini miligramu 500, mara 4 kila siku kwa wiki 1
NA
Bismasi (bismuth) miligramu 525, mara 4 kila siku kwa wiki 1
Usitumie tetrasaikilini na bismasi kwa wakati mmoja. Subiri saa 2 hadi 3 baada ya kutumia dawa moja, ndiyo umeze nyingine.